2010
Krismasi ya Umisionari
Desemba 2010


Vijana

Krismasi ya Ummisionari

Wakati wa Krismasi yangu ya pili kama mmisionari wa muda wote, mwenzi wangu nami tulikuwa tunatembelea mshiriki na familia yake ambao walikuwa wamebatizwa majuzi. Baada ya mlo mzuri wa Krismasi, tulishiriki nao ujumbe wa Krismasi.

Tuliuliza familia kuchora picha ya vitu ambavyo vinawakumbusha wao kipindi hiki, kama vile nyota, zawadi, kuzaliwa kwa Kristo, na miti ya Krismasi. Alafu tukasoma maandiko mengine, ikijumhisha 2 Nephi 19:6: “Kwani kwetu sisi mtoto amezaliwa, kwetu tumepewa mwana, na serikali itakuwa kwenye bega lake; nalo jina lake litaitwa, Ajabu, Mshauri, Mwenyezi Mungu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.” Tukaimba “Once in Royal David’s City” (Wimbo, no. 205), tukatazama sinema juu ya Kuzaliwa kwa Kristo, na tukatoa ushuhuda juu ya Yesu Kristo.

Ilikuwa Krismasi katika hali halisi, mbali kutoka kwa familia zetu na sherehe za Krismasi za kawaida, lakini tulipotoa ushuhuda juu ya Mwokozi, nilihisi upendo mwingi na shukrani kwa sababu Yake na kuzaliwa kwake zaidi ya nilivyojua mapema. Niligundua itakuwa Krismasi yangu ya mwisho katika huduma ya ummisionari wa muda wote kwa Baba yangu wa Mbinguni, lakini nafahamu kwamba Roho yake inaweza kunishuhudia mimi juu ya Mwanawe popote nilipokuwepo.