Vitabu vya Maelekezo na Miito
20. Shughuli


“20. Shughuli,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“20. Shughuli,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
msichana akiwa na bunduki ya maji

20.

Shughuli

20.1

Madhumuni

Shughuli za Kanisa zinawaleta waumini wa Kanisa na wengine pamoja kama “wenyeji” pamoja na watakatifu” (Waefeso 2:19). Madhumuni ya Shughuli yanaweza kujumuisha yafuatayo:

  • Kujenga imani katika Yesu Kristo.

  • Kutoa burudani na kukuza umoja.

  • Kutoa fursa kwa ajili ya ukuaji binafsi.

  • Kuwaimarisha watu binafsi na familia.

  • Kuwasaidia waumini washiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona 1.2).

20.2

Kupanga Shughuli

Kabla ya kupanga shughuli, viongozi wanafikiria mahitaji ya kiroho na kimwili ya waumini wao. Viongozi wanatafuta mwongozo wa Roho wakati wanapoamua ni aina gani ya shughuli itasaidia kukamilisha mahitaji hayo.

20.2.1

Majukumu kwa ajili ya Kupanga Shughuli

Shughuli za kata zinaweza kupangwa katika moja ya njia zifuatazo, kutokana na mahitaji ya mahali husika:

  • Baraza la kata linaweza kusimamia upangaji.

  • Baraza la kata linaweza kuvipangia vikundi maalumu kusaidia kupanga shuguli moja au zaidi.

  • Zinapohitajika na pale palipo na waumini wa kutosha, uaskofu unaweza kupanga kamati ya shughuli za kata.

Kwa maelezo kuhusu kupanga shughuli za vijana katika kata, ona 10.2.1.3 na 11.2.1.3.

20.2.2

Kuwaalika Wote Kushiriki

Wale wanaopanga shughuli wanapaswa kuwafikia wote hususani waumini wapya, wasioshiriki kikamilifu, vijana watu wazima waseja, watu wenye ulemavu, na watu wa imani zingine.

Shughuli hazipaswi kuweka mizigo isiyo ya lazima kwa viongozi au waumini.

20.2.3

viwango

Shughuli za Kanisa zinapaswa kuwa zenye kuinua na kutilia mkazo kile kilicho “chema, chenye kupendeza, au chenye taarifa njema au chenye kustahili sifa” (Makala ya Imani 1:13). Shughuli zisijumuishe chochote ambacho ni kinyume na mafundisho ya Kanisa.

20.2.6

Kugharamia Shughuli

Shughuli nyingi zinapaswa kuwa rahisi na zenye gharama ndogo au bila gharama. Matumizi lazima yapate kibali mapema kutoka kwa uaskofu au urais wa kigingi.

Waumini kwa kawaida hawapaswi kulipa ili washiriki katika shughuli. Kwa ajili ya sera na miongozo juu ya kugharamia shughuli, ona 20.6.

20.4

Mkutano wa Vijana

Kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 14 wavulana na wasichana wanaaalikwa kushiriki pamoja katika mkutano wa vijana. Mikutano ya vijana kwa kawaida inafanyika mara moja kwa mwaka kwenye ngazi ya kata au kigingi. Inaweza kufanyika pia kwenye ngazi ya vigingi vingi au eneo. Katika mwaka ambao vijana wanapangiwa kuhudhuria mkutano wa KNV, vigingi, na kata havipaswi kufanya mikutano.

Mikutano ya vijana ya kata inapangwa na kufanywa na baraza la Vijana la Kata chini ya maelekezo ya uaskofu (ona 29.2.6). Uaskofu unapata idhini ya urais wa kigingi juu ya mipango kwa ajili ya mkutano wa vijana wa kata.

Wakati viongozi na vijana wanapopanga mkutano wa vijana, wanapaswa kuzingatia sera katika sura hii na miongozo ifuatayo:

  • Dhima ya mwaka ya vijana wa Kanisa inaweza kutumika kama kauli mbiu ya mkutano.

  • Kupanga shughuli ambazo zinalingana na dhima hii.

  • Kupata kibali cha uaskofu au urais wa kigingi kwa ajili ya wazungumzaji wote na shughuli.

  • Kuhakikisha usimamizi wa kutosha wa watu wazima nyakati zote (ona 20.7.1).

20.5

Sera na Miongozo kwa ajili ya Kuchagua na Kupanga Shughuli

20.5.1

Shughuli za Kibiashara au Kisiasa

Shughuli zinazofanyika kwa dhumuni lolote la kibiashara au kisiasa haziruhusiwi (ona 35.5.2).

20.5.2

Dansi na Muziki

Katika dansi zote, mavazi, taa, mitindo ya kucheza dansi, maneno ya wimbo, na muziki vinapaswa kuchochea mazingira ambayo Roho wa Bwana anaweza kuwepo.

20.5.3

Usiku wa Jumatatu

Waumini wanahimizwa kufanya shughuli za kifamilia siku ya Jumatatu au nyakati zingine. Hakuna shughuli za Kanisa, mikutano, au huduma za ubatizo zinazopaswa kufanyika baada ya saa 12:00 jioni siku za Jumatatu.

20.5.5

Shughuli za Usiku kucha

shughuli za usiku kucha kwa ajili ya vikundi vilivyounganishwa vya wavulana na wasichana lazima viwe vimeidhinishwa na askofu na rais wa kigingi. Hiyo ni kweli pia kwa shughuli za waumini waseja wanaume na wanawake.

Shughuli za usiku kucha kwenye nyumba za mikutano ya Kanisa au viwanja vya nyumba ya mikutano haziruhusiwi.

20.5.8

Kuitii Siku ya Sabato

Hakuna kambi za Kanisa, matukio ya michezo, au matukio ya burudani yatakayopangwa kufanyika siku ya Jumapili. Wala vikundi vya vijana na watu wengine hawapaswi kusafiri kwenda au kutoka kwenye makambi au mikutano mikuu ya vijana siku ya Jumapili.

20.5.10

Kutembelea Hekalu

Kutembelea hekalu kunapangwa na kata au ngazi ya kingingi ndani ya eneo la wilaya ya hekalu iliyopangwa.

20.6

Sera na Miongozo kwa ajili ya Kugharamia Shughuli

20.6.1

Shughuli Zinazolipiwa na Fedha za Bajeti ya Kata au Kigingi

Fedha za bajeti za kata au kigingi zinapaswa kutumika kulipia shughuli zote—kwa uwezekano wa upekee ulioorodheshwa katika 20.6.2.

20.6.2

Gharama kwa ajili ya Kambi za Vijana

Kama bajeti za kata au kigingi hazina fedha za kutosha kwa ajili ya shughuli zilizoorodheshwa hapo chini, viongozi wanaweza kuwaomba washiriki kulipia sehemu ya gharama au gharama zote.

  • Kambi moja kubwa ya kila mwaka ya Ukuhani wa Haruni au shughuli kama hiyo.

  • Kambi moja kubwa ya kila mwaka ya wasichana au shughuli kama hiyo.

  • Kambi ya siku moja ya kila mwaka au shughuli kama hiyo kwa ajili ya watoto wa Msingi wenye umri wa miaka 8 mpaka 11

Gharama au usafiri kwa ajili ya kambi ya kila mwaka haipaswi kuwa ghali. Ukosefu wa fedha kwa mtu binafsi haupaswi kumzuia muumini yeyote kutokushiriki.

20.6.3

Kulipia Gharama za Mkutano wa KNV

Vijana wanaweza kuombwa kuchangia ada ya kuhudhuria mikutano ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (KNV). Kama gharama zitamzuia kijana kushiriki, askofu anaweza kutumia fedha ya bajeti ya kata kulipa ada yote au sehemu ya ada hii. Ona FSY.ChurchofJesusChrist.org.

20.6.5

Matukio ya Kuchangisha Fedha.

Matumizi kwa ajili ya shuguli za kigingi na kata kwa kawaida yanalipwa na fedha za bajeti. Hata hivyo, rais wa kata au askofu anaweza kuidhinisha tukio moja la uchangishaji wa fedha kila mwaka kwa ajili ya madhumuni yafuatayo pekee:

  • Kusaidia kulipia shughuli zilizoorodheshwa katika 20.6.2.

  • Kusaidia kununua vifaa ambavyo kitengo kinahitaji kwa ajili ya kambi za mwaka.

20.7

Sera za Usalama na Miongozo kwa ajili ya Shughuli

20.7.1

Usimamizi wa Watu Wazima

Angalau watu wazima wawili lazima wawepo kwenye shughuli zote za Kanisa zinazohudhuriwa na watoto na vijana. Watu wazima wa ziada wanaweza kuhitajika kutegemea na ukubwa wa kundi, utaalamu unaohitajika kwa ajili ya shughuli hiyo, au sababu nyinginezo. Wazazi wanahimizwa kusaidia.

Wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana. Ona ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org.

20.7.2

Mahitaji ya Umri kwa ajili ya Ushiriki katika Shughuli za Vijana

Kwa idhini ya wazazi wao, vijana wanaweza kuhudhuria kambi za usiku kucha kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 12. Wanaweza kuhudhuria dansi, mikutano ya vijana, na mikutano ya KNV kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 14.

20.7.4

Ruhusa ya Wazazi

Watoto na vijana yanawezekana wasishiriki katika shughuli za Kanisa bila idhini ya wazazi au walezi wao. Kwa ajili ya shughuli za Kanisa ambazo zinajumuisha kukaa usiku kucha, safari ndefu, au hatari za juu kuliko za kawaida, ruhusa ya kimaandishi ni muhimu.

Wazazi na walezi wanatoa ruhusa hii kwa kusaini Ruhusa na fomu ya Ruhusa ya Tiba

20.7.5

Taarifa za Unyanyasaji

Unyanyasaji wowote unaotokea wakati wa shughuli ya Kanisa unapaswa kuripotiwa kwa mamlaka za serikali. Askofu anapaswa kufahamishwa mara moja. Maelekezo kwa ajili ya waumini yapo katika 38.6.2.7. Maelekezo kwa ajili ya maaskofu yapo katika 38.6.2.1.

20.7.6

Tahadhari za Usalama, Kushughulikia Ajali, na Kuripoti Ajali

20.7.6.1

Tahadhari za Usalama

Viongozi na washiriki kwa makini wanaitathmini shughuli kuhakikisha kuwa kuna kiwango kidogo sana cha hatari ya kuumia au ugonjwa. Shughuli zinapaswa pia kuhusisha kiwango kidogo sana cha hatari ya uharibifu wa mali. Wakati wa shughuli, viongozi wafanye kila juhudi kuhakikisha kuna usalama.

20.7.6.2

Kushughulikia Ajali

Kama ajali au dhara linatokea kwenye mali za Kanisa au wakati wa shughuli za Kanisa, viongozi wazingatie miongozo ifuatayo, kadiri inavyohusika:

  • Toa huduma ya kwanza. Kama mtu anahitaji uangalizi wa kitabibu, wasiliana na huduma za dharura za tiba. Pia wasiliana na mzazi, mlezi, au ndugu mwingine wa karibu na askofu au rais wa kigingi.

  • Kama mtu fulani amepotea au anakufa, mara moja fahamisha vyombo vya usalama vya eneo husika.

  • Toa msaada wa kihisia.

  • Usihimize au kupuuzia hatua za kisheria. Usitoe ahadi kwa niaba ya Kanisa.

  • Kusanya na tunza majina ya mashahidi, taarifa za mawasiliano yao, maelezo ya nini kilitokea na picha.

  • Toa taarifa ya ajali (ona 20.7.6.3).

20.7.6.3

Kutoa Taarifa ya Ajali

Hali zifuatazo zinapaswa kutolewa Taarifa mtandaoni kwenye incidents.ChurchofJesusChrist.org.

  • Ajali au dhara linatokea kwenye mali ya Kanisa au wakati wa shughuli za Kanisa.

  • Mtu aliyekuwa anashiriki katika shughuli za Kanisa amepotea.

  • Mali ya mtu binafsi, ya umma, au ya Kanisa imeharbika wakati wa shughuli ya Kanisa.

  • Hatua ya kisheria inatishiwa au inatarajiwa.

Kama tukio linasababisha madhara makubwa, mauti, au mtu kupotea, rais wa kigingi askofu, au mshiriki anayemteua mara moja anaitaarifu ofisi ya eneo.

20.7.6.4

Bima na Maswali

Kama jeraha linatokea wakati wa tukio la Kanisa, viongozi wanaamua ikiwa Programu ya Msaada wa Tiba kwa Shughuji za Kanisa inatumika.

Katika baadhi ya hali, rais wa kigingi au askofu anaweza kuwa na maswali kuhusu masuala ya usalama au madai dhidi ya Kanisa. Rais wa kigingi (au askofu chini ya maelekezo yake) anapeleka maswali kama hayo kwenye Kitengo cha Menejimenti ya Hatari au kwenye ofisi ya eneo.

20.7.7

Usafiri

Usafiri kwa shughuli za Kanisa unapaswa kuidhinishwa na askofu au rais wa kigingi. Usafiri huu haupaswi kuweka mizigo isiyostahili juu ya waumini. Usafiri wa umbali mrefu kwa ajili ya shughuli hauhamasishwi.

Inapowezekana vikundi vya Kanisa vinapaswa kutumia usafiri wa kibiashara kwa ajili ya usafiri wa umbali mrefu. Usafiri napaswa kuwa una leseni na unalindwa na bima.

Wakati vikundi vya Kanisa vinasafiri na magari binafsi ya abiria kila gari lazima liwe katika hali salama ya utendaji kazi. Kila mtu anapaswa kutumia mkanda wa kiti. Kila dereva anapaswa kuwa mwenye leseni, mtu mzima mwenye kuwajibika.