2011
Ndoto ya Lehi: Kushikilia Fimbo
Oktoba 2011


“Ndoto ya Lehi: Kushikilia Fimbo,” Liahona, Okt. 2011, 32-37)

Ndoto ya Lehi

Kushikilia Fimbo

Picha
Mzee David A. Bednar

Dhamira kuu ya Kitabu cha Mormoni—kuwaalika wote kuja kwa Kristo—ni ya umuhimu mkubwa katika ono la Lehi.

Nakipenda Kitabu cha Mormoni. Baadhi ya kumbukumbu zangu za mwanzo kabisa za injili ni za usomaji wa mama yangu kwangu Hadithi za Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya Vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho, na Emma Marr Petersen. Katika zoefu hizo za utotoni na wakati wa maisha ya mafunzo binafsi yanayoendelea na maombi, Roho Mtakatifu kwa kurudia rudia ametoa ushuhuda kwenye roho yangu kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu.

Kitabu cha Mormoni ni ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo. Ninajua kwamba Nabii Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni kwa uwezo na nguvu za Mungu. Ninashuhudia leo kwamba Kitabu cha Mormoni ndicho “kitabu sahihi duniani, na ndicho jiwe la katikati la teo la dini yetu, na kuwa mwanadamu [ata] mkaribia Mungu zaidi kwa kufuata mafunzo yake, zaidi ya kitabu kingine.”1

Ishara Maalumu katika Ndoto ya Lehi

Umuhimu wa kusoma, kujifunza, kupekuwa, na kutafakari maandiko kwa ujumla na mahsusi Kitabu cha Mormoni umeonyeshwa katika ishara kadha za ono la Lehi la mti wa uzima (ona 1 Nefi 8).

Kitovu cha sehemu muhimu katika ndoto ya Lehi ni mti wa uzima—uwakilishi wa “upendo wa Mungu” (ona 1 Nefi 11:21–22). “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Hivyo, kuzaliwa, maisha, na dhabihu ya upatanisho ya Bwana Yesu Kristo ni onyesho kubwa mno la upendo wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake. Kama Nefi alivyoshuhudia, upendo huu ni “wa kupendeza zaidi ya vitu vyote” na, kama malaika katika ono lake alilvyotangaza, “inafurahisha moyo kwa shangwe” (1 Nefi 11:22–23;ona pia 1 Nefi 8:12,15) Sura ya 11 ya 1 Nefi inawakilisha maelezo ya kina ya mti wa uzima kama ishara kwa ajili ya maisha, huduma, na dhabihu ya Mwokozi—“ ufadhili wa Mungu” (1 Nefi 11:16)

Matunda katika mti ni ishara kwa baraka za Upatanisho wa Mwokozi. Kula matunda ya mti kunawakilisha kupokea kwa ibada na maagano katika hili upatanisho unaweza kuwa mkamilifu wa kufaa katika maisha yetu. Matunda yanaelezewa kama “yalitamanika kumfurahisha mtu” (1 Nefi 8:10) na yanasababisha shangwe kuu na tamaa kushiriki shangwe hiyo pamoja na wengine.

Kumaanisha, dhamira kuu ya Kitabu cha Mormoni—kuwaalika wote kuja kwa Kristo—ni ya umuhimu mkubwa katika ono la Lehi. Cha mvuto wa kipekee ni fimbo ya chuma ambayo iliongoza kwenye mti (ona 1 Nefi 8:19). Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu.

Kung’ang’ania dhidi ya Kushikilia Fimbo

Baba Lehi aliona makundi manne ya watu katika ndoto yake. Makundi matatu yalikuwa yakisonga mbele yakiambaa kwenye njia nyembamba iliyosonga wakitafuta kupata mti na matunda yake. Kundi la nne halikutafuta mti, wakitamani badala yake jengo kubwa na pana kama hatimaye mwisho wao safari yao (ona 1 Nefi 8:31–33).

Katika 1 Nefi 8:21–23 tunajifunza kuhusu kundi la kwanza la watu waliosonga mbele na walianza katika njia ambayo ilielekea kwenye mti wa maisha. Hata hivyo, wakati watu wakikabiliana na ukungu wa giza , ambalo linawakilisha “majaribio ya ibilisi” (1 Nefi 12:17, walipoteza njia yao, walizurura mbali na walipotea.

Fahamu kwamba hakuna palipotajwa katika mistari hii fimbo ya chuma. Wale ambao hawajali au kuchukulia kiwepesi neno la Mungu huwa hawana fursa kwenye ile dira takatifu ambayo inaonesha njia ya kwenda kwa Mwokozi.” Fikiria kwamba kundi hili lilipata njia na lilisonga mbele,wakionesha kipimo cha imani katika Kristo na wongofu wa kiroho, lakini walipotoshwa na majaribu ya ibilisi na walipotea

Katika 1 Nefi 8:24–28 tunasoma kuhusu kundi la pili la watu ambao walipata njia nyembamba iliyosonga ambayo ilielekea kwenye mti wa uzima. Kundi hili ‘lilisonga mbele kupitia giza la ukungu, waking’ang’ania kwenye fimbo ya chuma, hata mpaka walipotokea na kula tunda la mti’ (mstari24). Hata hivyo, wakati wakazi waliovalia kifahari wa lile jumba kubwa na pana walipowadhihaki kundi hili la pili la watu, “waliaibika” na “wakaingia katika njia zilizokataliwa na wakapotea” (mstari wa 28). … Tafadhali weka maanani kwamba kundi hili linaelezwa kama “wakishikilia fimbo ya chuma” (1 Nefi 8:24; mkazo umeongezwa).

Ni muhimu kwamba kundi la pili lilisonga mbele kwa imani na msimamo . Pia walikuwa na baraka iliyoongezwa ya fimbo ya chuma, na walikuwa wakiishikilia! Hata hivyo, wakati walipokuwa wanakabiliwa na mateso na shida, wakaingia katika njia zilizokataliwa na wakapotea. Hata pamoja na imani, msimamo, na neno la Mungu, kundi hili hatimaye lilipotea—labda kwa sababu tu baada ya kipindi fulani walisoma au walijifunza au walipekua maandiko. Kushikilia fimbo ya chuma kunapendekeza kwangu mara moja tu “mipasuko” ya mafunzo au kuchovya kusiko fuata kanuni badala ya kawaida, kuzamishwa kunakoendelea katika neno la Mungu.

“Katika mstari wa 30 tunasoma kuhusu kundi la tatu la watu waliosonga mbele “daima wameshikilia ile fimbo ya chuma, hadi wakafika na kuinama na kula matunda yaule mti.” Kishazi muhimu katika msitari huu ni daima wameshikilia fimbo ya chuma.

Kundi hili pia lilisonga mbele kwa imani na kusadiki sana; hata hivyo, hakuna ishara kwamba walizurura mbali, na wakaingia katika njia njia zilizokataliwa au walipotea. Labda kundi hili la tatu la watu kwa uaminifu walisoma na walijifunza na walipekua maandiko. Labda ilikuwa bidii na upendo kwa kilichoonekana “kidogo na rahisi [kitu]” (Alma 37:6) kilicho okoa kundi la tatu lisipotee. Labda ulikuwa “ufahamu wa Bwana” na “walielimishwa kwa ukweli” (Alma 25:5,6) uliopatikana kupitia mafunzo ya kiaminifu ya maandiko ambayo yaliacha karama ya kiroho ya unyenyekevu—kiasi kwamba kundi hili la watu “kuinama na kula matunda ya mti” (1 Nefi 8:30; msisitizo umeongezwa). Labda lilikuwa rutubisho la kiroho na nguvu vilivyotolewa kwa kuendelea “[ku]la na kusherehekea neno la Kristo” (2 Nefi 31:20) ambalo liliwezesha kundi hili kuto tilia maanani dharau na dhihaka za watu katika jumba kubwa na pana (ona 1 Nefi 8:33) Hili ni kundi ambalo wewe na mimi tunatakiwa tujitahidi kujiunga nalo.

Kaka wa Nefi waliuliza, “Nini maana ya fimbo ya chuma ambayo baba aliona, ikielekeza kwenye ule mti?

Na [Nefi] akawaambia kwamba ilikuwa neno la Mungu; na yeyote atakayesikiza hilo neno la Mungu, na alizingatie, hataangamia; wala majaribu na mishale ya moto ya adui kuwalemea na kuwapofusha, ili kuwaelekeza kwenye maangamio” (1 Nefi 15:23-24;msisitizo umeongezwa).

Kisha, ni nini, tofauti kati ya kung’ang’ania na kushikilia fimbo ya chuma? Wacha mimi nipendekeze kwamba kushikilia fimbo ya chuma kunalazimisha, kwa kiasi kikubwa, wenye maombi, daima, na matumizi ya bidii ya maandiko matakatifu kama chanzo cha uhakika cha ukweli uliooneshwa na kama mwongozo wa kuaminika kwa ajili ya safari kwenye njia iliyonyooka na kusonga kwenda kwenye mti wa uzima—hata kwa Bwana Yesu Kristo.

Na ikawa kwamba niliona ile fimbo ya chuma, ambayo baba yangu aliiona, ilikuwa neno la Mungu, na ilielekea hadi kwenye chemchemi ya maji ya uhai, au kwenye mti wa uzima” (1 Nefi 11:25).

Kitabu cha Mormoni ni kwa Ajili Yetu Leo.

Kitabu cha Mormoni kinatangaza kweli zinahusika na ambazo ni muhimu katika wakati wetu na kwa ajili ya hali zetu. Uhusuano muhimu wa kiroho na kiutendaji uhusiano wa Kitabu cha Mormoni katika wakati wetu unaoneshwa wazi na Moroni: “Tazama, ninawazungumzia kama vile mko hapa lakini hamko. Lakini tazama, Yesu Kristo amenionyesheni nyie kwangu, na ninajua yale mnayofanya” (Mormoni 8:35). Baada ya kuona wakati wetu na hali kupitia kujua kabla hakijatokea kwa Mungu, waandishi wakuu wa Kitabu cha Mormoni kwa bayana waliweka mada na mifano ya umuhimu mkubwa mno kwa wakazi wa dunia katika siku za mwisho.

Ninawaalika kufikiria kwa uangalifu na kwa maombi swali lifuatalo: ni masomo gani ninayoweza na ningeweza kujifunza kutokana na ono la Lehi la mti wa uzima na kutoka kanuni ya daima kushikilia fimbo ya chuma ambazo zitaniwezesha kusimama kiroho kwa nguvu katika ulimwengu tunaoishi leo?

Unapofanya kazi kwa bidii na kutafuta msukumo kujibu swali hili muhimu, utakuja kuelewa kwa uwazi mno kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mwote katika moyo wako na katika akili zako, umuhimu wa kuendelea kushikilia kwa nguvu kwenye fimbo ya chuma. Na utabarikiwa kutumia masomo hayo kwa imani na bidii katika maisha yako binafsi na katika nyumba yako.

Na sote tuwe na macho ya kuona na masikio ya kusikia masomo ya ziada kutoka ono la Lehi ambayo yatatusaidia “[kusonga] mbele [tu]kiwa na imani imara katika Kristo, [tu]kiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hivyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherekea neno la Kristo na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.” (2 Nefi 31:20).

Muhtasari

  1. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith (2007), 64.