Historia ya Kanisa
Maelezo ya Ono la Kwanza


Picha
Mwangaza wa jua upenyao kwenye miti

Maelezo ya Ono la Kwanza

Maelezo ya jumla

Joseph Smith aliandika kwamba Mungu Baba na Yesu Kristo walimtokea katika kijisitu cha miti karibu na nyumba ya wazazi wake magharibi mwa Jimbo la New York alipokuwa na umri wa miaka 14. Akihangaika na dhambi zake na hakujua njia ipi ya kiroho ya kufuata, Joseph alitafuta mwongozo kwa kuhudhuria mikutano, kusoma maandiko, na kusali. Kama jibu, alipokea mafunuo ya mbinguni. Joseph alishiriki na kuhifadhi Ono la Kwanza, kama ilivyokuja kujulikana, mara kadhaa; aliandika au kuwapa waandishi kuandika maelezo ya aina nne tofauti ya maono hayo.

Joseph Smith alichapisha maelezo ya aina mbili ya Ono la Kwanza wakati wa uhai wake. Maelezo ya kwanza, yanayojulikana leo kama Joseph Smith—Historia, yalifanywa katika Lulu ya Thamani Kuu na kwa hivyo yakawa maelezo yaliyojulikana zaidi. Maelezo ya aina mbili ambayo hayakuchapishwa, yalirekodiwa kwenye kitabu cha zamani cha historia binafsi cha Joseph Smith na baadae shajara, ambayo kwa ujumla yalisahaulika hadi wanahistoria waliofanya kazi kwa ajili ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho walipoyapata tena na kuyachapisha katika miaka ya 1960. Kuanzia wakati huo, nyaraka hizi zimejadiliwa mara kwa mara katika magazeti ya Kanisa, katika kazi zilizochapishwa na vyombo vinavyomilikiwa na washirika wa uchapishaji wa Kanisa, na Watakatifu wasomi wa Siku za Mwisho katika sehemu zingine.1 Kwa kuongezea kwenye maelezo ya awali, pia kuna maelezo ya aina tano ya ono la Joseph Smith yaliyorekodiwa na wenzake kwa wakati huo.2

Maelezo mbalimbali ya Ono la Kwanza yanasimulia hadithi thabiti, ingawa kwa asili hutofautiana kwa msisitizo na undani wa maelezo. Wanahistoria wanatarajia kwamba wakati mtu anaelezea tena na tena uzoefu katika mazingira mbalimbali kwa wasikilizaji tofauti kwa miaka mingi, kila maelezo yatasisitiza mambo mbalimbali ya uzoefu na kuwa na ukina wa kipekee. Kwa kweli, tofauti zinazofanana na zile za maelezo ya Ono la Kwanza yapo katika maelezo kadhaa ya kimaandiko ya ono la Paulo akiwa njiani kuelekea Dameski na uzoefu wa Mitume kwenye Mlima wa Kugeuka Sura.3 Walakini licha ya tofauti hizo, mlingano wa kimsingi unabaki katika maelezo yote ya Ono la Kwanza. Wengine wamesema kimakosa kuwa tofauti yoyote katika usimulizi wa hadithi ni ushahidi wa uzushi. Kinyume chake, rekodi tajiri ya kihistoria inatuwezesha kujifunza zaidi juu ya tukio hili lisilo na kifani kuliko tunavyoweza ikiwa haikuandikwa kwa wingi.

Maelezo juu ya Ono la Kwanza

Kila maelezo ya Ono la Kwanza la Joseph Smith na watu wa enzi yake yana historia na muktadha wake ambayo yaliathiri jinsi tukio hilo lilivyokumbukwa, kuwasilishwa, na kurekodiwa. Maelezo haya yamejadiliwa hapa chini.

Maelezo ya mwaka 1832. Maelezo ya kwanza kabisa ya Ono la Kwanza, maelezo pekee yaliyoandikwa kwa mikono yake mwenyewe Joseph Smith, hupatikana katika nakala fupi ya historia yake, ambayo hayakuchapishwa ambayo Joseph Smith aliyatoa katika nusu ya pili ya mwaka 1832. Katika maelezo hayo, Joseph Smith alielezea ufahamu wa dhambi zake mwenyewe na kufadhaika kwake kwa kukosa kupata kanisa linalofanana na lile alilosoma katika Agano Jipya na ambalo lingempeleka kwenye ukombozi. Alisisitizia Upatanisho wa Yesu Kristo na ukombozi wa kibinafsi ambao ulitolewa. Aliandika kwamba “Bwana” alimtokea na kumsamehe dhambi zake. Kama matokeo ya ono, Joseph alipata furaha na upendo, ingawa, kama alivyoona, hakupata mtu yeyote ambaye aliamini maelezo yake. Soma maelezo ya mwaka 1832 hapa.

Maelezo ya mwaka 1835. Katika majira ya kuanguka majani ya mwaka 1835, Joseph Smith aliandika Ono lake la Kwanza kwa Robert Matthews, mgeni huko Kirtland, Ohio. Nakala hiyo, iliyorekodiwa katika shajara ya Joseph na mwandishi wake Warren Parrish, inasisitiza jaribio lake la kugundua ni kanisa gani lilikuwa sahihi, upinzani aliouhisi alipokuwa akiomba, na kuonekana kwa mtu mmoja wa kiungu ambaye alifuatiwa na mtu mwingine muda mfupi. Maelezo haya pia yanabainisha kutokea kwa malaika katika ono.. Soma maelezo ya mwaka 1835 hapa.

Maelezo ya mwaka 1838. Simulizi ya Ono la Kwanza linalojulikana zaidi kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho leo ni maelezo ya mwaka 1838. Yalichapishwa kwanza mnamo mwaka 1842 katika Times and Seasons, gazeti la Kanisa huko Nauvoo, Illinois, maelezo hayo yalikuwa sehemu ya historia ndefu iliyotolewa na Joseph Smith kati ya vipindi vya upinzani mkali. Wakati maelezo ya mwaka 1832 yanasisitiza hadithi ya kibinafsi zaidi ya Joseph Smith kama kijana anayetafuta msamaha, maelezo ya mwaka 1838 yanazingatia ono kama mwanzo wa “kukua na kuendelea kwa Kanisa.” Kama maelezo ya mwaka 1835, swali kuu la hadithi ni kanisa lipi ni la kweli. Soma maelezo ya mwaka 1838 hapa.

Maelezo ya mwaka 1842. Yaliandikwa kama jibu kwa John Wentworth mhariri ambaye alikuwa mwanachama wa Chicago Democrat aliyeomba taarifa kuhusu Watakatifu wa Siku za Mwisho, maelezo haya yalichapishwa katika gazeti la Times and Season mwaka 1842. (“Barua ya Wentworth,” kama kawaida inavyojulikana, pia ni chanzo cha Makala ya Imani.)4 Maelezo hayo, yaliyokusudiwa kuchapishwa kwa hadhira isiyojua imani za Wamormoni, ni mafupi na ya moja kwa moja. Kama ilivyo kwa maelezo ya hapo awali, Joseph Smith alibaini mkanganyiko alioupata na kuonekana kwa watu wawili kama jibu la ombi lake. Mwaka uliofuata, Joseph Smith alituma maelezo haya na marekebisho madogo kwa mwanahistoria aliyeitwa Israel Daniel Rupp, ambaye aliichapisha kama sura katika kitabu chake, He Pasa Ekklesia [The Whole Church]: Historia ya Asili ya Madhehebu ya Dini Yaliyopo Marekani Hivi Sasa.5 Soma maelezo ya mwaka 1842 hapa.

Maelezo ya Pili. Mbali na haya maelezo kutoka kwa Joseph Smith mwenyewe, maelezo matano yaliandikwa na watu waliomsikia Joseph Smith akiongea juu ya ono hilo.. Soma haya maelezo hapa.

Hoja Kuhusu Maelezo ya Ono la Kwanza la Joseph Smith

Aina na idadi ya maelezo ya Ono la Kwanza imesababisha wakosoaji wengine kuhoji ikiwa maelezo ya Joseph Smith yanaendana na ukweli wa uzoefu wake. Hoja mbili zinaletwa mara kwa mara dhidi ya uaminifu wake: maswali ya kwanza yanahoji kumbukumbu ya Joseph Smith ya matukio hayo; maswali ya pili yanahoji ikiwa alipamba matukio ya hadithi kwa kigezo cha muda.

Kumbukumbu. Hoja moja kuhusu maelezo ya Ono la Kwanza la Joseph Smith inadai kwamba ushahidi wa kihistoria hauungi mkono maelezo ya Joseph Smith juu ya uamsho wa kidini huko Palmyra, New York, na maeneo yake ya karibu mnamo mwaka 1820. Wengine wanahoji kwamba hii inadhoofisha madai ya Joseph Smith ya hamasa isiyo ya kawaida ya kidini na maelezo ya ono lenyewe.

Ushahidi uliohifadhiwa wa kimaandishi, hata hivyo, unaunga mkono taarifa za Joseph Smith kuhusu uamsho. Eneo alilokuwa akiishi likaja kuwa maarufu kwa hamasa ya kidini na bila shaka ilikuwa moja ya kichocheo cha uamsho wa kidini. Wanahistoria wanataja mkoa huo kama “wilaya iliyochomwa moto” kwa sababu wahubiri walichosha ardhi wakifanya uamsho wa makambi na kutafuta waongofu mwanzoni mwa miaka ya 1800.6 Mnao Juni 1818, kwa mfano, mkutano wa kambi ya Wamethodisti ulifanyika huko Palmyra, na msimu uliofuata wa kiangazi, Wamethodisti walikusanyika tena huko Vienna (sasa Phelps), New York, maili 15 kutoka shamba la familia ya Smith. Shajara za mhubiri wa Kimethodisti anayesafiri zinatoa historia ya msisimko mwingi wa kidini katika eneo la kijiografia la Joseph mnamo mwaka 1819 na 1820. Wanaripoti kwamba Padri George Lane, mhubiri wa Kimethodist wa uamsho, alikuwa katika mkoa huo katika miaka yote miwili, akiongea “juu ya njia ya Mungu katika kuleta Mageuzi.”7 Ushahidi huu wa kihistoria ni sawa na maelezo ya Joseph. Alisema kuwa msisimko usio wa kawaida wa kidini katika wilaya yake au mkoa “ulianza na Wamethodisti.” Kwa kweli, Joseph alisema kwamba alikuwa “ kwa sehemu fulani” kwenye Umethodisti.8

Mapambo. Hoja ya pili iliyotolewa mara kwa mara juu ya maelezo ya Ono la Kwanza la Joseph Smith ni kwamba alipamba hadithi yake kwa kigezo cha muda. Hoja hii inazingatia maelezo mawili: idadi na utambulisho wa viumbe wa mbinguni ambao Joseph Smith alisema kwamba aliwaona. Maelezo ya Ono la Kwanza la Joseph yanaelezea viumbe wa mbinguni kwa undani zaidi kwa wakati. Maelezo ya mwaka 1832 yanasema, “Bwana alinifungulia mbingu na nikamwona Bwana.” Maelezo yake ya mwaka 1838 yanasema, “Niliwaona Viumbe wawili,” mmoja wao akamtambulisha mwingine kama “Mwanangu Mpendwa.” Kama matokeo, wakosoaji wamesema kwamba Joseph Smith alianza kuripoti kumwona kiumbe mmoja—“Bwana”—na kuishia kudai kuwa amewaona wote Baba na Mwana.9

Kuna njia zingine, thabiti zaidi za kuona ushahidi. Mwafaka wa kimsingi katika masimulizi yanayolenga suala la muda lazima ukubaliwe tangu mwanzo: maelezo ya aina tatu kati ya hayo manne yanasema wazi kwamba watu wawili walimtokea Joseph Smith katika Ono la Kwanza. Ono la tofauti ni maelezo ya Joseph Smith ya mwaka 1832, ambayo yanaweza kusomwa kurejelea mtu mmoja au wawili. Kama likisomwa kumaanisha mtu mmoja wa mbinguni, inawezekana ni kwa mtu ambaye alimsamehe dhambi zake. Kulingana na maelezo ya baadaye, mtu wa kwanza wa kimungu alimwambia Joseph Smith “amsikilize” wa pili, Yesu Kristo, ambaye baadaye alitoa ujumbe mkuu, ambao ulijumuisha ujumbe wa msamaha.10 Maelezo ya Joseph Smith ya mwaka 1832, basi, yanaweza kuwa yalilenga kwa Yesu Kristo, mbebaji wa msamaha.

Njia nyingine ya kusoma maelezo ya mwaka 1832 ni kwamba Joseph Smith alitaja viumbe wawili, ambao wote aliwaita “Bwana.” Hoja ya kupamba maneno inategemea dhana ya kwamba maelezo ya mwaka 1832 yanaelezea kuonekana kwa mtu mmoja tu wa kiungu. Lakini maelezo ya mwaka 1832 hayasemi kwamba kiumbe mmoja tu alionekana. Kumbuka kuwa marejeleo mawili ya “Bwana” yametengwa kwa wakati: kwanza “Bwana” anafungua mbingu; ndipo Joseph Smith anamwona “Bwana.” Usomaji huu wa maelezo ni sawa na maelezo ya Joseph ya mwaka 1835, ambayo mtu mmoja anaonekana kwanza, ikifuatiwa na mwingine punde hapo baadaye. Maelezo ya mwaka 1832, basi, yanaweza kusomwa kwa busara kumaanisha kwamba Joseph Smith aliona kiumbe ambaye baadaye alimfunua mwingine na kwamba aliwataja wote wawili kama “Bwana”: “Bwana alifungua mbingu juu yangu na nikamwona Bwana.”11

Ufafanuzi maalum wa Joseph kwa hivyo unaweza kusomwa kwa nguvu kama ushahidi wa kuongezeka kwa ufahamu, ukiongezeka kulingana na muda, ukizigatia na uzoefu. Kwa sehemu, tofauti kati ya maelezo ya mwaka 1832 na maelezo ya baadaye yanaweza yakawa yanahusisha tofauti kati ya maneno yaliyoandikwa na maneno yaliyosemwa. Maelezo ya mwaka 1832 yanawakilisha jaribio la mara ya kwanza la Joseph Smith alipojaribu kuandika historia yake. Mwaka huo huo, alimwandika rafiki ambaye alihisi amefungwa na “kalamu ya karatasi na Wino na Lugha iliyopotoka iliyotawanyika na isiyo kamilifu.” Aliyaita maandishi “gereza dogo jembamba.”12 Upanuzi wa maelezo ya baadaye unaeleweka kwa urahisi zaidi na hata kutarajiwa wakati tunapogundua kwamba yalikuwa ni maelezo yaliyotamkwa—njia rahisi, isiyo na kikwazo kwa Joseph Smith na ile iliyoruhusu maneno kutiririka kwa urahisi zaidi.

Hitimisho

Joseph Smith alishuhudia tena na tena kwamba alipokea ono lisilo na kifani la Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo. Si ukweli wa Ono la Kwanza wala hoja dhidi yake zinaweza kuthibitishwa na utafiti wa kihistoria pekee. Kujua ukweli wa ushuhuda wa Joseph Smith kunahitaji kila anayetafuta ukweli kwa bidii kusoma rekodi na kisha kutumia imani ya kutosha katika Kristo kumuuliza Mungu kwa sala ya dhati, na ya unyenyekevu ikiwa kumbukumbu hiyo ni ya kweli. Ikiwa mtafutaji anauliza kwa nia halisi ya kuchukua hatua juu ya jibu lililofunuliwa na Roho Mtakatifu, ukweli wa ono la Joseph Smith utadhihirika. Kwa njia hii, kila mtu anaweza kujua kwamba Joseph Smith alizungumza kwa uaminifu wakati alipotangaza, “Niliona ono, nilijua hivyo, na nilijua kwamba Mungu alijua, na siwezi kukataa.”13

Kanisa linatambua mchango wa wasomi kwenye maudhui ya kihistoria yaliyowasilishwa katika makala hii; kazi yao hutumiwa kwa idhini.

Awali yalichapishwa Novemba 2013

Mada Husika

  • Kujibu Maswali ya Injili

  • Uungu

  • Mungu Baba

  • Yesu Kristo

  • Joseph Smith

  • Urejesho wa Kanisa

  • Urejesho wa Ukuhani

Maandiko Matakatifu

Kumbukumbu ya maandiko

Jumbe kutoka kwa Viongozi wa Kanisa

Video

“Urejesho”

“Joseph Smith: Nabii wa Urejesho”

“Wimbo wa Maandalizi ya Misheni Namba 14: Gordon B. Hinckley”

Nyenzo za Kujifunzia

Nyenzo za Jumla

History, circa Summer 1832,” The Joseph Smith Papers

Journal, 1835–1836,” The Joseph Smith Papers

History, circa June 1839–circa 1841 [Draft 2],” The Joseph Smith Papers

‘Church History,’ 1 March 1842,” The Joseph Smith Papers

‘Latter Day Saints,’ 1844,” The Joseph Smith Papers

Primary Accounts of Joseph Smith’s First Vision of Deity,” The Joseph Smith Papers

Magazeti ya Kanisa

Preparing for the Restoration,” Ensign, June 1999

Book of Mormon Personalities Known by Joseph Smith,” Ensign, December 1983

Vitabu vya Kiada vya Kujifunzia

  1. Ona, kwa mfano, James B. Allen, “Maelezo ya Aina Nane ya Kisasa ya Ono la Kwanza — Je, Tunajifunza Nini Kutoka Kwayo?” Improvement Era, 73 (1970): 4–13; Richard L. Anderson, “Joseph Smith’s Testimony of the First Vision,” Ensign, Apr. 1996, 10–21; Milton V. Backman, Joseph Smith’s First Vision: The First Vision in Its Historical Context (Salt Lake City: Bookcraft, 1971; 2nd ed., 1980); Steven C. Harper, Joseph Smith’s First Vision: A Guide to the Historical Accounts (Salt Lake City: Deseret Book, 2012).

  2. Maelezo haya yote yalichapishwa tena katika Dean C. Jessee, “Maelezo ya Mwanzo yaliyohifadhiwa ya Ono la Kwanza la Joseph Smith,” katika John W. Welch, ed., Na Erick B. Carlson Opening the Heavens: Accounts of Divine Manifestations, 1820–1844 (Provo and Salt Lake City: Brigham Young University Press and Deseret Book, 2005), 1–33.

  3. Matendo ya Mitume 9:3–9; 22:6–21; 26:12–18; Mathayo 17:1–13; Marko 9:2–13; Luka 9:28–36.

  4. Barua kamili inaweza kupatikana katika Joseph Smith, “Historia ya Kanisa,” Times and Seasons 3 (Machi. 1, 1842): 706–10.

  5. Joseph Smith, “Latter Day Saints,” in I. Daniel Rupp, He Pasa Ekklesia: An Original History of the Religious Denominations at Present Existing in the United States (Philadelphia: J. Y. Humphreys, 1844), 404–10.

  6. Whitney R. Cross, The Burned-Over District: The Social and Intellectual History of Enthusiastic Religion in Western New York, 1800–1850 (Ithaca, N.Y.: Cornell University Press, 1950); Paul E. Johnson, A Shopkeeper’s Millennium: Society and Revivals in Rochester, New York, 1815–1837 (New York: Hill and Wang, 1983); Nathan O. Hatch, The Democratization of American Christianity (New Haven: Yale University Press, 1989).

  7. Benajah Williams diary, July 15, 1820, copy in Church History Library, Salt Lake City; spelling regularized.

  8. Maelezo ya mwaka 1838 (Joseph Smith—Historia ya 1:5, 8).

  9. 1832 account (Joseph Smith History, ca. Summer 1832, 3, in Joseph Smith, “Letter Book A,” Joseph Smith Collection, Church History Library, Salt Lake City); 1838 account (Joseph Smith—Historia ya 1:17).

  10. Maelezo ya mwaka 1838 (Joseph Smith—Historia ya 1:17); maelezo ya mwaka 1835 (Joseph Smith, “Sketch Book of the use of Joseph Smith, jr.,” Journal, Nov. 9–11, 1835, Joseph Smith Collection, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Salt Lake City.

  11. 1832 account (Joseph Smith History, ca. Summer 1832, 3, in Joseph Smith, “Letter Book A,” Joseph Smith Collection, Church History Library, Salt Lake City).

  12. Joseph Smith to William W. Phelps, Nov. 27, 1832, Joseph Smith Collection, Church History Library, Salt Lake City; available at www.josephsmithpapers.org.

  13. Maelezo ya mwaka 1838 (Joseph Smith—Historia ya 1:25).