2010–2019
Nguvu ya Imani ya Kuidhinisha
Mkutano Mkuu wa Aprili 2019


Nguvu ya Imani ya Kuidhinisha

Kwa kuinua mkono wako kuidhinisha, unafanya ahadi na Mungu, ambaye hawa ni watumishi wake, kwamba utawaidhinisha.

Mara nyingi nimewasikia viongozi wa ukuhani wakitoa shukrani kwa imani ya kuidhinisha ya wale wanaowatumikia. Kutokana na hisia katika sauti zao, unajua shukrani zao ni za kina na za kweli. Azma yangu leo ni kuwasilisha shukrani za Bwana kwa kuidhinisha kwenu watumishi Wake katika Kanisa Lake. Na pia ni kuwatia moyo kutumia na kukua katika nguvu ile ya kuwaidhinisha wengine kwa imani yenu.

Kabla hamjazaliwa, mlionesha nguvu kama hiyo. Fikiria nyuma kwa kile tunachojua juu ya ulimwengu wa roho kabla ya kuzaliwa. Baba yetu wa Mbinguni alitoa mpango kwa ajili ya watoto Wake. Tulikuwepo pale. Lusiferi, ndugu yetu wa kiroho, alipinga mpango ambao ungetupatia uhuru wa kuchagua. Yehova, Mwana Mpendwa wa Baba wa Mbinguni, aliukubali mpango. Lusiferi aliongoza uasi. Sauti ya kuidhinisha ya Yehova ilishinda, na alijitolea kuwa Mkombozi wetu.

Ukweli kwamba uko katika maisha ya kufa sasa unatuhakikishia kwamba ulimuidhinisha Baba na Mwokozi. Ilichukuwa imani katika Yesu Kristo kuuidhinisha mpango wa furaha na mahali pa Yesu Kristo ndani yake wakati ulipojua kidogo tu juu ya changamoto ambazo ungekumbana nazo katika maisha ya kufa.

Imani yako kuwaidhinisha watumishi wa Mungu imekuwa kiini cha furaha yako katika maisha haya vilevile. Wakati ulipokubali changamoto ya umisionari kuomba kujua kama Kitabu cha Mormoni kilikuwa neno la Mungu, ulikuwa na imani ya kumuidhinisha mtumishi wa Mungu. Wakati ulipokubali mwaliko wa kubatizwa, ulimuidhinisha mtumishi mnyenyekevu wa Mungu.

Wakati ulipomruhusu mtu fulani aweke mikono yake juu ya kichwa chako na kusema, “Pokea Roho Mtakatifu,” ulimuidhinisha yeye kama mwenye kushikilia Ukuhani wa Melkizedeki.

Tangu siku ile, umekuwa, kwa kutumikia kwa uaminifu, umemuidhinisha kila mtu aliyepasisha ukuhani juu yako na kila aliyekutawaza kwenye ofisi katika ukuhani ule.

Mapema katika uzoefu wako wa ukuhani, kila idhinisho lilikuwa tukio rahisi la kumwamini mtumishi wa Mungu. Sasa, wengi wenu mmesogea juu kwenye sehemu ambapo kuidhinisha kunahitaji zaidi.

Mnachagua ikiwa mtawaidhinisha wote ambao Bwana anawaita—katika lolote ambalo Bwana amewaitia. Uchaguzi huo unatokea katika mikutano ulimwenguni kote. Umetokea katika mkutano huu. Katika mikutano kama hiyo, majina ya wanaume na wanawake—watumishi wa Mungu—yanasomwa, na mnaalikwa kuinua mikono yenu kuidhinisha. Mnaweza kuzuia kura zenu za kuidhinisha, au mnaweza kuonesha kwa ishara imani yenu ya kuidhinisha. Kwa kuinua mkono wako kuidhinisha, unaweka ahadi. Unaweka ahadi na Mungu, ambaye hawa ni watumishi wake, kwamba utawaidhinisha.

Hawa ni wanadamu wasio wakamilifu, kama wewe ulivyo. Kutunza ahadi zako kutahitaji imani isiyo tetereka kwamba Bwana amewaita. Kutunza ahadi hizo kutaleta pia furaha ya milele. Kutozitunza kutaleta huzuni kwako na kwa wale uwapendao—na hata upotevu zaidi ya uwezo wako wa kufikiri.

Mnaweza kuwa mmeulizwa, au mtaulizwa, ikiwa mnamuidhinisha askofu wenu, rais wa kigingi,Viongozi wenu Wakuu wenye Mamlaka, na Maafisa Wakuu wa Kanisa. Inaweza kutokea mnapotakiwa kuwaidhinisha maafisa na viongozi katika mkutano. Wakati mwingine inaweza kuwa katika usahili na askofu au rais wa kigingi.

Ushauri wangu ni kwamba ujiulize maswali hayo mwenyewe kabla, kwa umakini na wazo la maombi. Unapofanya hivyo, unaweza kutazama nyuma juu ya mawazo yako ya hivi karibuni, maneno, na vitendo. Jaribu kukumbuka na kubuni majibu utakayotoa wakati Bwana anapokusahili, ukijua kwamba kuna siku Yeye atafanya hivyo. Ungeweza kujiandaa kwa kujiuliza Mwenyewe maswali kama yafuatayo:

  1. Je, nimewahi kufikiria au kusema juu ya udhaifu wa kibinadamu kwa watu nilioahidi kuwaidhinisha?

  2. Je, nimewahi kutafuta ushahidi kwamba Bwana anawaongoza?

  3. Je, nimefuata uongozi wao kwa dhamira njema na kwa uaminifu?

  4. Je, nimewahi kuzungumza kuhusu ushahidi ninaoweza kuona kwamba wao ni watumishi wa Mungu?

  5. Je, ninasali kwa ajili ya yao mara kwa mara kwa jina na kwa hisia ya upendo?

Maswali hayo, kwa wengi wetu, yatapeleka kwenye wasiwasi kiasi na haja ya kutubu. Tumeamriwa na Mungu tusihukumu wengine bila haki, bali kwa mazoea, tunaona kwamba hilo ni gumu kuliepuka. Takribani kila kitu tunachofanya katika kufanya kazi na watu kinatupelekea sisi kuwatathmini. Na katika takribani kila kipengele cha maisha yetu, tunajifananisha na wengine. Tunaweza kufanya hivyo kwa sababu nyingi, baadhi yake za maana, bali mara nyingi zinatupeleka kuwa wakosoaji.

Rais George Q. Canon alitoa onyo ambalo ninawapa ninyi kama la kwangu mwenyewe. Ninaamini alisema ukweli: “Mungu amewachagua watumishi wake. Anastahili kama haki yake kuwashutumu, ikiwa wanahitaji shutuma. Hajaitoa kwetu binafsi kulaumu na kuwashutumu. Hakuna mtu, hata kama ana nguvu namna gani katika imani, hata kama yupo juu katika Ukuhani, anaweza kusema uovu juu ya waliopakwa mafuta na Bwana na kupata makosa kwenye mamlaka ya Mungu juu ya dunia bila kupata chuki Yake. Roho Mtakatifu atajiondoa kutoka kwa mtu yule, na atakwenda gizani. Jambo likiwa hivi, huoni jinsi ilivyo muhimu kwamba tunapaswa kuwa waangalifu?”1

Ugunduzi wangu ni kwamba waumini wa Kanisa ulimwengu kote kwa kawaida ni watiifu kati yao na kwa wale wanao wasimamia. Yapo, hata hivyo, maboresho tunayopaswa kufanya na lazima tuyafanye. Tungeweza kuinuka juu zaidi katika nguvu yetu ya kumuidhinisha kila mmoja wetu. Itachukua imani na juhudi. Hapa ni mapendekezo manne ninatoa kwa ajili yetu kufanyia kazi katika mkutano huu.

  1. Tungeweza kutambua matendo maalumu wazungumzaji wanayopendekeza na kuanza leo kuyatekeleza. Tunapofanya hivyo, nguvu yetu ya kuwaidhinisha itaongezeka.

  2. Tungeweza kusali kwa ajili yao wanapozungumza kwamba Roho Mtakatifu apeleke maneno yao kwenye mioyo ya watu maalumu tunaowapenda. Wakati tunapogundua baadae kwamba sala yetu ilijibiwa, nguvu yetu ya kuwaidhinisha viongozi hao itaongezeka.

  3. Tungeweza kusali kwamba wazungumzaji maalumu wabarikiwe na kukuzwa wanapotoa jumbe zao. Wakati tunapoona kwamba walikuzwa, tutakua katika imani yetu kuwaidhinisha, na itadumu.

  4. Tungeweza kusikiliza jumbe kutoka kwa wazungumzaji ambazo zinakuja kama jibu kwa sala zetu binafsi kwa ajili ya msaada. Wakati majibu yanapokuja, na yatakuja, tutakua katika imani yetu kuwaidhinisha watumishi wote wa Bwana.

Kwa kuongezea kwenye uboreshaji katika kuwaidhinisha wale wanao hudumia katika Kanisa, tutajifunza kwamba kuna mahala pengine ambapo tunaweza kukua katika nguvu hiyo. Huko, inaweza kuleta hata baraka kubwa mno kwetu. Ipo katika nyumba na familia.

Ninazungumza na kijana mdogo mwenye ukuhani anayeishi katika nyumba pamoja na baba yake. Acha niwaambieni kutoka uzoefu wangu mwenyewe kile inachomaanisha kwa baba kuhisi idhinisho lako la imani. Anaweza kuonekana mwenye kujiamini kwako. Lakini anakabiliana na changamoto nyingi kuliko unavyojua. Wakati mwingine hawezi kuona njia ya kuyapita matatizo mbele yake.

Kuvutiwa kwako kwake kutamsaidia kiasi. Upendo wako kwake utasaidia hata zaidi. Lakini kitu ambacho kitasaidia zaidi ni maneno ya kweli kama haya: “Baba, nimesali kwa ajili yako, na nimehisi kwamba Bwana atakusaidia. Kila kitu Kitafanikiwa. Najua itakuwa hivyo.”

Maneno kama hayo pia yana nguvu katika mwelekeo mwingine, baba kwa mtoto. Wakati mwana amefanya kosa kubwa, pengine hata katika mambo ya kiroho, anaweza kuhisi kwamba ameshindwa. Kama baba yake, katika wakati ule, unaweza kushangazwa wakati, baada ya kusali kujua nini cha kufanya, Roho Mtakatifu anaweka maneno haya kwenye mdomo wako: “Mwana, nipo pamoja nawe wakati wote. Bwana anakupenda. Kwa msaada wake, unaweza kurudi. Ninajua kwamba unaweza na kwamba utarudi. Ninakupenda.”

Katika akidi ya ukuhani na katika familia, ongezeko la imani kumuidhinisha kila mmoja ni njia ambayo tunaijenga Sayuni Bwana anayotutaka tujenge. Kwa msaada Wake tunaweza, na tutaweza. Itachukuwa kujifunza kumpenda Bwana kwa moyo wetu wote, uwezo, akili, na nguvu na kupendana kama tunavyojipenda wenyewe.

Tunapokua katika upendo huo msafi wa Kristo, mioyo yetu hulainika. Upendo huo utatunyenyekeza na kutuongoza kutubu. Kujiamini kwetu katika Bwana na katika kila mmoja wetu kutakua. Na kisha tutasonga mbele kwenye kuwa wamoja, kama Bwana anavyoahidi tunaweza kuwa.2

Ninashuhudia kwamba Baba wa mbinguni anawajua na anawapenda. Yesu ni Kristo aliye hai. Hili ni kanisa Lake. Tunashikilia ukuhani Wake. Ataheshimu juhudi zetu za kukua katika nguvu yetu ya kuutumia na kuidhinishana sisi kwa sisi. Ninashuhudia hivyo katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.