2010–2019
Mpaka Tutakapokutana Tena
Oktoba 2014


Mpaka Tutakapokutana Tena

Na sisi sote tutafakari kweli tulizosikia, na ziweze kutusaidia kuwa hata wafuasi jasiri zaidi.

Ndugu na kina dada, tumepata uzoefu wa siku mbili tukufu za jumbe za kuinua. Mioyo yetu imeguswa na imani yetu imeimarishwa tuliposhiriki roho ambayo imekuwa hapa wakati wa hivi vikao vya mkutano mkuu. Tunapohitimisha, tunamshukuru Baba yetu wa Mbinguni kwa baraka zake nyingi kwetu.

Tumeinuliwa na kupata maongozi kwa muziki mtamu ambao umetolewa wakati wa vikao hivi. Sala ambazo zimetolewa zimetuvuta karibu na mbinguni.

Acheni mimi nitoe shukrani za moyoni za Kanisa lote kwa Ndugu zetu ambao wameachiliwa katika mkutano huu. Tutawakosa. Mchango wao kwa kazi ya Bwana umekuwa mkubwa sana na utahisiwa katika vizazi vyote vinavyokuja.

Na turudi nyumbani kwetu na azimio katika mioyo yetu la kuwa bora zaidi kuliko tulivyokuwa katika siku zilizopita. Na tuwe wakarimu kidogo zaidi na kuwa wenye kuwafikira wengine. Na tuwafikie kwa usaidizi, siyo tu washiriki wenzetu bali pia wale ambao si wa imani yetu. Tunapoingiliana nao, na tuweze kuonyesha heshima yetu kwao.

Kuna wale wanaotaabika kila siku na changamoto. Acheni tuwanyoshee kujali kwetu, pamoja na mkono wa usaidizi. Tunapojaliana mmoja na mwingine, tutabarikiwa.

Na tuwakumbuke wakongwe na wale wasiojiweza kutoka nyumbani. Tunapochukua muda wa kuwatembelea, watajua kwamba wao wanapendwa na kuthaminiwa. Na tufuate jukumu la “wasaidie wadhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na yaimarishe magoti yaliyo dhaifu.”1

Na sisi tuwe watu waaminifu na waadilifu, tukijaribu kufanya kile kilicho sahihi wakati wote na katika mazingira yote. Na tuwe wanafunzi waaminifu wa Kristo, mifano ya wema, basi kuwa nuru za ulimwengu.”2

Ndugu na dada zangu, nawashukuru kwa maombi yenu kwa niaba yangu. Yaliniimarisha na kuniinua nilivyokuwa ninajitahidi kwa moyo wangu na nguvu kutenda mapenzi ya Mungu na kumtumikia Yeye na kuwatumikia ninyi.

Tunapoondoka kutoka kwa mkutano huu, nawaombeeni baraka za mbinguni juu kila mmoja wenu. Na ninyi ambao mko mbali kutoka nyumbani kwenu mrudi huko salama na mpate mambo yote yakiwa swari. Na sisi sote tutafakari kweli tulizosikia, na ziweze kutusaidia kuwa hata wanafunzi jasiri sana kuliko tulivyokuwa kabla mkutano huu kuanza.

Mpaka tutakapokutana tena katika miezi sita, naomba baraka za Bwana ziwe juu yenu na, kwa kweli juu yetu sote, na ninafanya hivyo katika jina Lake takatifu---hata Yesu Kristo, Bwana na Mwokozi wetu---amina.