2011
Sehemu Pana ya Matendo
Desemba 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Desemba 2011

Sehemu Pana ya Matendo

Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Imani • Familia • Usaidizi

Bwana, Kanisa Lake, familia na jamii wanahitaji ushawishi wa akina mama wenye haki. Hakika, Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba, “Kila dada katika Kanisa ambaye amefanya maagano na Bwana ana jukumu takatifu la kusaidia kuokoa nafsi, na kuongoza wanawake wa ulimwengu, kuimarisha nyumba za Sayuni, na kujenga ufalme wa Mungu.”1

Baadhi ya akina dada wanaweza kushangaa kama wanaweza kutimiza lengo hii kuu. Lakini, kama vile Eliza R Snow (1804–87), Rais wa Pili wa Ushirika wa Usaidizi wa kina Mama alieleza “hakuna dada aliyewekwa kando sana hata nafasi yake kuwa nyembamba, lakini yale makuu anayoweza kufanya katika kuimarisha Ufalme wa Mungu duniani.”2 Dada Snow pia alifundisha kuwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulipangwa kwa “kutimiza kazi zote njema zenye uadilifu.”3

Kushiriki katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama hupanua nafasi zetu kwa kumpa kila dada nafasi ya kujenga imani, kuimarisha familia na nyumba, na kutoa huduma nyumbani na kote ulimwenguni. Na kwa bahati njema, bidii zetu binafsi na kama Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama hazihitaji kuwa kubwa na za kutushinda, lakini ni lazima ziwe za kukusudiwa na za kuendelea. Matendo ya haki kama vile maombi ya kibinafsi na ya familia, kusoma maandiko kila siku na kuinua miito yetu kanisani kutasaidia kujenga Ufalme wa Bwana.

Kwa akina dada wanaoshangaa ikiwa mambo haya yanayoonekana kama michango mitulivu inaleta tofauti, Mzee Ballard amekubali: “Kila dada anayesimama kwa haki na utakatifu hudidimiza athari za uovu. Kila dada anayeimarisha na kutunza familia yake anafanya kazi ya Mungu. Kila dada anayeishi kama mwanamke wa Mungu huwa kielelezo kwa wengine, kufuata na hupanda mbegu zenye ushawishi takatifu ambazo zitavunwa kwa miongo inayokuja.”4

Kutoka kwa Maandiko

1 Wakorintho 12:4–18; 1 Timotheo 6:18–19; Mosia 4:27; Makala ya Imani 1:13

Kutoka kwa Historia Yetu

Eliza R Snow, ambaye alikuwa amehudumu kama mwandishi wakati Muungano wa Usaidizi wa kina Mama ulipokuwa ukipangwa huko Nauvoo, aliitwa na Rais Brigham Young (1801–77) kutembea kote katika Kanisa, kuwasaidia maaskofu kupanga Muungano wa Usaidizi wa kina Mama katika kata zao.

Dada Snow alifundisha: “Ikiwa yeyote kati ya mabinti na akina mama katika Israeli wanahisi kupungukiwa katika nafasi zao, sasa watapata nafasi ya kutosha kwa kila nguvu na uwezo wa kutenda mema kwa yale ambayo wamewezeshwa kwa vipawa. … Rais Young amegeuza ufunguo kwa upana na ukubwa wa nafasi wa matendo na utumishi.”5

Muhtasari

  1. M. Russell Ballard, “Women of Righteousness,” Liahona, Dec. 2002, 39.

  2. Eliza R. Snow, “An Address,” Woman’s Exponent, Sept. 15, 1873, 62.

  3. Eliza R. Snow, “Female Relief Society,” Deseret News, Apr. 22, 1868, 81.

  4. M. Russell Ballard, Liahona, Dec. 2002, 39.

  5. Eliza R. Snow, Deseret News, Apr. 22, 1868, 81.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Ninawezaje kuwasaidia akina dada ninaowatembelea kutenda kazi kwa uwezo wao na kuwa na ushawishi wa haki?

  2. Ninawezaje kutumia vipawa vyangu vya kipekee na talanta ili kuwabariki wengine?