2011
Yote Ninayoweza Kupeana
Julai 2011


Vijana

Yote Ninayoweza Kupeana

Nilikuwa na mfadhaiko kuhusu jinsi ningelipia vitu nilivyotaka kufanya msimu wa joto: madarasa, warsha, kambi za msimu wa joto, na mengeneo. Nilidhani Ningelia. Halafu nikakumbuka mambo yote ambayo nilifundishwa kuhusu kuwa na tumaini na imani katika Bwana. Niliamua kukabidhi hali hiyo katika mikono ya Bwana na kutumanini kwamba ikiwa ilikuwa ni mapenzi Yake, Yeye angepeana njia.

Haikuwa muda baada ya hiyo, mama yangu alipata hundi ambayo ilikuwa haijabadilishwa kwa fedha taslimu kutoka kwa kazi niliyofanya mapema mwaka huo, na siku ile ile iliofuata nilipata zawadi ndogo ya pesa kwenye barua kwa kupata nafasi ya pili katika mashindano. Huu ulikuwa ni ushuhuda mkubwa kwangu kwamba Mungu anaishi, kwamba Yeye ananipenda na kunijali na atanipa.

Nilijawa na shukrani na upendo kwa Baba Yangu wa Mbinguni na Mwokozi. Nilihisi kama kwamba ningalipasuka! Nilitaka sana kuonyesha jinsi nilivyoshukuru, kumtukuza Mungu vyema niwezavyo, na kushirikisha hisia hiyo. Wengine wamefanya hivi kwa kutunga wimbo, kuandika shairi, ama kuchora picha, lakini nilijihisi mpungufu kuweza kufanya mojawapo ya mambo hayo. Niligundua kitu tu ambacho ningeweza kupeana ambacho chenye sifa ya kutosha ingekuwa maisha yangu—kuweza kuwa “kielelezo kwao waaminio” (1 Timotheo 4:12), ili kupeana maisha yangu kwa Kristo. Hiyo ndio yote Anayoomba, na ndio yote Ninayoweza kupeana.