Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Ufuasi: Nini na Jinsi Gani
Januari 2024


“Ufuasi: Nini na Jinsi Gani,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan. 2024.

Ufuasi: Ni nini na Jinsi Gani

Ili kujua hakika wewe ni nani na unaweza kuwa wa namna gani, shikilia vyote nini na jinsi gani za kuwa mfuasi wa Yesu Kristo.

Picha
alt text

Pakua PDF

“Mimi ni Nani?”

Ni swali ambalo vijana wengi hutafuta majibu pia. Kadiri unavyokua na kujifunza na kuongezeka katika njia yako ya kipekee, kawaida utajiuliza ni kipi hukutambulisha, kipi hukupa utambulisho wako. Rais Russell M. Nelson alitoa mwongozo mzuri kuhusu swali hili:

“Wewe ni nani? Kwanza na zaidi ya yote,wewe ni mwana wa Mungu, mwana wa agano na mfuasi wa Yesu Kristo. Kadri unavyokumbatia kweli hizi, Baba yetu wa Mbinguni atakusaidia kufikia lengo lako kuu la kuishi milele katika uwepo Wake mtakatifu.”(“Choices for Eternity” [worldwide devotional for young adults, May 15, 2022], broadcasts.ChurchofjesusChrist.org).

Rais Nelson alifundisha kwamba hakuna alama zingine zinazopaswa kuwa muhimu kwako kuliko vichwa hivi vitatu vya utambulisho: (1) mwana wa Mungu,(2) mtoto wa agano na (3) mfuasi wa Yesu Kristo.

Utambulisho wa Mfuasi

Hebu tuongelee kidogo zaidi utambulisho huu wa tatu, mfuasi wa Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani unakumbatia utambulisho huu na kuwa mfuasi?

Ili kumfuata Mwokozi na kuwa mfuasi Wake, unahitaji kuzingatia vyote nini unafanya na jinsi gani unafanya.

Kwa mfano, Mwokozi anatutaka kutoa kwa wengine na kuwatumikia, ila Anatukaribisha kufanya hivyo kwa utashi na kwa furaha kuliko kwa kinyongo. Wakati tunapotaka kutoa na kutumikia, tunapokea zawadi kubwa ya kuwa wafuasi wa kweli. (Ona 2 Wakorinto 9:7; Moroni 7:8.)

Hivyo, hebu tuangalie nini wafuasi hufanya na jinsi gani hufanya.

Nini Mfuasi Hufanya

Hapa kuna machache kati ya mengi ambayo mfuasi wa Kristo anaweza kufanya ili kumfuata Mwokozi.

  • Kuwa mwenye imani kama wafuasi wanavyotumia imani.

  • Kutumikia kama wafuasi wanavyotumikia.

  • Kusali kama wafuasi wanavyosali.

  • Kujifunza kama wafuasi wanavyojifunza.

  • Kutubu kama wafuasi wanavyotubu.

  • Kufikiri kama wafuasi wanavyofikiri.

  • Kumpenda Mungu kama wafuasi wanavyompenda Mungu.

  • Kuwapenda wengine kama wafuasi wanavyowapenda wengine.

  • Kufundisha kama wafuasi wanavyofundisha.

  • Kuvumilia kwama wafuasi wanavyovumilia.

Jinsi Gani kama Mfuasi hufanya

Hapa kuna maelekezo ya namna mfuasi anavyoweza kufanya mambo haya. Mengi ya maelekezo yanaweza kutumika kati ya mengi ya mambo haya. Baadhi yake yanaweza kutumika kwa yote.

  • Kwa mioyo na akili zilizoelekezwa kwa Yesu Kristo

  • Kwa utayari

  • Kwa unyenyekevu

  • Kwa upendo

  • Kwa uadilifu

  • Mara kwa mara

  • Kwa moyo wote

  • Kwa bidii

  • Kwa moyo wa dhati

  • Bila chuki au kinyongo

  • Kwa uvumilivu

  • Kwa nguvu

  • Kwa ujasiri

  • Ukizingatia mahitaji ya wengine

  • Ukizingatia maandiko

  • Bila kutetereka

  • Kwa wema

  • Kwa kujawa matumaini

  • Kwa hamu ya kuwa kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

  • Bila uharibifu

Unaweza kufaidika kutokana na kufikiria vyote nini unafanya kumfuata Mwokozi na jinsi gani unavyofanya. Ikiwa unahisi unahitaji kufanya mabadiliko fulani kati ya vipengele hivi, hilo ni jambo zuri. Inaweza kuwa Roho anakusukuma kuwa mfuasi bora zaidi.

Utambulisho wa Kuukumbatia na Kuuthamini

Kama Rais Nelson alivyosema, kuwa mfuasi wa Yesu Kristo ni sehemu muhimu ya utambulisho wako. Kadiri unavyokumbatia na kutafuta utambulisho huu, Baba yako wa Mbinguni atakusaidia kuwa mtu ambaye Yeye anajua utakuwa—mtu ambaye, kwa dhati, unataka kuwa.