Vitabu vya Maelekezo na Miito
26. Vibali vya Hekaluni


“26. Vibali vya Hekaluni,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“26. Vibali vya Hekaluni,“ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
Askofu akihojiana na mtu

26.

Kibali cha Hekaluni

26.0

Utangulizi

Kuingia Hekaluni ni fursa takatifu. Viongozi wa kata na vigingi wanawahimiza waumini wote kuwa wenye kustahili na kuwa na kibali hai cha hekaluni hata kama hawaishi karibu na hekalu.

Viongozi wa Kanisa wanafanya kila juhudi kuona kwamba watu wote wanaoingia hekaluni wanastahil kufanya hivyo (ona Zaburi 24:3–5).

Waumini lazima wawe na kibali hai cha hekaluni ili kuingia hekaluni.

Askofu anashauriana na rais wake wa kigingi ikiwa ana maswali kuhusu vibali vya hekaluni ambayo hayajajibiwa katika sura hii. Rais wa kigingi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Urais wa Kwanza akiwa na maswali.

26.1

Aina za Vibali vya Hekaluni

Kuna aina tatu za vibali:

  1. Vibali vya Hekaluni kwa waumini wasio na endaumenti Vibali hivi ni kwa ajili ya waumuni wasio na endaumenti wanaounganishwa kwa wazazi wao au kufanya ubatizo na uthibitisho kwa niaba. Vinatolewa kupitia Leader and Clerk Resources (LCR). Kwa maelezo zaidi, ona 26.4.

  2. Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya ibada za walio hai. Vibali hivi ni kwa ajili ya waumini wanaopokea endaumenti zao wenyewe au kuunganishwa kwa mume au mke. Kibali kwa ajili ya ibada za walio hai kimeambatishwa kwenye kibali cha hekaluni cha kawaida kwa ajili ya waumini wenye endaumenti (imeelezwa hapo chini).

  3. Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya waumini wenye endaumenti. Vibali hivi ni kwa ajili ya waumini ambao awali walikuwa wamekwisha kupata endaumenti. Vinatolewa kupitia (LCR). Vinamruhusu muumini ashiriki katika ibada zote za hekaluni kwa ajili ya marehemu. Pia vinatumika wakati muumini mwenye endaumenti anapounganishwa kwa wazazi au watoto walio hai au waliofariki. Kwa maelezo zaidi, ona 26.3.

26.2

Kuvilinda Vibali vya Hekaluni

26.2.1

Viongozi wa Ukuhani Wanavilinda Vibali vya Hekaluni

Viongozi wa Ukuhani ambao wamepewa mamlaka ya kuwa na vitabu vya vibali vya hekaluni wanapaswa kuvilinda kwa uangalifu.

Viongozi wa Ukuhani pia wanahakikisha kwamba watu binafsi ambao hawana ruhusa hawapati nafasi ya kuzifikia taarifa za kibali cha hekaluni kwenye LCR.

26.2.3

Vibali Vilivyopotea au Kuibiwa

Askofu anawaomba waumini wampe taarifa mapema iwezekanavyo ikiwa kibali chao kimepotea au kuibiwa. Yeye au mshauri aliyeteuliwa au karani atatumia LCR kukifuta kibali hicho haraka iwezekanavyo. Kama utaratibu huu haupatikani, askofu anawasiliana na ofisi ya hekalu ili kukifuta kibali hicho.

26.2.4

Wenye Vibali Ambao Hawaishi Viwango vya Ustahili

Ikiwa askofu anaamua kwamba muumini ambaye ana kibali hai haishi viwango vya ustahili (ona 26.3), anakiomba kibali hicho kutoka kwa muumini. Yeye anatumia LCR kukifuta kibali hicho. Kama utaratibu huu haupatikani, askofu anawasiliana na ofisi ya hekalu ili kukifuta kibali hicho.

26.3

Mwongozo wa Jumla kwa ajili ya Utoaji wa Vibali vya Hekaluni

Viongozi wa Ukuhani wanapaswa kutoa kibali pale tu ikiwa muumini anajibu maswali ya kibali cha hekaluni kwa usahihi.

Mahojino ya kibali cha hekaluni hayapaswi kuharakishwa. Yanapaswa kuwa ya faragha. Hata hivyo mtu anayefanyiwa usaili anaweza kumwalika, mtu mzima mwingine kuwepo wakati wa mahojiano.

Viongozi wa ukuhani hawapaswi kuongeza mahitaji yoyote zaidi ya yale ambayo yapo kwenye muhtasari katika kitabu cha vibali vya Hekaluni. Wala hawapaswi kuondoa masharti yoyote.

Katika vigingi, mshiriki wa urais wa kigingi au karani wa kigingi anaweza kukifanya hai kibali cha hekaluni kwenye LCR baada ya kibali kutolewa. Katika wilaya, mshiriki wa urais wa misheni au karani wa misheni anafanya kibali kuwa hai. Vibali kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho kwa niaba vinafanywa hai wakati vinapochapishwa na mshiriki wa uaskofu au na rais wa tawi.

26.3.1

Mahojiano ya Kibali cha Hekaluni kwa ajili ya Waumini katika Kata na Matawi

Katika kata, askofu au mshauri aliyepangiwa anaendesha mahojiano ya kibali cha hekaluni na anatoa kibali kwa wale ambao wanastahili. Katika tawi, ni rais wa tawi pekee ndiye anayeendesha mahojiano ya hekaluni na anatoa vibali.

Katika kata askofu pekee anawafanyia usaili waumini ambao:

  • Wanapokea endaumenti zao wenyewe (ona 27.1 na 27.2).

  • Wanaunganishwa kwa mume au mke (ona 27.3).

Katika hali ya dharura wakati askofu au rais wa kigingi hawapatikani, anaweza kumruhusu mmoja wa washauri wake kuendesha mahojiano haya.

Kabla ya kutoa kibali katika hali zozote zilizoorodheshwa hapo juu, askofu huipitia upya kumbukumbu ya muumini ili kuthibitisha kwamba haijumuishi nukuu kuhusu vizuizi vya uumini wa Kanisa. Kwa waumini wanaopokea endaumenti zao wenyewe au kuunganishwa kwa mume au mke, pia anahakikisha kwamba:

  • Ubatizo na uthibitisho wa mtu umerekodiwa katika kumbukumbu ya uumini.

  • Wanaume wamepokea Ukuhani wa Melkizedeki.

Baada ya usaili na mshiriki wa uaskofu au rais wa tawi, mshiriki wa urais wa Kigingi anawasaili waumini wanaoishi katika kigingi. Mshiriki wa urais wa misheni anaendesha usaili wa pili kwa ajili ya waumini ambao wanaishi katika wilaya. Rais wa wilaya haendeshi mahojiano ya kibali cha hekaluni isipokuwa kama ameidhinishwa na Urais wa Kwanza.

26.3.2

Usaili wa Vibali vya hekaluni kwa ajili ya Waumini Katika Maeneo yaliyojitenga

Baadhi ya waumini wanaishi katika maeneo ambayo yatahitaji gharama kubwa kusafiri au ni shida kubwa kukutana na mshiriki wa urais wa kigingi au misheni. Katika hali kama hizi, rais wa hekalu anaweza kumsaili mtu na kusaini kibali. Kabla ya kuendesha usaili, anashauriana na rais wa kigingi au wa misheni. Askofu, mshauri aliyeidhinishwa au rais wa tawi anapaswa kuwa tayari alikwisha kumsaili muumini huyu na kusaini kibali.

26.4

Kutoa Vibali vya Hekaluni kwa Waumini Wasio na Endaumenti

26.4.1

Mwongozo wa Jumla

Vibali vya hekaluni vinatolewa kwa waumini wasio na endaumenti kama ifuatavyo:

  • Kwa ajili ya waumini wenye umri wa miaka 11 na zaidi ili kubatizwa na kuthibitishwa kwa niaba ya wafu. (Wasichana na wavulana waliotawazwa wanastahili kwa ajili ya kibali cha hekaluni kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12.)

  • Kwa waumini wenye umri wa miaka 8 mpaka 20 ili kuunganishwa na wazazi wao Watoto walio wadogo chini ya miaka 8 hawahitaji kibali ili kuunganishwa kwa wazazi wao (ona 26.4.4).

  • Kwa ajili ya waumini wenye umri wa miaka 8 mpaka 20 ili kuangalia kuunganishwa kwa ndugu zao walio hai, ndugu zao wa kambo, au ndugu zao waliochangia nao mzazi mmoja kuunganishwa na wazazi wao.

Waumini ambao hapo mwanzo walipokea endaumenti hawapewi kibali chochote kilichoelezewa katika sehemu hii.

Muumini mwanamume wa Kanisa mwenye umri wa kutosha kuwa na ukuhani lazima atawazwe kwenye ofisi ya ukuhani kabla ya kupokea kibali cha hekakuni.

26.4.2

Vibali vya Hekaluni kwa Ajili ya Waumini Wapya Waliobatizwa

Askofu anawasaili waumini wapya ambao ni wa umri sahihi kupokea kibali cha hekaluni kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho pekee kwa niaba ya wafu. Anafanya usaili huu punde baada ya uthibitisho wa muumini, kwa kawaida ndani ya wiki (ona 26.4.1). Kwa kaka wenye ukuhani, usaili huu unaweza kufanywa kama sehemu ya usaili wa kupokea Ukuhani Haruni.

26.4.3

Vibali vya Hekaluni kwa ajili ya Ubatizo na Uthibitisho wa Uwakilishi pekee

Vibali vya Hekaluni ambavyo vinatolewa kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho kwa niaba vinaweza kutumika kwa ajili ya makusudi hayo pekee.

26.4.4

Kibali cha Hekaluni kwa Ajili ya Kuwaunganisha Watoto Walio Hai kwa Wazazi

Waumini ambao wana umri wa miaka 21 au zaidi wanaweza kuunganishwa kwa wazazi wao au kuangalia kuunganishwa ikiwa tu (1) wana endaumenti na (2)wana kibali hai cha hekaluni.

26.5

Kutoa Vibali vya Hekaluni katika Hali Maalumu

26.5.1

Waumini Wanapokea Endaumenti Zao Wenyewe

Waumini wanaostahili wanaotamani kupokea endaumenti zao wenyewe wanaweza kufanya hivyo wakati wanapokamilisha masharti yote yafuatayo:

  • Wana umri angalau wa miaka 18.

  • Wamemaliza shule ya upili au hawahudhurii tena shule ya upili, shule ya sekondari, au zinazofanana na hizo.

  • Mwaka mmoja kamili umepita tangu kuthibitishwa kwao.

  • Wanahisi tamanio la kupokea na kuheshimu maagano ya hekaluni kwa maisha yao yote.

Kwa nyongeza, mwanamume lazima awe na Ukuhani wa Melkizedeki kabla ya kupokea endaumenti yake. Kwa maelezo kuhusu waumini kujitayarisha kupokea endaumenti zao wenyewe, ona 25.2.8. Kwa maelezo kuhusu nani anaweza kupokea endaumenti, ona 27.2.1.

26.5.3

Wamisionari Vijana Wanaorudi Kutoka Kwenye Huduma Mbali na Nyumbani

Raisi wa misheni anaweka tarehe na anakifanya hai kibali ili kiishe matumizi miezi mitatu kuanzia tarehe mmisionari anaporudi nyumbani.

Askofu anawasaili wamisionari waliorudi ili kuwapa kibali kipya cha hekaluni karibu na mwisho wa kumalizika kipindi cha miezi mitatu.

26.5.4

Waumini Ambao Hawajaishi katika Kata ileile kwa Angalau Mwaka Mmoja

Askofu au mshauri aliyepangiwa anawasiliana na askofu wa awali kabla ya kuendesha usaili wa kibali cha kwenda hekaluni.

26.5.7

Waumini Ambao Wanatambulika kama Wamebadilisha Jinsia

Rais wa kigingi anapaswa kushauriana na urais wa Eneo kuzungumzia hali binafsi ya mtu na kwa tahadhari na Upendo kama wa Kristo 38.6.23).

26.5.8

Waumini Waliofanya Dhambi Kubwa

Muumini aliyefanya dhambi kubwa hapokei kibali cha hekaluni hadi pale atakapotubu (ona 32.6).

26.5.9

Waumini Ambao Wamepokelewa Tena baada ya Kunyang’anywa Ushiriki au Kujitoa kwenye Ushiriki Kanisani

26.5.9.1

Waumini Ambao Hawakupewa Endaumenti Hapo Mwanzo

Waumini hawa hawapewi kibali cha kupokea endaumenti zao wenyewe mpaka mwaka mmoja kamili baada ya tarehe ya kurudishwa kwao katika Kanisa kwa kubatizwa na kuthibitishwa.

26.5.9.2

Waumini Ambao Walipokea Endaumenti Hapo Mwanzo

Waumini ambao Walikuwa na endaumenti hapo mwanzo hawapokei aina yoyote ya kibali cha hekaluni mpaka baraka zao za hekaluni zitakapokuwa zimerejeshwa kupitia ibada ya urejesho wa baraka.