2011
Ndugu, Nimejitolea
Julai 2011


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Julai 2011

Ndugu, Nimejitolea

Ndugu wawili vijana walisimama juu ya jabali ndogo lililotokea juu ya maji masafi ya ziwa buluu. Hii ilikuwa eneo la kupiga mbizi lililopendwa na wengi, na kila mara ndugu hawa waliongea kuhusu kupiga mbizi—kitendo ambacho waliona wengine wakifanya.

Ingawa wote walitaka kuruka, hakuna aliyetaka kutangulia. Urefu wa jabali haukuwa mkubwa sana, lakini kwa vijana hawa wawili, inaonekana umbali uliongezeka walipoanza kuinama mbele—na ujasiri wao ulipungua kwa haraka.

Hatimaye, ndugu mmoja aliweka mguu mmoja ukingoni mwa jabali na kusogea mbele kwa ujasiri. Kwa wakati huo ndugu yake akanong’oneza, “Pengine tungesubiri hadi msimu ujao wa joto.”

Msukumo wa ndugu yule wa kwanza hata hivyo, tayari ulikuwa unamvuta mbele. “Ndugu,” alijibu, “Nimejitolea!”

Aliporuka ndani ya maji na kuibuka haraka kwa mayowe ya shangwe. Ndugu wa pili akafuatia mara moja. Baadaye, wote wakacheka kuhusu maneno ya mwisho ya kijana wa kwanza kabla ya kutumbukia ndani ya maji: “Ndugu, Nimejitolea.”

Kujitolea ni kama kupiga mbizi majini. Ama umejitolea au la. Ama unaenda mbele au umesimama imara. Hakuna njia nusu. Sote tunakumbana na nyakati za maamuzi yanayobadilisha maisha yetu yote. Kama wafuasi wa Kanisa, lazima tujiulize, “Je nitazamia ndani ama kusimama tu ukingoni? Je, nitasongea mbele ama kuonja tu halijoto ya maji kwa vidole vya miguu yangu?”

Dhambi zingine hutendwa kwa sababu tunafanya kosa; dhambi zingine hutendwa kwa sababu hatufanyi kitu. Kujitolea kidogo kwa injili husababisha uvunjikaji wa moyo, huzuni, na hatia. Hii haifai kutugusa kwa ajili sisi ni watu wa agano. Tunaweka maagano na Bwana tunapobatizwa na tunapoingia katika nyumba ya Bwana. Wanaume huweka maagano na Bwana wanapotawazwa kwa ukuhani. Hakuna kilicho muhimu zaidi ya kuweka ahadi ambayo tumefanya na Bwana Acha tuweze kukumbuka jibu la Raeli na Lea kwake Yakobo katika Agano la Kale. Ilikuwa rahisi na dhahiri na ilionyesha kujitolea kwao: “Basi yoyote Mungu aliyokuambia, uyafanye” (Mwanzo 31:16).

Wale ambao wamejitolea kidogo wanaweza kutarajia kupokea baraka chache za ushuhuda, furaha, na amani. Madirisha ya mbinguni pengine yanaweza kufunguliwa kidogo kwao. Si itakuwa ujinga kufikiria, “Sasa nitajitolea asili mia 50, lakini wakati Kristo atakapotokea kwenye Ujio Wake wa Pili, Nitajitolea asili mia 100?”

Kujitolea kwa maagano yetu na Bwana ni tunda la uongofu wetu. Kujitolea kwa Mwokozi na Kanisa Lake hujenga sifa yetu na kuimarisha roho yetu ili tunapokutana na Kristo, Atatukumbatia na kusema, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu.” (Mathayo 25:21)

Kuna tofauti baina ya nia na tendo. Wale ambao tu wana nia ya kujitolea wanaweza kupata visingizio kila mara. Wale ambao wamejitolea dhahiri hukabiliana na changamoto zao vilivyo na kujisemeza, “Ndio, hiyo ingekeuwa sababu nzuri ya kuahirisha, lakini Nimefanya maangano, vivyo hivyo nitafanya nilichoahidi kufanya.” Wanapekua maandiko na kwa bidii wanatafuta mwongozo wa Baba yao aliye Mbinguni. Wanakubali na kupanua miito yao ya Kanisa. Wanahudhuria mikutano yao. Wanafanya mafundisho yao ya nyumbani na matembelezi.

Mithali ya Kijerumani inasema, “Ahadi ni kama mwezi mpevu. Ikiwa hazitimizwi mara moja, zinadidimia siku baada ya siku.” Kama washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tumejitolea kutembea katika njia ya ufuasi. Tumejitolea kufuata mfano wa Mwokozi wetu. Fikiri jinsi ulimwengu ungebarikiwa na kubadilishwa kwa wema wakati washiriki wote wa Kanisa la Bwana wangeishi kwa uwezo wao—kuongolewa ndani ya nafsi zao na kujitolea kujenga ufalme wa Mungu.

Kwa njia nyingine, kila mmoja wetu hujipata kwenye eneo la uamuzi linalopakana na maji. Ni ombi langu kwamba tutakuwa na imani, kusogea mbele, kukabiliana na uoga na wasiwasi wetu kwa ujasiri, na kujisemeza, “Nimejitolea!”

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

“Njia moja ya kusaidia wanaojifunza kuelewa kanuni za injili ni kuwawezesha kuchora picha. Uchoraji unawaruhusu kugundua na kudhihirisha ujuzi wao na hisia za hadithi za injili na kanuni” (Teaching, No Greater Call [1999], 166). Fikiria kusoma nakala, kujadili kanuni za kujitolea kwa injili, na kuwauliza wanaopenda kufanya hivyo kuchora picha ya shughuli ya injili inayoonyesha kujitolea. Watoto wadogo wanaweza kuhitaji maoni juu ya kile wanachohitaji kuchora.