Kufundisha na Kujifunza
Kwa Ajili ya Viongozi—Kuwaelekeza na Kuwasaidia Walimu


“Kwa Ajili ya Viongozi—Kuwaelekeza na Kuwasaidia Walimu,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Kuwaelekeza na Kuwasaidia Walimu,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

watu wakizungumza

Kwa Ajili ya Viongozi—Kuwaelekeza na Kuwasaidia Walimu

Kama kiongozi, unalo jukumu la “kukutana na walimu wapya walioitwa” katika kikundi chako na “kuwasaidia kujiandaa kwa ajili ya miito yao” (Kitabu cha Maelekezo ya Jumla, 17.3, Gospel Library). Mikutano hii ni fursa ya kuwatambulisha walimu hao wapya kwenye miito yao mitakatifu na kuwahamasisha kwa ono la kile inachomaanisha kufundisha katika njia ya Mwokozi. Kama kiongozi, unaweza kuwasaidia walimu wapya kujiandaa kutumikia kwa kufanya mambo yafuatayo:

  • Elezea kujiamini kwamba Mwokozi atawasaidia katika wito wao (ona Mafundisho na Maagano 88:78).

  • Wape walimu wapya nakala ya nyenzo hii, na kuwahimiza kutafuta njia za kutumia kanuni zake katika kufundisha.

  • Shiriki na walimu wapya kitu cho chote kuhusu kikundi chako ambacho kitakuwa msaada kwao kujua.

  • Kadiri inavyohitajika, waambie walimu wapya ni chumba gani watakachotumia kufundisha na somo watakaloanza nalo. Toa taarifa yo yote wanayohitaji kuhusu darasa lao na washiriki wa darasa hilo.

  • Waelezee walimu wapya kwamba unaweza kuwasaidia katika wito wao. Toa msaada darasani na kwa upatikanaji wa nyenzo kama itahitajika.

  • omba kuangalia madarasa ya walimu mara kwa mara, na toa mrejesho kadiri utakavyoongozwa na Roho.

  • Waalike walimu kushiriki katika mikutano ya robo mwaka ya baraza la mwalimu.

Katika huduma yote ya walimu, endelea kukutana nao mara kwa mara ili kutoa msaada endelevu. Kwa mfano, ungeweza kuwa na majadiliano ya muda mfupi na mwalimu kabla au baada ya darasa ili kujadili kanuni za Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi. Muulize mwalimu kuhusu kitu gani wanahisi wanafanya vizuri na njia ambazo wangependa kuboresha. Watie moyo kwa ukarimu na kwa shukrani kwa huduma wanayotoa.

Unatakiwa kujiandaa kwa majadiliano haya kwa kumwangalia mwalimu akifundisha. Tafuta kuelewa vyema nguvu ya mwalimu na gundua jinsi unavyoweza kumpatia msaada. Kujenga juu ya nguvu za mwalimu ni muhimu kama ilivyo kutambua fursa za uboreshaji.