Sura ya 7
Mamajusi
Mamajusi fulani waliishi katika nchi nyingine. Walijua kile ambacho manabii walikuwa wamesema kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Walipoiona nyota mpya angani, walijua kwamba mfalme mpya alikuwa amezaliwa.
Mathayo 2:1–2
Mamajusi walienda kumwona Herode, mfalme wa Wayahudi, huko Yerusalemu. Walimuuliza wapi mfalme mpya alipokuwa. Herode aliwaambia wakatafute Bethlehemu. Watakapompata mtoto wangerudi na kumwambia Herode.
Mathayo 2:1–2, 8
Mamajusi walienda Bethlehemu na kumpata Yesu. Walimwabudu na kumpa zawadi. Waliambiwa katika ndoto wasirudi Yerusalemu na kumwambia Herode wapi alipo mtoto. Hawakurudi.
Mathayo 2:11–12