Vitabu vya Maelekezo na Miito
22. Kukidhi Mahitaji ya Kimwili na Kujenga Kujitegemea


“22. Kutoa kwa ajili ya Mahitaji ya Kimwili na Kukuza Kujitegemea,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“22. Kutoa kwa ajili ya Mahitaji ya Kimwili na Kukuza Kujitegemea,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
mtu akifanya kazi

22.

Kutoa kwa ajili ya Mahitaji ya Kimwili na Kukuza Kujitegemea

22.0

Utangulizi

Waumini wa Kanisa wanaweka agano la “kubebeana mizigo, …kuomboleza na wale wanaoomboleza … na kuwafariji wale wanaohitaji kufarijiwa” (Mosia 18:8–9).

Waumini wa Kanisa pia wanashauriwa waimarishe kujitegemea kwao wenyewe kupitia kufanya kazi kwa bidii na kwa msaada wa Bwana. Kujitegemea ni uwezo, msimamo na juhudi ya kukimu mahitaji muhimu ya kiroho na ya kimwili ya maisha kwa ajili ya mtu binafsi na familia.


JUHUDI ZA MTU BINAFSI NA FAMILIA


22.1

Kuzaa Kujitegemea

Kwa msaada kutoka kwa Bwana, waumini wanakuza kujitegemea katika njia zifuatazo:

  • Kukuza nguvu za kiroho, kimwili, na kihisia.

  • Kupata elimu, na ajira.

  • Kuboresha utayari wa kimwili.

22.1.4

Utayari wa Kimwili

Maandiko yanafundisha umuhimu wa kuwa tayari (ona Ezekiel 38:7; Mafundisho na Maagano 38:30). Waumini wanashauriwa kuwa tayari ili waweze kujitunza wao wenyewe, familia zao, na kuwatunza wengine nyakati za shida.

Waumini wanaongeza matayarisho yao ya kifedha kwa:

  • Kulipa zaka na matoleo (ona Malaki 3:8–12).

  • Kulipa na kuepuka madeni kadiri iwezekanavyo.

  • Kujitayarisha na kuishi ndani ya bajeti.

  • Kuweka akiba kwa ajili ya baadaye.

  • Kupata elimu sahihi ili iwasaidie kukidhi mahitaji yao wenyewe na familia zao (ona 22.3.3).

Kujitayarisha pia kunajumuisha kukuza mpango kwa ajili ya jinsi ya kushughulikia mahitaji ya msingi wakati wa dharura. Waumini wananahimizwa kutunza vyote, akiba ya muda mfupi na ya muda mrefu ya chakula, maji, na vingine ambavyo ni muhimu.

22.2

Wahudumie Wale Walio na Mahitaji ya Kimwili na Kiroho

Wafuasi wa Bwana wanafundishwa “kupendana … na kutumikiana” na “kuwasaidia wale ambao wanahitaji … msaada” (Mosia 4:15–16). Waumini wanajitahidi kuwaona wengine kama vile Mwokozi anavyowaona, kuelewa nguvu yao ya kipekee na mahitaji yao. Mahitaji haya yanaweza kujumuisha chakula, mavazi, nyumba, elimu, ajira, afya ya kimwili, na afya ya kihisia.

22.2.1

Ghala la Bwana

Nyenzo zote zinazopatikana katika Kanisa ili kuwasaidia wale walio na mahitaji ya kimwili zinaitwa ghala la Bwana (ona Mafundisho na Maagano 82:18–19). Hizi zinajumuisha matoleo ya waumini ya muda wao, vipaji, huruma, vifaa, na nyezo za kifedha ili kuwasaidia wale wenye shida.

Ghala la Bwana lipo katika kila kata na kigingi. Viongozi wanaweza mara kwa mara kuwasaidia watu binafsi na Familia wapate ufumbuzi kwa mahitaji yao kwa kuchota kutoka kwenye maarifa, ujuzi, na huduma inayotolewa na waumini wa kata na Vigingi.

22.2.2

Sheria ya Mfungo na Matoleo ya Mfungo

Mungu ameanzisha sheria ya mfungo na matoleo ya mfungo ili kuwabariki watu Wake na kuwapa njia kwa ajili yao kuwahudumia wale wenye shida. Waumini wanasonga karibu zaidi na Bwana na kuongezeka katika uimara wa kiroho wakati wanapoishi sheria ya mfungo. (Ona Isaya 58:6–12; Malaki 3:8–12.)

Kufunga kunaweza kufanywa wakati wowote. Hata hivyo, waumini kwa kawaida hutumia Sabato ya kwanza ya mwezi kama siku ya mfungo. Siku ya mfungo kwa kawaida inajumuisha yafuatayo:

  • Kusali

  • Kutokula au kunywa kwa kipindi cha saa 24 (ikiwa afya inaruhusu)

  • Kutoa kwa ukarimu matoleo ya mfungo

Matoleo ya mfungo ni mchango wa kuwasaidia wale wenye shida. Wakati waumuni wanapofunga wanaalikwa kutoa sadaka ambayo angalau ni sawa na gharama ya milo ile ambayo haikuliwa.

Waumini wanaweza kutoa matoleo yao ya mfungo na kukamilisha fomu ya utoaji wa Zaka na Matoleo Mengine kwa askofu au mmoja wa washauri wake. Katika sehemu zingine, wanaweza pia kufanya matoleo yao kwa njia ya mtandao.


JUHUDI ZA KIONGOZI


22.3

Mpangilio kwa ajili ya Kukuza Kujitegemea na Kuwatumikia Wale Walio katika Shida

22.3.1

Watafute Wale Wenye Shida.

Askofu ana wajibu mtakatifu wa kuwatafuta na kuwatunza wale walio katika shida (ona Mafundisho na Maagano 84:112). Wengine ambao wana wajibu muhimu katika kumsaidia askofu kwenye wajibu huu ni pamoja na:

  • Akina kaka na akina dada wahudumiaji

  • Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee.

  • Washauri wa askofu.

  • Washiriki wengine wa baraza la kata.

22.3.2

Kuwasaidia Waumini Watambue na Kushughulikia Mahitaji ya Muda Mfupi

Waumini wanajitahidi kukamilisha mahitaji yao ya msingi kupitia juhudi zao wenyewe na msaada kutoka kwa jamaa zao. Wakati hii inapokuwa haitoshi, waumini wanaweza kuhitaji msaada kutoka vyanzo vingine kama vile:

  • Vyanzo vya serikali na jumuiya (ona 22.12

  • Msaada wa Kanisa.

Msaada wa Kanisa unaweza kujumuisha msaada kwenye mahitaji ya muda mfupi kama vile chakula, vifaa vya afya, mavazi, nyumba, au vingine vya msingi. Maaskofu wanaweza kutumia matoleo ya mfungo ili kutatua shida hizi. Pale mipango ya askofu inapopatikana, maaskofu kwa kawaida wanatumia hiyo kutoa chakula na vitu vingine vya msingi (ona “Bishops Orders and Referrals” katika Leaders and Clerk Resources [LCR]).

22.3.3

Kuwasaidia Waumini Wajenge Kujitegeme kwa Muda Mrefu

Waumini wanaweza kuhitaji msaada endelevu ili kutatua changamoto za muda mrefu. Elimu, mafunzo ya ufundi stadi, au vyanzo vingine vinaweza kuwasaidia wakuze kujitegemea na kujipatia mahitaji yao ya muda mrefu.

Mpango wa Kujitegemea unawasaidia waumini watambue nguvu zao na mahitaji yao. Pia unawasaidia watambue nyenzo zinazoweza kutumika. Mpango huu unapaswa kutumika kila wakati msaada wa Kanisa unapofikiriwa.

22.3.4

Wahudumie Wale Wenye Mahitaji ya Kihisia

Waumini wengi wanapitia changamoto za kihisia. Akina kaka na akina dada wahudumiaji na viongozi wa kata wanaweza kuwa vyombo katika kuwasaidia waumini wenye changamoto hizi.

22.4

Kanuni ya Kutoa Msaada wa Kanisa

Kwa msaada wa Bwana, wauminu wanatafuta kujikimu kwa ajili yao wenyewe na familia zao.

Msaada wa Kanisa umekusudiwa kuwasaidia waumini wakuze kujitegemea, siyo kuwa tegemezi. Msaada wowote unaotolewa unapaswa kuwamarisha waumini katika juhudi zao za kuwa wanao itegemea.

22.4.1

Himiza Uwajibikaji Binafsi na wa Familia

Viongozi wanafudisha kwamba watu binafsi na familia wana wajibu wa msingi kwa ajili ya ustawi wao wenyewe wa kimwili, kihisia, na kiroho.

Kabla ya kutoa msaada wa Kanisa, askofu (au kiongozi mwingine au Muumini ambaye askofu anampa jukumu) anarejea upya akiwa pamoja na waumini ni nyenzo zipi wanatumia kukamilisha mahitaji yao wenyewe.

22.4.2

Toa Msaada wa Muda kwa ajili ya Mahitaji Muhimu

Lengo la msaada wa Kanisa ni kukidhi kwa muda mahitaji ya msingi wakati waumini wanapojitahidi kujitegemea.

Maaskofu wanapaswa kutumia maamuzi mazuri na kuomba maelekezo ya kiroho wakati wanapozingatia kiasi cha msaada na kiasi cha muda ambao msaada umetolewa. Wanapaswa wawe wenye huruma na wakarimu wakati huohuo wasijenge utegemezi.

22.4.3

Toa Nyenzo au Huduma Badala ya Fedha

Kama inawezekana Askofu anapaswa kuepuka kutoa fedha. Badala yake, anapaswa kutumia matoleo ya mfungo au mipango ya askofu kuwapa waumini mahitaji ya nyumbani au huduma. Waumini wanaweza kisha kutumia pesa zao wenyewe kulipia mahitaji yao mengine.

Wakati hii inapokuwa haitoshi, askofu anaweza kusaidia kwa kutumia matoleo ya mfungo kulipa kwa muda bili muhimu (ona 22.5.2).

22.4.4

Toa Kazi au Fursa za Huduma

Maaskofu wanawaalika wale ambao wanapokea msaada kufanya kazi au kutoa huduma kwa kiwango cha uwezo wao. Hii inawasaidia waumini wadumishe hisia za utu. Pia inaongeza uwezo wao wa kujitegemea.

22.4.5

Tunza Siri kuhusu Taarifa za Msaada wa Kanisa

Askofu na viongozi wengine wa kata wanatunza siri ya taarifa yoyote kuhusu waumini ambao wanaweza kuhitaji msaada wa Kanisa. Hii inalinda faragha na utu wa waumini.

22.5

Sera kwa ajili ya Kutoa Msaada wa Kanisa

Viongozi wa Kanisa wanapaswa kufuata sera zilizowekwa kwenye sehemu hii wakati wanapotoa msaada kupitia matoleo ya mfungo au mipango ya askofu kwa ajili ya chakula na bidhaa zingine za msingi.

22.5.1

Sera Kuhusu Wapokeaji wa Msaada wa Kanisa

22.5.1.1

Msaada kwa Washiriki wa Kata

Kwa ujumla, waumini wanaopokea msaada wa Kanisa wanapaswa kuwa wanaishi katika mipaka ya kata na wawe na kumbukumbu zao za uumini katika kata. Msaada unaweza kutolewa bila kujali kama muumini anahudhuria mara kwa mara mikutano ya Kanisa au anafuata viwango vya Kanisa.

22.5.1.2

Msaada kwa Maaskofu na Marais wa Kigingi

Idhini ya maandishi ya rais wa kigingi inahitajika kabla ya askofu kutumia matoleo ya mfungo au kuidhinisha mipango ya askofu kwa ajili yake au familia yake.

22.5.1.4

Msaada kwa Watu Ambao Siyo Waumini wa Kanisa

Watu ambao siyo waumuni wa Kanisa kwa kawaida hupelekwa kwenye rasilimali za jamii ya mahali husika kwa ajili ya msaada. Mara chache sana kadiri atakavyoongozwa na Roho, askofu anaweza kuwasaidia kwa matoleo ya mfungo au mipango ya askofu.

22.5.2

Sera juu ya Kutumia Matoleo ya Mfungo

22.5.2.1

Tiba au Huduma Zingine za Afya.

Kila eneo la Kanisa limeanzisha mipaka iliyoidhinishwa kwa ajili ya kutumia matoleo ya mfungo kulipa gharama za tiba, tiba ya meno, au afya ya akili.

Kwa ajili ya kuidhinisha kiasi na miongozo, ona “Matumizi ya matoleo ya Mfugo kwa ajili ya Gharama za Tiba.”

22.5.2.3

Marejesho ya Fedha ya Matoleo ya Mfungo

Waumini hawafanyi marejesho ya msaada wa matoleo ya mfungo wanaoupokea kutoka Kanisani.

22.5.2.4

Kiasi cha Matumuzi ya Matoleo ya Mfungo katika Kata

Maaskofu hawatakiwi kuweka ukomo wa msaada wa matoleo ya mfungo kwa ajili ya waumini wa kata kwenye kiasi cha matoleo yaliyokusanywa ndani ya kata.

22.5.3

Sera ya Kufanya Malipo

Kama inawezekana, malipo yanapaswa kulipwa moja kwa moja kwa biashara ambazo zinatoa bidhaa na huduma.

22.5.4

Sera juu ya Malipo Ambayo Yatamnufaisha Askofu au Rais wa Kigingi

Wakati wa kuwapa waumini msaada wa matoleo ya mfungo, askofu anaweza asitumie fedha kulipia bidhaa au huduma kwa njia ambayo itamnufaisha yeye binafsi.

Ikiwa malipo ya matoleo ya mfungo kwa ajili ya muumini yatamnufaisha rais wa kigingi au biashara anayoimiliki, idhini ya Urais wa Eneo inahitajika.

22.6

Wajibu wa Viongozi wa Kata

22.6.1

Askofu na Washauri Wake

Askofu anao wajibu mtakatifu wa kuwatafuta na kuwatunza wale wenye shida ya kimwili (ona Mafundisho na Maagano 84:112). Ananaibisha sehemu kubwa ya kazi hii kwa Urais wa Muungano wa Usaidizi na akidi ya wazee. Hata hivyo, majukumu fulani yanafanywa na askofu pekee. Kwa mfano, askofu:

  • Anaamua aina, kiasi, na muda wa msaada wowote wa kimwili uliotolewa.

  • Anaidhinisha msaada wa matoleo ya mfungo (ona 22.4 na 22.5) na mipango ya askofu kwa ajili ya chakula na bidhaa zingine za msingi (ona 22.13).

  • Yeye binafsi anapitia upya mipango ya waumini ya kujitegemea. Anawapangia viongozi wengine wa kata kufuatilia mipango hiyo kama inavyotakiwa.

Askofu na Washauri Wake wana majukumu yafuatayo:

  • Kufundisha kanuni na baraka zenye uhusiano na (1)Kuwatunza wale ambao wana mahitaji ya kimwili na kihisia na (2) kukuza kujitegemea (ona 22.1).

  • Kufundisha sheria ya mfungo na kuwatia moyo waumini watoe matoleo ya mfungo kwa ukarimu (ona 22.2.2).

  • Kusimamia ukusanyaji na hesabu za matoleo ya mfungo (ona 34.3.2).

22.6.2

Urais wa Muungano wa Usaidizi na Akidi ya Wazee

Chini ya maelekezo ya askofu, Muungano wa Usaidizi na Akidi ya Wazee wanalo jukumu muhimu katika kuwatunza wale wenye mahitaji katika kata (ona 8.2.2 na 9.2.2). Viongozi hawa wanawafundisha waumuni wa kata:

  • Kuwahudumia wale wenye mahitaji.

  • Kuishi sheria ya mfungo.

  • Kukuza kujitegemea

  • Kuongeza matayarisho ya mtu binafsi na familia.

22.6.3

Akina kaka na akina dada wahudumiaji

Usaidizi wa mahitaji ya kiroho na kimwili mara nyingi unaanza na akina kaka na akina dada wahudumiaji (ona 21.1). Wanatoa taarifa juu ya mahitaji ya wale ambao wanawahudumia kwa urais wao wa akidi ya wazee au Muungano wa Usaidizi katika mahojiano ya uhudumiaji na nyakati zingine. Wanaweza kumwambia askofu moja kwa moja juu ya mahitaji ambayo ni ya faragha.

22.7

Jukumu la Baraza la Kata

Jukumu muhimu la Baraza la Kata ni kupanga jinsi ya kuwatunza wale wenye mahitaji na kuwasaidia wawe wenye kujitegemea (ona 4.4). Washiriki wa baraza wanaweka msingi wa mipango hii kwenye taarifa kutoka kwenye usaili wa kuhudumu na kutokana na mawasiliano yao binafsi na wale wenye mahitaji. Katika kujadiliana mahitaji ya waumini, baraza linaheshimu matamanio ya yeyote anayeomba usiri.

22.8

Jukumu la Baraza la Vijana katika Kata

Kusudi moja la baraza la vijana la kata ni kuwasidia vijana wawe wafuasi waliowekwa wakfu wa Yesu Kristo (ona 29.2.6).

Chini ya mwongozo wa uaskofu, baraza la Vijana la kata linapanga njia za kuwahudumia wale wenye shida katika kata na jamii yao.