Vitabu vya Maelekezo na Miito
38. Sera za Kanisa, na Miongozo


“38. Sera na Miongozo ya Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“38. Sera na Miongozo ya Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

38.

Sera na Miongozo ya Kanisa

38.1

Ushiriki Kanisani

Baba Yetu wa Mbinguni anawapenda watoto Wake. “Wote ni sawa kwa Mungu,” na Anawaalika wote “kuja kwake na kupokea wema Wake” (2 Nefi 26:33).

38.1.1

Mahudhurio kwenye Mikutano ya Kanisa

Wote wanakaribishwa kuhudhuria mikutano ya sakramenti, mikutano mingine ya Jumapili na matukio ya kijamii ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Afisa anayeongoza ana wajibu wa kuhakikisha kwamba wote wanaohudhuria wanaheshimu mpangilio mtakatifu.

Wale wanaohudhuria wanapaswa kuepuka kadhia au vurugu ambavyo ni kinyume na kuabudu au malengo mengine ya mkutano. Mahitaji yote ya umri na tabia za mikutano tofauti tofauti ya Kanisa vinapaswa kuheshimiwa. Hiyo inahitaji kujiepusha na tabia za wazi za kimapenzi na kwa mavazi au unadhifu ambao unaweza kuvuruga mawazo. Pia inazuia kutoa kauli za kisiasa au kuzungumza juu ya mambo ya kijinsia au tabia zingine binafsi katika njia ambayo inaondoa mawazo kutoka kwenye mkutano uliofokasi kwa Mwokozi.

Kama kuna tabia isiyofaa, askofu au rais wa kigingi atatoa ushauri wa faragha katika roho ya upendo. Anawahimiza wale ambao tabia zao hazifai kwenye tukio hilo kufokasi kwenye kudumisha mazingira matakatifu kwa ajili ya kila mtu aliyehudhuria kwa msisitizo maalumu juu ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Mwokozi.

Nyumba za mikutano ya Kanisa zinabaki kuwa mali binafsi zinazopaswa kukufuata sera za Kanisa. Watu ambao hawako tayari kufuata miongozo hii wataombwa katika njia ya heshima kutohudhuria mikutano na matukio ya Kanisa.

38.2

Sera kwa ajili ya Ibada na Baraka

Maelezo ya jumla kuhusu ibada na baraka yametolewa katika sura ya 18. Maelezo kuhusu ibada za hekaluni yametolewa katika sura ya 27 na 28. Maaskofu wanaweza kuwasiliana na rais wa kigingi kama wana maswali. Marais wa vigingi wanaweza kuwasiliana na Urais wa Eneo kama wana maswali.

38.3

Ndoa za Kiserikali

Viongozi wa Kanisa huwahimiza waumini kuwa wenye kustahili kwa ajili ya kufunga ndoa na kuunganishwa hekaluni. Kama sheria za eneo husika zinaruhusu, viongozi wa Kanisa wanaweza kufungisha ndoa za kiserikali.

Ndoa za kiserikali zinapaswa kufungwa kulingana na sheria za mahali ambapo ndoa inafungwa.

38.3.1

Nani Anaweza Kufungisha Ndoa za Kiserikali

Kama sheria ya eneo husika inaruhusu, maafisa wa Kanisa wafuatao ambao bado wana wito wanaweza, kupitia wito wao kufungisha ndoa ya kiserikali:

  • Rais wa misheni

  • Rais wa kigingi

  • Rais wa wilaya

  • Askofu

  • Rais wa tawi

Maafisa hawa wanaweza tu kutimiza wajibu wa kufungisha ndoa ya kiserikali kati ya mwanamume na mwanamke. Masharti yote yafuatayo lazima pia yatumike:

  • Bibi harusi au bwana harusi ni muumini wa Kanisa au ana tarehe ya kubatizwa.

  • Kumbukumbu ya uumini ya bibi harusi au bwana harusi ipo au itakuwepo baada ya ubatizo, kwenye eneo la Kanisa ambalo afisa huyo anasimamia.

  • Afisa wa Kanisa anaruhusiwa kisheria kufungisha ndoa ya kiserikali katika mamlaka ya kisheria ya eneo ambapo ndoa itafungwa.

38.3.4

Ndoa za Kiserikali Zilizofungwa Katika Majengo ya Kanisa

Sherehe ya harusi inaweza kufanyika katika jengo la Kanisa kama haivurugi ratiba ya shughuli za kawaida za Kanisa. Ndoa hazipaswi kufungwa katika siku ya Sabato au jioni ya Jumatatu. Ndoa zinazofungwa katika majengo ya Kanisa zinapaswa kuwa za kawaida na zenye heshima. Muziki unapaswa kuwa mtakatifu, wenye staha na shangwe.

Ndoa zinaweza kufungwa katika Kanisa, bwalo la utamaduni au chumba chochote kinachofaa. Ndoa zinapaswa kufuata miongozo kwa ajili ya matumizi sahihi ya nyumba ya mikutano.

38.3.6

Sherehe ya Ndoa ya Kiserikali

Ili kufungisha ndoa ya kiserikali, afisa wa Kanisa anawahutubia maharusi na anasema, “Tafadhali mshikane kwa mkono wa kulia.” Kisha anasema, “[Jina kamili la Bwana Harusi] na [Jina kamili la Bibi harusi], mmeshikana kwa mikono ya kulia katika ahadi ya viapo mtakavyoingia sasa katika uwepo wa Mungu na mashahidi hawa.” (Maharusi wanaweza kuchagua au kupendekeza mashahidi hawa kabla ya tukio hili.)

Kisha afisa anamuuliza bwana harusi, “[Jina kamili la Bwana harusi], je, unampokea [Jina kamili la bibi harusi] kama mke wako wa ndoa kisheria, na kwamba kwa hiari yako na uchaguzi wako kwa dhati unaahidi kama mwenza wake na mume wake wa ndoa kisheria kwamba utaambatana naye na si mwingine; kwamba utatii sheria zote, majukumu yote na wajibu wote unaohusiana na hali takatifu ya ndoa; na kwamba utampenda, kumheshimu na kumthamini kwa kipindi chote cha maisha yenu?”

Bwana harusi anajibu, “ndiyo” au “Nitafanya hivyo.”

Afisa wa Kanisa kisha anamuuliza bibi harusi, “[Jina kamili la Bibi harusi], je, unampokea [Jina kamili la bwana harusi] kama mume wako wa ndoa kisheria, na kwamba kwa hiari yako na uchaguzi wako kwa dhati unaahidi kama mwenza wake na mke wake wa ndoa kisheria kwamba utaambatana naye na si mwingine; kwamba utatii sheria zote, majukumu yote na wajibu wote unaohusiana na hali takatifu ya ndoa; na kwamba utampenda, kumheshimu na kumthamini kwa kipindi chote cha maisha yenu?”

Bibi harusi anajibu, “ndiyo” au “Nitafanya hivyo.”

Afisa wa Kanisa kisha anasema kwa wenza hawa, “Kwa uwezo wa mamlaka ya kisheria niliyokabidhiwa kama mzee wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, nawatangaza ninyi, [jina la bwana harusi] na [bibi harusi], mume na mke, mliooana kisheria kwa kipindi chote cha maisha yenu ya duniani.”

(Maneno mbadala kwa ajili ya kasisi asiyehudumu kama afisa msimamizi wa Kanisa: “Kwa uwezo wa mamlaka ya kisheria niliyokabidhiwa kama kasisi katika [tawi la jeshi au asasi ya kijamii], nawatangaza ninyi, [jina la bwana harusi] na [bibi harusi], mume na mke, mliooana kisheria kwa kipindi chote cha maisha yenu ya duniani.”

“Mungu na abariki muungano wenu kwa furaha katika uzao wenu na maisha marefu ya furaha pamoja, na awabariki katika kutunza viapo vyenu vitakatifu mlivyovifanya. Baraka hizi ninaziomba juu yenu katika jina la Bwana Yesu Kristo, amina.”

Mwaliko wa kubusiana kama mume na mke ni wa hiari, kutegemeana na desturi za kitamaduni.

38.4

Sera za Kuunganisha

Ibada za kuunganisha za hekaluni huunganisha familia kwa ajili ya milele yote pale waumini wanapojitahidi kuheshimu maagano waliyoyafanya wakati walipopokea ibada. Ibada za kuunganisha zinajumuisha:

  • Kuunganishwa kwa mume na mke.

  • Kuwaunganisha watoto kwa wazazi.

Wale ambao wanashika maagano yao wataendelea kuwa na baraka zao binafsi zilizotolewa wakati wa kuunganishwa. Hii ni kweli hata kama mwenza wa mtu amevunja maagano au amejiondoa kutoka kwenye ndoa.

Watoto waaminifu ambao wameunganishwa kwa wazazi au wamezaliwa katika agano watabakia na baraka ya malezi ya milele. Hii ni kweli hata kama wazazi wao walifuta kuunganishwa kwao kwa ndoa, kuondoa uumini wao wa Kanisa au kujiuzulu uumini wao.

Waumini washauriane na askofu wao kama wana maswali kuhusu sera za kuunganishwa. Askofu anawasiliana na rais wa kigingi kama ana maswali. Marais wa vigingi wanaweza kuwasiliana na urais wa hekalu katika wilaya yao, Urais wa Eneo au Ofisi ya Urais wa Kwanza kama wana maswali.

38.5

Nguo na Gamenti za Hekaluni

38.5.1

Nguo za Hekaluni

Wakati wa ibada za endaumenti na kuunganishwa hekaluni, waumini wa Kanisa wanavaa nguo nyeupe. Wanawake wanavaa nguo nyeupe zifuatazo: gauni la mikono mirefu au gauni la mkikono ya robo tatu (au sketi na blauzi mikono mirefu au robo tatu), soksi na viatu au ndala.

Wanaume wanavaa nguo nyeupe zifuatazo: shati mikono mirefu, tai ndefu au ya kipepeo, suruali, soksi na viatu au ndala.

Wakati wa ibada za endaumenti na kuunganishwa waumini wanavaa nguo za ziada za sherehe juu ya nguo zao nyeupe.

38.5.2

Kupata Mavazi na nguo za Hekaluni

Viongozi wa Kata na Kigingi huwahimiza waumini wenye endaumenti wapate mavazi yao wenyewe ya hekaluni. Nguo na gamenti za hekaluni zinaweza kununuliwa kutoka kituo cha Usambazaji Cha Kanisa au kwenye store.ChurchofJesusChrist.org. Makarani wa kigingi na kata wanaweza kuwasaidia waumini waagize mavazi.

38.5.5

Uvaaji na Utunzaji wa Gamenti

Waumini ambao wanapokea endaumenti hufanya maagano ya kuvaa gamenti ya hekaluni maisha yao yote.

Ni heshima takatifu kuvaa vazi la hekaluni. Kufanya hivyo ni kudhihirisha msimamo wa ndani wa kumfuata Mwokozi Yesu Kristo.

Vazi ni ukumbusho wa maagano yaliyofanywa hekaluni. Linapovaliwa kwa usahihi maishani mwote, litakuwa kama kinga.

Gamenti inapaswa kuvaliwa ndani ya nguo za nje. Ni jambo la uamuzi binafsi ikiwa nguo zingine za ndani zivaliwe kwa juu au ndani ya gamenti.

Gamenti haipaswi kuvuliwa kwa ajili ya shughuli ambazo zinaweza kufanywa wakati gamenti ikiwa imevaliwa. Gamenti haipaswi kurekebishwa ili kukidhi fasheni mbalimbali za mavazi.

Gamenti ni takatifu na inapaswa kutendewa kwa heshima. Waumini waliopokea endaumenti wanapaswa kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu ili kujibu maswali binafsi kuhusu uvaaji wa gamenti.

38.5.7

Utupaji wa Mavazi na Nguo za Sherehe za Hekaluni

Ili kutupa gamenti za hekaluni zilizochakaa, waumini wanapaswa kuondoa alama na kuziharibu. Waumini kisha wanakatakata vitambaa viliyobaki ili isiweze kutambulika kama ni gamenti. Nguo iliyobaki inaweza kutupwa.

Waumini wanaweza kuwapa waumini wengine wenye endaumenti gamenti na nguo za hekaluni ambazo ziko katika hali nzuri.

38.5.8

Nguo za Hekaluni za Mazishi

Kama inawezekana, waumini waliofariki ambao wana endaumenti wanapaswa kuzikwa au kuchomwa wakiwa katika nguo za hekaluni. Kama tamaduni za kimila au desturi za mazishi zinafanya hii ionekane kutofaa au ngumu, vazi linaweza kukunjwa na kuwekwa karibu na mwili.

Mwili wa mwanamume unavalishwa gamenti ya hekaluni na nguo nyeupe zifuatazo: shati ya mikono mirefu, tai ndefu au ya kipepeo, suruali, soksi na viatu au ndala. Mwili wa mwanamke unavalishwa gamenti ya hekaluni na nguo nyeupe zifuatazo: gauni la mikono mirefu au gauni la mkikono ya robo tatu (au sketi na blauzi ya mikono mirefu au robo tatu), soksi na viatu au ndala.

Vazi la ibada ya hekaluni linavalishwa kwenye mwili kama ilivyoelekezwa katika endaumenti. Joho linawekwa kwenye bega la kulia na kufungwa na kamba ya kuvuta kwenye upande wa kushoto wa kiuno. Aproni inafungwa kuzunguka kiuno. Mkanda unawekwa kuzunguka kiuno na kufungwa katika fundo juu ya paja la kushoto. Kofia ya mwanamume kwa kawaida inawekwa karibu na mwili wake mpaka muda wa kufunga jeneza au chombo. Kofia kisha inawekwa fundo likiwa juu ya sikio la kushoto. Shela ya mwanamke inaweza kufunikwa kwenye mto nyuma ya kichwa chake. Kufunika uso wa mwanamke kwa shela kabla ya maziko au kuchomwa siyo lazima, kama itaamuliwa na familia.

38.6

Sera kwenye Maswala ya Maadili

38.6.1

Utoaji Mimba

Bwana aliamuru, “Wala … usiue, wala usifanye chochote kinachofanana na hiayo” (Mafundisho na Maagano 59:6). Kanisa linapinga utoaji mimba kwa mtu kujichagulia au kwa sababu za kijamii. Waumuni hawatakiwi kutoa, kupanga kwa ajili ya, kulipia, kukubali, au kuhimiza utoaji mimba. Hali pekee zinazoruhusu hili ni wakati:

  • Mimba inatokana na ubakaji au kujamiiana kwa maharimu (maharimu-watu wenye undugu wa damu).

  • Daktari bingwa amegundua kwamba maisha au afya ya mama ipo kwenye hatari kubwa.

  • Daktari bingwa amegundua kuwa kitoto ambacho hakijazaliwa kina kasoro kubwa ambazo hazitaruhusu mtoto kuishi baada ya kuzaliwa.

Hata mambo haya yenye upekee hayahalalishi utoaji mimba. Utoaji mimba ni jambo zito sana. Linapaswa kufikiriwa tu baada ya watu wanaohusika nalo kuwa wamepokea uthibitisho kupitia sala. Waumini wanaweza kushauriana na maaskofu wao kama sehemu ya mchakato huu.

38.6.2

Unyanyasaji

Unyanyasaji ni kutesa au kutojali wengine kwa njia ambayo inasababisha madhara ya kimwili, kijinsia, kuhisia au kifedha. Msimamo wa Kanisa ni kwamba unyanyasaji wa aina yoyote hauwezi kuvumiliwa. Wale wanaowanyanyasa wenzi wao, watoto, wanafamilia wengine au mtu mwingine wanakiuka sheria za Mungu na za binadamu.

Waumini wote, hususani wazazi na viongozi, wanahimizwa kuwa makini na wenye bidii na kufanya yote wanayoweza kuwalinda watoto pamoja na wengine dhidi ya unyanyasaji. Kama Waumini wanafahamu unyanyasaji wowote, watoe taarifa kwa mamlaka ya kiserikali na kushauriana na askofu. Viongozi wa Kanisa wanapaswa kuchukulia taarifa za unyanyasaji kwa uzito na kamwe kutozipuuza.

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto au vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja aada ya kukubaliwab(ona ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Wanatakiwa kurudia mafunzo haya kila baada ya miaka mitatu.

Wakati unyanyasaji unatokea, jukumu la kwanza na la haraka la viongozi wa Kanisa ni kuwasaidia wale walionyanyaswa na kuwalinda watu walio katika hatari kutokana na unyanyasaji wa baadaye. Viongozi wanapaswa kutomtia moyo mtu kubaki kwenye nyumba au hali ambayo ni ya manyanyaso au isiyo salama.

38.6.2.1

Simu ya Msaada wa Manyanyaso

Katika baadhi ya nchi, Kanisa limeanzisha simu ya siri ya msaada wa manyanyaso kuwasaidia marais wa vigingi na maaskofu. Viongozi hawa wanapaswa kwa haraka kupiga simu ya msaada kuhusu kila hali ambayo mtu anaweza kuwa amenyanyaswa—au katika hatari ya kunyanyaswa. Wanapaswa pia kupiga namba hiyo kama wakifahamu kwamba muumini anaangalia, ananunua, au anasambaza ponografia ya watoto.

Katika nchi ambazo hazina simu ya msaada, askofu ambaye anafahamu juu ya unyanyasaji anapaswa kuwasiliana na rais wake wa kigingi. Rais wa kigingi anapaswa kuomba mwongozo kutoka kwa mshauri wa sheria wa eneo.

38.6.2.2

Kushauri katika Kadhia za Unyanyasaji

Wahanga wa unyanyasaji mara nyingi wanateseka kwa kiwewe. Marais wa vigingi na maaskofu wanaitikia kwa moyo wa dhati wa huruma na uwezo wa kuhisi maumivu ya mwingine. Wanatoa ushauri wa kiroho na msaada kuwasaidia wahanga kushinda athari angamizi za unyanyasaji.

Wakati mwingine wahanga wana hisia za aibu au hatia. Wahanga hawana hatia ya dhambi. Viongozi wanawasaidia wao pamoja na familia zao waelewe upendo wa Mungu na uponyaji ambao huja kupitia Yesu Kristo (ona Alma 15:8; 3 Nefi 17:9).

Marais wa Vigingi na maaskofu wanapaswa kuwasaidia wale waliofanya unyanyasaji watubu na waache tabia yao ya unyanyasaji. Kama mtu mzima amefanya dhambi ya kijinsia dhidi ya mtoto, tabia inaweza kuwa ngumu sana kuibadili. Mchakato wa toba unaweza kuwa mrefu sana. Ona 38.6.2.3.

Kwa kuongezea kwenye kupokea msaada wa kutia moyo wa viongozi wa Kanisa, wahanga, wahalifu, na familia zao wanaweza kuhitaji ushauri wa kitaalamu. Kwa maelezo, ona 31.3.6.

38.6.2.3

Unyanyasaji wa Mtoto au Kijana

Unyanyasaji wa mtoto au kijana ni dhambi kubwa sana (ona Luka 17:2). Kama ilivyotumuka hapa, unyanyasaji wa mtoto au kijana unajumuisha yafuatayo:

  • Unyanyasaji kimwili: Kutesa na kuleta madhara mabaya ya kimwili kwa kulazimisha. Baadhi ya madhara yanaweza yasionekane.

  • Unyanyasaji wa Kijinsia au unyonyaji: Kuwa na shughuli zozote za kijinsia na mtoto au kijana au kwa makusudi kuruhusu au kuwasaidia wengine kuwa na shughuli kama hizo. Kama ilivyotumika hapa, unyanyasaji wa kijinsia haujumuishi shughulu za kujamiiana kati ya watoto wawili ambao umri wao unafanana.

  • Unyanyasaji wa kihisia: Kutumia vitendo na maneno ili kudhuru vibaya hisia za mtoto au kijana za kujiheshimu au kujiona mwenye thamani. Hii kwa kawaida inahusisha matusi ya mara kwa mara, kulaghai, na lawama ambazo zinadhalilisha na kudunisha. Inaweza pia kujumuisha utelekezaji wa hali ya juu.

  • Ponografia ya watoto: ona 38.6.6.

Kama askofu au rais wa kigingi anajua juu ya, au anashuku unyanyasaji wa mtoto au kijana, kwa haraka anafuata maelekezo katika 38.6.2.1. Pia anachukuwa hatua kusaidia kulinda dhidi ya unyanyasaji zaidi.

Baraza la uumini la Kanisa na kumbukumbu za maelezo ya ufafanuzi zinatakiwa ikiwa muumini mtu mzima anamnyanyasa mtoto au kijana kama ilivyoelezwa katika sehemu hii. Ona pia 38.6.2.5.

Kama mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 anamnyanyasa mtoto, rais wa kigingi anawasiliana na Ofisi ya Urais wa Kwanza kwa ajili ya maelekezo.

38.6.2.4

Unyanyasaji wa Mke au Mume au Mtu Mzima Mwingine

Mara nyingi hakuna ufafanuzi mmoja wa unyanyasaji ambao unaweza kutumika katika hali zote. Badala yake, kuna ukubwa tofauti tofauti katika tabia ya unyanyasaji. Utofauti huu unaanzia kwenye kutumia maneno makali mara chache chache hadi kwenye kuleta madhara makubwa.

Kama askofu au rais wa kigingi anajua juu ya unyanyasaj wa mke au mume au mtu mzima mwingine, mara moja anafuata maelekezo katika 38.6.2.1. Pia anachukuwa hatua kusaidia kulinda dhidi ya unyanyasaji zaidi.

Viongozi wanatafuta maelekezo ya Roho kuamua kama ushauri binafsi au baraza la Uumini ndiyo mpangilio unaofaa zaidi kushughulikia unyanyasaji. Wanaweza pia kushauriana moja kwa moja na kiongozi wa ukuhani kuhusu mpangilio. Hata hivyo, unyanyasaji wowote wa Mke au Mume au Mtu mzima mwingine ambao unafikia viwango vilivyoelezwa hapa chini unahitaji kuitishwa kwa baraza la uumini.

  • Unyanyasaji kimwili: Kutesa na kuleta madhara mabaya ya kimwili kwa kulazimisha. Baadhi ya madhara yanaweza yasionekane.

  • unyanyasaji wa Kijinsia: Ona hali zilizobainishwa katika 38.6.18.3.

  • Unyanyasaji wa kihisia: Kutumia vitendo na maneno ili kudhuru vibaya hisia za mtoto au kijana za kujiheshimu au kujiona mwenye thamani. Hii kwa kawaida inahusisha matusi ya mara kwa mara, kulaghai, na lawama ambazo zinadhalilisha na kudunisha.

  • Unyanyasaji wa kifedha: kujinufaisha na fedha za mtu fulani. Hii inajumuisha matumizi yasio halali au ambayo hayajaidhinishwa ya mali za mtu, fedha, au vitu vingine vya thamani. Inaweza pia kujumuisha kupata nguvu ya kifedha kwa udanganyifu juu ya mtu fulani. Hii Inaweza kujumuisha kutumia nguvu za kifedha kulazimisha tabia fulani.

38.6.2.5

Miito ya Kanisa, Vibali vya Hekaluni, na Maelezo ya Ufafanuzi kwenye Kumbukumbu za Uumini

Waumini walionyanyasa wengine hawapaswi kupewa miito ya Kanisa na wanaweza wasiwe na kibali cha hekaluni mpaka hapo watakapokuwa wametubu na vizuizi vya uumini wa Kanisa vime ondolewa.

Kama mtu alimyanyasa mtoto au kijana kijinsia au alimnyanyasa vibaya sana mtoto au kijana kimwili au kihisia, kumbukumbu zake za Uumini zitatolewa maelezo ya ufafanuzi. Yeye kamwe hatapewa wito wowote au majukumu yoyote yanayowahusu watoto au vijana. Hii inajumuisha kutokupewa jukumu la kuhudumu kwa familia yenye vijana au watoto nyumbani. Pia inajumuisha kutokuwa na kijana kama mwenzi katika kuhudumu. Vizuizi hivi vinapaswa kubaki kama vilivyo isipokuwa kama Urais wa Kwanza unaidhinisha viondolewe kwa maelezo ya ufafanuzi.

38.6.2.6

Mabaraza ya Kata na Kigingi

Katika mabaraza ya kigingi na kata, urais wa kigingi na uaskofu simamizi mara kwa mara wanarejea upya sera za Kanisa na miongozo juu ya kuzuia na kushughulikia unyanyasaji. Viongozi na washiriki wa baraza wana tafuta mwongozo wa Roho wakati wanapofundisha na kijadili mada hii nyeti.

Washiriki wa baraza pia wanapaswa wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana (ona 38.6.2).

38.6.2.7

Maswala ya kisheria Yanayohusu Unyanyasaji

Kama shughuli za unyanyasaji za muumini zimevunja sheria inayotumika, askofu au rais wa kigingi anapaswa kumsihi muumini atoe taarifa ya shughuli hizi kwa watumishi wa vyombo vya sheria au mamlaka zingine sahihi za kisheria za serikali.

Viongozi wa Kanisa na waumini wanapaswa kutimiza matakwa yote ya kisheria ya kutoa taarifa ya unyanyasaji kwa mamlaka za umma.

38.6.4

Uzazi wa Mpango

Ni heshima ya wanandoa ambao wana uwezo kwa kuzaa watoto kutoa miili ya kufa kwa ajili ya watoto wa kiroho wa Mungu, watoto ambao wana jukumu la kuwalea na kuwatunza (ona 2.1.3). Uamuzi kuhusu ni watoto wangapi wa kuwa nao na ni wakati gani wa kuwa nao ni wa binafsi zaidi. Unapaswa kuachwa kati ya wanandoa na Bwana.

38.6.5

Usafi wa Kimwili na Uaminifu

Sheria ya Bwana ya usafi wa kimwili ni:

  • kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa ya kisheria kati ya mwanamume na mwanamke.

  • Uadilifu ndani ya ndoa

Vitendo vya kimwili vya kimapenzi kati ya mume na mke vinakusudiwa kuwa vizuri na vitakatifu. Vimeamriwa na Mungu kwa ajili ya uumbaji wa watoto na kwa ajili ya kuonesha upendo kati ya mume na mke.

38.6.6

Ponografia ya Mtoto

Kanisa linalaani ponografia ya mtoto katika aina yoyote. Kama askofu au rais wa kingingi anajua kwamba muumini anahusika na ponografia ya mtoto, kwa haraka anafuata maelekezo katika 38.6.2.1.

38.6.8

Ukeketaji wa Viungo vya Uzazi vya Mwanamke

Kanisa linalaani ukeketaji wa Viungo vya Uzazi vya Mwanamke.

38.6.10

Kujamiiana kwa Maharimu

Kanisa linalaani aina yoyote ya kujamiiana kwa maharimu. Kama ilivyotumika hapa, Kujamiiana kwa Maharimu ni mahusiano ya kimapenzi kati ya:

  • Mzazi na Mtoto.

  • Babu au bibi na mjukuu (wa kike au kiume).

  • Ndugu (baba mmoja na mama mmoja).

  • Mjomba au shangazi na mpwa (mtoto wa kike au wa kiume wa kaka au dada).

Kama ilivyotumika hapa, Mtoto, mjukuu, ndugu, mpwa wa kike, na mpwa wa kiume hujumuisha uhusiano wa kibaiolojia, aliyeasiliwa, wa kambo, au wa kulea.

Wakati mtoto mdogo ni mhanga wa Kujamiiana kwa maharimu, askofu au rais wa kigingi anapiga simu ya Kanisa ya msaada wa unyanyasaji katika nchi ambazo inapatikana (ona 38.6.2.1). Katika nchi zingine,rais wa kigingi anapaswa kutafuta mwongozo kutoka kwa mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo. Pia anahimizwa kushauriana na mfanyakazi wa huduma za Familia au meneja wa ustawi na kujitegenea kwenye ofisi za eneo.

Baraza la uumini wa Kanisa na kumbukumbu ya malezo ya ufafanuzi vinatakiwa kama muumini anashiriki kujamiiana kwa maharimu. Kujamiiana kwa maharimu mara zote kunahitaji Kanisa kuondoa uumini wa mtu.

Kama mtoto mdogo anashiriki kujamiiana kwa maharimu, rais wa kigingi anawasiliana na Ofisi ya Urais wa Kwanza kwa ajili ya maelekezo.

Wahanga wa kujamiiana kwa maharimu mara nyingi wanateseka kwa kiwewe. Viongozi wanaitikia kwa huruma ya dhati na kuweza kuhisi maumivu ya mwingine. Wanatoa msaada wa kiroho na ushauri kuwasaidia kushinda matokeo mabaya ya kujamiiana kwa maharimu.

Wakati mwingine wahanga wana hisia za aibu au hatia. Wahanga hawana hatia ya dhambi. Viongozi wanawasaidia wao pamoja na familia zao waelewe upendo wa Mungu na uponyaji ambao huja kupitia Yesu Kristo (ona Alma 15:8; 3 Nefi 17:9).

Kwa kuongezea kwenye kupokea msaada wa kutia moyo kutoka kwa viongozi wa Kanisa, wahanga na familia zao wanaweza kuhitaji ushauri wa wataalamu. Kwa maelezo, ona 38.6.18.2

38.6.12

Uchawi

Uchawi unafokasi kwenye giza na kuongoza kwenye udanganyifu. Unaharibu Imani katika Kristo.

Uchawi hujumuisha kumwabudu Shetani. Pia hujumuisha shughuli za siri ambazo hazina upatanifu na injili ya Yesu Kristo. Shughuli kama hizo zinajumuisha (lakini hazina kikomo kwa) wapiga ramli, laana, na matendo ya uponyaji ambayo ni uigaji wa nguvu za ukuhani wa Mungu (ona Moroni 7:11–17).

Waumini wa Kanisa hawapaswi kushiriki katika aina yoyote ya ibada ya shetani au kushiriki katika njia yoyote kwenye uchawi. Hawapaswi kufokasi kwenye giza kama hilo katika mazungumzo au mikutano ya Kanisa.

38.6.13

Ponografia

Kanisa linalaani ponografia katika aina yoyote. Matumizi ya ponografia ya aina yoyote yanaharibu maisha ya mtu binafsi, familia, na jamii. Pia yanamfukuza kabisa Roho wa Mungu. Waumini wa Kanisa wanapaswa kuepuka aina yoyote ya nyenzo zenye ponografia na kupinga uzalishaji wake, usambazaji na matumizi yake.

Ushauri binafsi na vizuizi visivyo rasmi vya Uumini kwa kawaida vinatosha wakati wa kumsadia mtu atubu kwa kutumia ponografia. Mabaraza ya Uumini kwa kawaida hayaitishwi. Hata hivyo, baraza linaweza kuwa muhimu kwa ajili ya matumizi ya hali ya juu yaliyokubuhu ya ponografia ambayo yamesababisha madhara muhimu kwa ndoa ya muumini na familia (ona 38.6.5). Baraza linahitajika ikiwa muumini anafanya, anashiriki, anamiliki, au mara kwa mara anaangalia picha za ponografia za watoto (ona 38.6.6).

38.6.14

Chuki

Watu wote ni watoto wa Mungu Wote ni akina kaka na akina dada ambao ni sehemu ya familia Yake takatifu (ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu”). Mungu “amefanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja” (Matendo ya Mitume 17:26). “Wote wako sawa” kwake Yeye (2 Nefi 26:33). Kila mtu ni “mwenye thamani mbele yake kama mwingine” (Yakobo 2:21).

Chuki haipatani na neno la Mungu lililofunuliwa. Kupendelewa au kutokupendelewa na Mungu kunategemea msimamo wetu kwake na kwenye amri zake, siyo kwenye rangi ya ngozi ya mtu au sifa zingine.

Kanisa linawataka watu wote kuacha tabia na vitendo vya chuki dhidi ya kundi lolote au mtu binafsi. Waumini wa Kanisa wanapaswa kuwa mifano katika kusimamia heshima kwa ajili ya watoto wote wa Mungu. Waumini wanafuata amri ya Mwokozi ya kuwapenda wengine (ona Mathayo 22:35–39). Wanajitahidi kuwa watu wenye mapenzi mema kwa watu wote, wakikataa chuki ya aina yoyote. Hii inajumuisha chuki iliyo na chanzo kwenye mbari, utaifa, kabila, jinsia, umri, ulemavu, hadhi ya kiuchumi na kijamii, imani za dini au kutoamini, na utambulisho wa kijinsia.

38.6.15

Kuvutiwa na Jinsia Moja na Tabia ya Jinsia Moja

Kanisa linazihimiza familia na waumini kuwafikia kwa kujali, upendo, na heshima watu wanaovutiwa kwa wengine wenye jinsia sawa na yao. Kanisa pia linahimiza uelewa katika jamii kwa ujumla ambayo inaakisi mafundisho yake kuhusu ukarimu, ujumuishi, upendo kwa wengine, na heshima kwa binadamu wote. Kanisa halichukuwi upande wowote juu ya vyanzo vya mvuto wa jinsia moja.

Amri ya Mungu inakataza tabia zote za kuzini iwe kwa jinsia tofauti au jinsia moja. Viongozi wa Kanisa wanawashauri waumini waliokiuka sheria ya usafi wa kimwili. Viongozi wanawasaidia wawe na uelewa wa wazi wa imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, mchakato wa toba , na kusudi la maisha ya dunuani.

Kama waumini wanahisi kuvutiwa na jinsia moja na wanajitahidi kuishi sheria ya usafi wa kimwili, viongozi wawasaidie na kuwatia moyo katika uamuzi wao. Waumini hawa wanaweza kupokea miito ya Kanisa, kuwa na vibali vya hekaluni, na kupokea ibada za hekaluni kama wanastahili. Waumini wa Kanisa wa Kiume wanaweza kupokea na kuutumia ukuhani.

Waumini wote wanaotunza maagano yao watapokea baraka zote zilizoahidiwa bila kujali kama hali zao zinawaruhusu kupokea baraka za ndoa za milele na uzazi katika maisha haya (ona Mosia 2:41).

38.6.16

Ndoa ya Jinsia Moja

Kama sera ya kimafundisho, ikiwa na msingi wa maandiko, kanisa linakiri kwamba ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa ajili ya mpango wa Muumbaji kwa ajili ya hatma ya watoto Wake. Kanisa pia linakiri kwamba sheria ya Mungu inafafanua ndoa kama muungano wa kisheria na wa halali kati ya mwanamume na mwanamke.

38.6.17

Elimu ya Jinsia

Wazazi wana jukumu la msingi kwa ajili ya elimu ya jinsia ya watoto wao. Wazazi wanapaswa kuwa na uaminifu, uwazi, na mazungumzo endelevu na watoto wao kuhusu mapenzi yenye afya na uadilifu.

38.6.18

Unyanyasaji wa Kijinsia, Ubakaji, na aina zingine za Ushambuliaji wa Kijinsia

Kanisa linalaani unyanyasaji wa kijinsia. Kama lilivyotumika hapa, Unyanyasaji wa kijinsia unafafanuliwa kama kulazimisha shughuli zisizotakiwa za kimapenzi kwa mtu mwingine. Shughuli ya kimapenzi kwa mtu ambaye hawezi kutoa idhini ya kisheria inachukuliwa ni unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia unaweza pia kutokea kwa mume au mke au katika mahusiano ya miadi. Kwa maelezo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto au kijana, ona 38.6.2.3.

Unyanyasaji wa kijinsia una uwanda mpana wa matendo, kuanzia usumbufu mpaka ubakaji na aina zingine za shambulio la kijinsia. Unaweza kutokea kimwili, kwa maneno, na katika njia zingine. Kwa mwongozo kuhusu kuwashauri waumini ambao amepata tukio la unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji au aina zingine za shambulio la kijinsia, ona 38.6.18.2.

Kama waumini wanamshuku au wanajua juu ya unyanyasaji wa kijinsia, wanachukua hatua kuwalinda wahanga pamoja na wengine haraha iwezekanavyo. Hii inajumuisha kutoa taarifa kwa mamlaka za kiserikali na kumpa taarifa askofu au rais wa kigingi. Kama mtoto amenyanyaswa, waumini wanapaswa kufuata maelekezo katika 38.6.2..

38.6.18.2

Ushauri kwa ajili ya Wahanga wa Unyanyasaji wa Kijinsia, Ubakaji, na aina zingine za Ushambuliaji wa Kijinsia

Wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, au aina zingine za ushambuliaji wa kijinsia mara nyingi wanateseka kiwewe kikubwa sana. Wanapotoa siri kwa askofu au rais wa kigingi, anajibu kwa huruma ya dhati na kutoa faraja. Anatoa ushauri wa kiroho na msaada kuwasaidia wahanga washinde matokeo mabaya ya unyanyasaji. Anaweza pia kupiga simu ya msaada wa unyanyasaji ya Kanisa kwa ajili ya mwongozo pale unapopatikana.

Wakati mwingine wahanga wana hisia za aibu au hatia. Wahanga hawana hatia ya dhambi. Viongozi hawawalaumu wahanga. Viongozi wanawasaidia wahanga na familia zao waelewe upendo wa Mungu na uponyaji ambao unakuja kupitia Yesu Kristo na upatanisho Wake (ona Alma 15:8; 3 Nefi 17:9).

Wakati waumini wanaweza kuchagua kushiriki taarifa kuhusu unyanyasaji au mashambulizi ya kudhuru, viongozi hawapaswi kufokasi kwa uzito kwenye kila kitu. Hii inaweza kuwa ya kudhuru kwa wahanga.

Kwa kuongezea kwenye kupokea msaada wa kutia moyo kutoka kwa viongozi wa Kanisa, wahanga na familia zao wanaweza kuhitaji ushauri wa wataalamu. Kwa maelezo, ona 31.3.6.

38.6.18.3

Mabaraza ya Uumini

Baraza la uumini linaweza kuwa la muhimu kwa ajili ya mtu ambaye amemshambulia kijinsia au amemnyanyasa mtu fulani. Baraza la uumini linahitajika kama muumini amebaka au ana hatia ya aina nyingine ya shambulizi la kijinsia.

38.6.20

Kujiua

Maisha ya duniani ni zawadi ya thamani kutoka ka Mungu—zawadi ambayo inapaswa kuthaminiwa na kulindwa. Kanisa kwa nguvu zote linaunga mkono uzuiaji wa kujiua.

Watu wengi ambao wamefikiria kuhusu kujiua wanataka kupata faraja kutoka kwenye maumivu ya kimwili, kiakili, kihisia, au kiroho. Watu kama hao wanahitaji upendo, msaada, na kuungwa mkono kutoka kwa familia, viongozi wa Kanisa, na wataalamu waliobobea.

Askofu anatoa msaada wa kikanisa kama muumini anafikiria kujiua au amejaribu kujiua. Pia kwa haraka anamsaidia muumini apate msaada wa kitaalamu.

Licha ya juhudu nzuri za awapendao, viongozi, na wataalamu, kujiua si mara zote kunazuilika. Kunaacha nyuma kuvujika moyo, mtikisiko wa kihisia na maswali yasiyo na majibu kwa wapendwa wake pamoja na wengine. Viongozi wanapaswa kuishauri na kuifariji familia. Wanatoa malezi na msaada.

Siyo sahihi kwa mtu kujitoa uhai. Hata hivyo, Mungu peke Yake anaweza kuhukumu mawazo ya mtu, vitendo na kiwango cha uwajibikaji (ona 1 Samweli 16:7; Mafundisho na Maagano 137:9).

Wale ambao wamempoteza mpendwa wao kwa kujiua wanaweza kupata tumaini na uponyaji katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

38.6.23

Watu wenye Jinsia Mbili

Watu wenye jinsia mbili wanakumbana na changamoto ngumu. Waumini na wasio waumini ambao wanatambulika kama wana jinsia mbili—na familia zao na marafiki—wanapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari, ukarimu, huruma, na wingi wa upendo kama wa Kristo. Wote wanakaribishwa kuhudhuria mikutano ya sakramenti, mikutano mingine ya Jumapili, na matukio mengine ya kijamii ya Kanisa (Ona 38.1.1)

Jinsia ni tabia muhimu ya mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Maana iliyo kusudiwa ya Jinsia katika tangazo la familia ni jinsia ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa. Baadhi ya watu wana uzoefu wa hisia za kutofaa kati ya jinsia ya kibaiolojia na jinsia ya utambulisho Kwa matokeo haya wanaweza kujitambulisha kama wenye jinsia mbili. Kanisa halichukui upande wowote wa watu wanaojitambulisha kama wa jinsia mbili.

Ushiriki mwingi Kanisani na baadhi ya ibada za ukuhani hazibagui jinsia. Watu wenye jinsia mbili wanaweza kubatizwa na kuthibitishwa kama ilivyobainishwa katika 38.2.8.10. Wanaweza pia kushiriki sakramenti na kupokea baraka za ukuhani. Hata hivyo, utawazo kuwa kuhani na ibada za hekaluni zinapokelewa kufuatana na jinsia ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa.

Viongozi wa Kanisa wanashauri dhidi ya tiba ya kutumia madawa au upasuaji kwa lengo la kujaribu kubadili kutoka jinsia ya mtu ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa kwenda jinsia tofauti (“upangaji upya wa jinsia”). Viongozi wanashauri kwamba kuchukua maamuzi haya kutakuwa sababu ya kuweka vizuizi kwenye uumini wa Kanisa.

Viongozi pia wanashauri dhidi ya mabadiliko ya kijamii Mabadiliko ya kijamii yanajumuisha kubadili nguo au tabia, au kubadili jina au kiwakilishi, mtu kujitambulisha kwa jinsia nyingine badala ya jinsia yake ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa. Viongozi wanashauri kwamba wale ambao wanafanya mabadiliko ya kijamii watapitia baadhi ya vizuizi vya uumini wa Kanisa kwa kipindi cha mabadiliko haya.

Vizuizi vinajumuisha kupokea au kutumia ukuhani, kupokea au kutumia kibali cha hekaluni, na kupokea baadhi ya miito ya Kanisa. Ingawa baadhi ya fursa za uumini wa Kanisa zimezuiliwa, ushiriki mwingine Kanisani unakaribishwa.

Kama muumini anaamua kubadili jina lake alipendalo au viwakilishi vya jinsi anavyoitwa, jina linalopendwa linaweza kuandikwa katika sehemu ya jina linalopendwa kwenye kumbukumbu ya muumini. Mtu anaweza kuitwa kwa jina linalopendwa katika kata.

Hali zinatofautiana sana kutoka kitengo kimoja hadi kingine na mtu mmoja na mwingine. Waumini na viongozi wanashauriana pamoja wao kwa wao na wanashauriana na Bwana. Marais wa maeneo watawasaidia kwa tahadhari viongozi wa mahala husika kushughulikia hali za mtu binafsi. Maaskofu wanashauriana na rais wa kigingi. Marais wa vigingi na marais wa misheni lazima watafute ushauri kutoka Rais wa Eneo (ona 32.6.3).

38.7

Sera za Tiba na Afya

38.7.2

Mazishi na Kuchoma Moto

Familia ya mtu aliyefariki inaamua ikiwa mwili wake unapaswa kuzikwa au kuchomwa. Wanaheshimu matakwa ya mtu.

Katika nchi zingine, sheria inataka mwili uchomwe moto. Katika hali zingine mazishi hayawezi kufanyika au familia haiwezi kumudu. Katika hali zote, mwili unapaswa kutendewa kwa heshima na staha. Waumini wanapaswa kuhakikishiwa kwamba nguvu ya Ufufuko siku zote inatumika (ona Alma 11:42–45).

Pale inapowezekana, mwili wa muumini marehemu ambaye ana endaumenti unapaswa kuvishwa mavazi kufuata utaratibu wa hekaluni wakati unapozikwa au kuchomwa 38.5.8).

38.7.3

Watoto Ambao Wanakufa kabla ya Kuzaliwa (Wanao Kufa Kabla ya Kuzaliwa na Watoto wa Mimba zilizoharibika)

Wazazi wanaweza kuamua ikiwa wafanye huduma ya mazishi au huduma fupi ya maombezi kaburini ambapo masalia ya mwili uliochomwa yametunzwa.

Ibada za Hekaluni hazihitajiki kufanywa kwa niaba ya watoto wanaokufa kabla ya kuzaliwa. Hii haikanushi uwezekano kwamba watoto hawa wanaweza kuwa sehemu ya familia katika milele. Wazazi wanahimizwa kumtumaini Bwana na kutafuta faraja Yake.

38.7.4

Eutanasia (Kifo cha Huruma)

Maisha ya duniani ni zawadi ya thamani kutoka kwa Mungu. Eutanasia ni kukatisha kwa makusudi maisha ya mtu ambaye anateseka kutokana na ugonjwa usiopona au hali zingine. Mtu anayeshiriki katika eutanasia, ikijumuisha kumsaidia mtu fulani kufa kwa kujiua, anakiuka amri ya Mungu na anaweza kukiuka sheria za mahala husika.

Kukatisha au kujihusisha na hatua za juu za msaada wa maisha kwa ajili ya mtu katika kilele cha maisha haichukuliwi kama eutanasia (ona 38.7.11).

38.7.5

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI

Waumini ambao wameambukizwa Virusi vya Ukimwi (human immunodeficiency virus) au ambao wana UKIMWI (Upungufu wa Kinga mwilini) wanapaswa kukaribishwa kwenye mikutano na shughuli za Kanisa. Kuhudhuria kwao siyo hatari kiafya kwa wengine.

38.7.8

Tiba na Utunzaji wa Afya

Kutafuta msaada stadi wa tiba, kutumia imani, na kupokea baraka za Ukuhani vinafanya kazi pamoja kwa ajili ya uponyaji, kulingana na mapenzi ya Bwana.

Waumini hawapaswi kutumia au kutangaza tiba au kanuni za afya ambazo zina mashaka kimaadili, kiroho ama kisheria. Wale wenye matatizo ya kiafya wanapaswa kushauriana na wataalamu wenye weledi wa tiba ambao wana leseni katika maeneo wanakofanyia kazi

38.7.9

Tiba ya Bangi

Kanisa linapinga matumizi ya bangi kwa ajili ya makusudi yasiyo ya tiba. Ona 38.7:14.

38.7.11

Kurefusha Maisha (pamoja na Kumsaidia Mtu Kuishi)

Waumini hawapaswi kuhisi kuwa na wajibu wa kurefusha maisha ya duniani kwa njia za zinazovuka mipaka. Maamuzi haya yanafanywa vizuri na mtu , kama inawezekana, au wanafamilia. Wanapaswa kutafuta ushauri stadi wa tiba na mwongozo mtakatifu kupitia sala.

38.7.13

Chanjo

Chanjo zinazosimamiwa na wataalamu hodari wa tiba zinalinda afya na zinalinda maisha. Waumini wa Kanisa wanahimizwa kujilinda wao wenyewe, watoto wao, na wanajamii wao kupitia chanjo.

Hatimaye, watu binafsi wana wajibu wa kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu chanjo. Kama waumini wana mashaka, wanapaswa kushauriana na wataalamu hodari wa tiba na pia kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu.

38.7.14

Neno la Hekima na Utekelezaji wa Tiba

Neno la Hekima ni amri ya Mungu. Manabii wameeleza wazi kwamba mafundisho katika Mafundisho na Maagano 89 hujumuisha kutokutumia tumbaku, vinywaji vikali (pombe), na vinywaji vya moto (chai na kahawa).

Kuna vitu vingine vyenye madhara na mazoea ambayo hayajaelezwa bayana katika Neno la Hekima. Waumini wanapaswa kutumia hekima na maamuzi ya sala katika kufanya chaguzi ili kusimamia afya ya kimwili, kiroho, na kihisia.

38.8

Sera za Utawala

38.8.1

Kuasili na Uleaji wa Watoto Wasio wa Kuzaa Mwenyewe

Kuasili watoto na kulea watoto wasio wa kuwazaa kunaweza kuwabariki watoto pamoja na familia. Familia za milele zenye upendo zinaweza kuundwa kupitia kuasili. Kama mtoto anakuja kwenye familia kupitia kuasili au kuzaliwa, wao ni baraka yenye thamani sawa.

Waumini wanaotafuta kuasili au kutoa malezi kwa watoto wasio wa kuwazaa wanapaswa kutii sheria zote zinazotumika za nchi na serikali husika.

38.8.4

Sahihi na Picha za Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Maofisa Wakuu, na Sabini wa Eneo

Waumini wa Kanisa hawapaswi kutafuta sahihi za Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Maafisa Wakuu, au Sabini wa Maeneo. Kufanya hivyo kunapunguza sifa kutoka kwenye miito yao mitakatifu na roho ya mikutano. Inaweza pia kuwazuwia kuwasalimia waumini wengine.

Waumini hawapaswi kupiga picha za Viogozi Wakuu Wenye Mamlaka, Maafisa Wakuu au Sabini wa Maeneo katika makanisa.

38.8.7

Magazeti ya Kanisa

Magaziti ya Kanisa yanajumuisha:

Urais wa Kwanza unawahimiza waumini wote wasome magazeti ya Kanisa. Magazeti yanaweza kuwasaidia waumini wajifunze injili ya Yesu Kristo, wajifunze mafundisho ya manabii walio hai, wahisi kuunganishwa kwenye familia ya Kanisa ulimwenguni kote, wakabiliane na changamoto kwa imani, na wamkaribie zaidi Mungu.

38.8.8

Jina la Kanisa, Wordmark, na Ishara

Picha
Nembo ya bidhaa na alama ya Kanisa

Jina la Kanisa, nembo ya bidhaa na alama ni vitambulisho muhimu vya Kanisa.

Nembo ya bidhaa na alama. Nembo ya bidhaa na alama ya Kanisa (ona picha hapo juu), vinapaswa kutumika kama ilivyoidhinishwa na Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Zisitumike kama vitu vya mapambo. Wala kutumika kwa njia yoyote binafsi, ya kibiashara, au njia ya matangazo.

38.8.10

Kompyuta

Kompyuta na data zinazotumika katika nyumba za mikutano ya Kanisa zimetolewa na kusimamiwa na Makao makuu ya Kanisa au ofisi za eneo Viongozi na Waumini wanatumia nyenzo hizi kusaidia malengoya Kanisa, ikiwa ni pamoja na kazi ya historia ya familia.

Data zote kwenye kompyuta hizi lazima zipate leseni kikamilifu.

38.8.12

Nyenzo za Mitaala

Kanisa linatoa vifaa ili kuwasaidia waumini wajifunze na, waishi Injili ya Yesu Kristo. Hizi zinajumuisha maandiko, jumbe za Mkutano Mkuu, magazeti, vitabu vya kiada, vitabu, na nyenzo zingine. Viongozi wanawahimiza waumini kutumia maandiko na vyenzo zingine kama inavyotakiwa ili kujifunza injili nyumbani.

38.8.14

Mavazi na Mwonekano

Waumini wa Kanisa wanahimizwa kuonesha heshima kwa mwili katika chaguzi zao kuhusu mavazi yanayofaa na mwonekano. Nini kinafaa hutofautiana kulingana na tamaduni na hali tofauti tofauti.

38.8.16

Siku ya Mfungo

Waumini wanaweza kufunga wakati wowote. Hata hivyo, kwa kawaida wanazingatia Sabato ya kwanza ya mwezi kama siku ya kufunga.

Siku ya mfungo kwa kawaida inajumuisha kusali, kutokula au kunywa kwa kipindi cha masaa 24 (kama afya inaruhusu) na kutoa kwa ukarimu matoleo ya mfungo. Matoleo ya mfungo ni mchango ili kuwasaidia wale wenye mahitaji (ona 22.2.2).

Wakati mwingine mikutano ya Kanisa ulimwenguni kote au mikutano ya mahala husika inafanyika kwenye Sabato ya kwanza ya mwezi. Wakati hii inapotokea, urais wa kigingi unaamua Sabato inayofuata kuwa kwa ajili ya siku ya mfungo.

38.8.17

Kamari na Bahati Nasibu

Kanisa linapinga na kushauri dhidi ya kamari katika njia yoyote. Hii inajumuisha kuweka dau la michezo (kubeti), na bahati nasibu zinazofadhiliwa na serikali.

38.8.19

Uhamiaji.

Waumini wa Kanisa wanaobaki katika nchi zao za kuzaliwa mara nyingi wana fursa za kulijenga na kuliimarisha Kanisa huko. Hata hivyo, kuhamia kwenye nchi nyingine ni uchaguzi binafsi.

Waumini wanaohamia nchi nyingine wanapaswa kutii sheria zote zinazotumika (ona Mafundisho na Maagano 58:21).).

Wamisionari hawapaswi kudhamini uhamiaji kwa wengine.

38.8.22

Sheria za nchi

Waumini wanapaswa kutii, kuheshimu, na kuidhinisha sheria katika nchi yoyote ambapo wanaishi au kusafiri (ona Mafundisho na Maagano 58:21–22; Makala za Imani 1:12). Hii ni pamoja na sheria ambayo inakataza watu kutoa mafundisho ya dini.

38.8.25

Waumini Kuwasiliana na Makao Makuu ya Kanisa

Waumini wa Kanisa hawahimizwi kupiga simu, kutuma barua pepe au kuandika barua kwa Viongozi Wakuu wenye Mamlaka kuhusu maswali ya injili, changamoto binafsi au maombi yoyote. Waumini wanahimizwa kuwafikia viongozi wao wa maeneo husika ikijumuisha Muungano wa Usaidizi au rais wa akidi ya wazee, wakati wanapotafuta mwongozo wa kiroho (ona 31.3).

38.8.27

Waumini wenye Ulemavu

Viongozi na waumini wanahimizwa kushughulikia mahitaji ya wote wanaoishi ndani ya kitengo chao. Waumini wenye ulemavu wanathaminiwa na wanaweza kuchangia katika njia zenye maana sana. Ulemavu unaweza kuwa wa akili, kijamii, kihisia, au kimwili.

38.8.29

Imani zingine

Mengi ambayo yanavutia, yana uadilifu, na yanayostahili heshima kubwa yanapatikana katika imani zingine nyingi. Wamisionari na waumini wengine lazima wawe wepesi kujali na wenye heshima kwenye imani na desturi za wengine.

38.8.30

Siasa na Shughuli za Kiraia

Waumini wa Kanisa wanahimizwa kushiriki katika siasa na shughuli za kiserikali. Katika nchi nyingi, hii inaweza kujumuisha:

  • Kupiga kura.

  • Kujiunga au kuhudumu katika vyama vya siasa.

  • Kutoa msaada wa kifedha.

  • Kuwasiliana na viongozi na wagombea wa chama.

  • Kuhudumu katika ofisi zilizochaguliwa au kuteuliwa katika serikali ya mtaa na taifa.

Waumini pia wanahimizwa kushiriki katika mambo yanayostahili ili kuzifanya jumuia zao ziwe mahala pazuri pa kuishi na kulea familia.v

Viongozi wa Kanisa wa maeneo husika hawapaswi kuweka mazingira ya kushiriki kwenye masuala ya kisiasa. Wala viongozi wasijaribu kushawishi jinsi waumini wanavyoshiriki kwenye mambo ya kisiasa.

Viongozi na waumini wanapaswa pia kuepuka kauli au tabia ambazo zinaweza kutafsiriwa kama Kanisa kuunga mkono chama chochote cha siasa, jukwaa la kisiasa, sera za kisiasa, au mgombea wa kisiasa.

38.8.31

Faragha za Waumini

Viongozi wa Kanisa wanalazimika kulinda faragha za waumini. Kumbukumbu za Kanisa, vitabu vyenye orodha ya majina na anwani za waumini, na nyenzo zinazofanana na hizo visitumike kwa malengo binafsi, ya kibiashara, au ya kisiasa.

38.8.35

Wakimbizi

Kama sehemu ya jukumu lao la kuwatunza wale wenye mahitaji (ona Mosia 4:26), waumuni wa Kanisa wanatoa muda wao, vipaji, na urafiki kuwakaribisha wakimbizi kama washiriki wa jumuia zao.

38.8.36

Maombi kwa Ajili ya Msaada wa Kifedha wa Kanisa

Waumini wenye shida wanahimizwa kuzungumza na askofu wao badala ya kuwasiliana na Makao Mkuu ya Kanisa au kuomba fedha kutoka kwa viongozi wengine au waumini wa Kanisa.