Vitabu vya Maelekezo na Miito
21. Uhudumiaji


“21. Kuhudumu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“21. Kuhudumu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
wanaume wakiinua mwamba

21.

Uhudumiaji

21.0

Utangulizi

Kuhudumu maana yake ni kuwatumikia wengine kama Mwokozi alivyofanya (ona Mathayo 20:26–28).

Bwana anawataka waumini wote wa Kanisa Lake wapokee uangalizi kama huo. Kwa sababu hii, wanaoshikilia ukuhani wamepangiwa kama akina kaka wahudumiaji kwa kila kaya. Akina dada wahudumiaji wamepangiwa kwa kila dada mtu mzima.

21.1

Majukumu ya akina Dada na akina Kaka Wahudumiaji

Akina dada na akina kaka wahudumiaji wana majukumu yafuatayo kwa watu binafsi na familia walizopangiwa.

  • Kuwasaidia waimarishe imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Kuwasaidia wajitayarishe kufanya na kushika maagano matakatifu na Mungu pale wanapopokea ibada.

  • Kutambua mahitaji na kutoa upendo kama wa Kristo, kuwajali, na kuwahudumia.

  • Kuwasaidia wawe wenye kujitegemea kiroho na kimwili.

21.2

Upangaji wa Kazi za Uhudumiaji

21.2.1

Upangaji wa Majukumu

Urais wa akidi ya wazee na Urais wa Muungano wa Usaidizi kwa sala hufikiria majukumu kwa ajili ya akina kaka na akina dada wahudumiaji. Kwa kawaida huwapanga akina kaka wawili au akina dada wawili kama mtu na mwenzake. Wanatafuta idhini ya askofu kwa ajili ya mtu na mwenzake na majukumu.

Wanandoa wanaweza kupangiwa kuhudumu pamoja kwa mtu binafsi au familia.

Akina kaka na akina dada wahudumiaji hawaitwi, kukubaliwa, au kusimikwa.

21.2.2

Kazi za Uhudumiaji kwa Vijana

Msichana anaweza kuhudumu kama mhudumu mwenza kwa dada wa Muungano wa Usaidizi wakati msichana anapokuwa tayari na anaweza kufanya hivyo. Anaweza kuanza kuhudumu katika mwaka anaofikisha miaka 14.

Mvulana anahudumu kama mhudumu mwenza kwa anayeshikilia Ukuhani wa Melkizedeki wakati anapotawazwa kwenye ofisi ya mwalimu au kuhani.

21.3

Mahojiano juu ya Uhudumiaji

Rais wa akidi ya wazee na washauri wake wanawasaili akina kaka wahudumiaji. Rais wa Muungano wa Usaidizi na washauri wake wanawasaili akina dada wahudumiaji.

Usaili huu hufanyika angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

Madhumuni yake ni:

  • Kushauriana kuhusu uimara, mahitaji, na changamoto za watu binafsi na familia walizopangiwa.

  • Kujadili njia za kuwasaidia watu wajitayarishe kupokea ibada kama inahitajika.

  • Kufikiria jinsi gani akidi ya wazee, Muungano wa Usaidizi, baraza la kata, na wengine wanavyoweza kusaidia.

  • Kuwafundisha na kuwatia moyo akina kaka na akina dada wahudumiaji.

21.4

Kuratibu Jitihada za Uhudumiaji

Urais wa Muungano wa Usaidizi na Urais wa Akidi ya Wazee wanakutana pamoja angalau kila robo ya mwaka. Wanarejelea yale waliyojifunza katika usaili wao wa kuhudumu (ona 21.2 Pia wanaratibu upangaji wa majukumu ya kuhudumu.

Katika vitengo vyenye waumini wachache wanaoshiriki kikamilifu, urais wa Muungano wa Usaidizi na urais wa akidi ya wazee wanaweza kuamua kutowapangia baadhi ya waumini akina kaka na akina dada wahudumiaji.