Vitabu vya Maelekezo na Miito
19. Muziki


“19. Muziki,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“19. Muziki,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
mwanamke na mtoto wakipiga piano

19.

Muziki

19.1

Madhumuni ya Muziki katika Kanisa

Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo “Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za staha, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

19.2

Muziki ndani ya Nyumba

Kupitia manabii Wake, Bwana amewahimiza watu binafsi na familia kutumia muziki unaoinua katika maisha yao ya kila siku.

Miziki ya Kanisa iliyorekodiwa inapatikana kutoka katika vyanzo vifuatavyo:

19.3

Muziki katika Mikutano ya Kanisa

19.3.1

Kupanga Muziki kwa ajili ya Mikutano ya Kanisa

Waratibu wa Muziki katika kata na Vigingi wanafanya kazi na viongozi wa ukuhani kupanga muziki kwa ajili ya huduma za ibada. Wanachagua muziki ambao unachochea roho wa kuabudu katika mikutano.

19.3.2

Muziki katika Mkutano wa Sakramenti

Muziki katika mkutano wa sakramenti unajumuisha kusanyiko kuimba nyimbo za dini ili kufungua na kufunga mkutano na kabla ya utoaji wa sakramenti. Wimbo wa dini wa sakramenti unapaswa kurejelea kwenye sakramenti yenyewe au kwenye dhabihu ya Mwokozi.

Muziki wa utangulizi unapigwa pale waumini wanapokusanyika kabla ya mkutano kuanza. Baada ya sala ya kufunga, muziki wa ala unapigwa wakati waumini wanapoondoka mkutanoni.

Mkutano wa sakramenti unaweza pia kujumuisha wimbo wa dini wa ziada utakaoimbwa katikati ya mkutano—kwa mfano, kati ya jumbe zitakazo zungumzwa.

19.3.3

Muziki katika Madarasa na Mikutano Mingine ya Kata

Viongozi wanawahimiza walimu kutumia nyimbo za dini na muziki mwingine mtakatifu kuimarisha mafundisho yao.

19.3.6

Vifaa vya Muziki

Vifaa mubashara kwa kawaida vinatumika kwa ajili ya muziki wa utangulizi na wa kufunga na kwa ajili ya kiambata cha wimbo wa dini katika mikutano ya Kanisa. Pale ambapo vinapatikana na pale ambapo waumini wanaweza kuvipiga, vinanda na piano ni zana zenye kiwango. Uaskofu unaweza kuidhinisha matumizi ya vifaa vingine kuendana na uimbaji wa mkutano, kwa ajili ya muziki wa utangulizi na wa baada ya mkutano kufunga, na chaguzi zingine za muziki.

Kama piano, kinanda, au mpigaji hayupo, muziki uliorekodiwa unaweza kutumika (ona 19.2).

19.3.7

Kwaya

19.3.7.1

Kwaya za Kata

Pale walipo waumini wa kutosha, kata zinaweza kuanzisha kwaya ambazo zinaimba katika mikutano ya sakramenti mara kwa mara.

Kwa nyongeza kwenye kwaya ya kata, familia na vikundi vya wanawake, wanaume, vijana, au watoto vinaweza kualikwa kuimba katika mikutano ya kanisa.

19.4

Uongozi wa Muziki katika Kata

19.4.1

Uaskofu

Askofu anawajibika kwa muziki wa kata. Anaweza kumpangia jukumu hili mmoja wa washauri wake.

19.4.2

Mratibu wa Muziki katika Kata

Mratibu wa muziki katika kata anahudumu chini ya maelekezo ya askofu. Yeye ana wajibu ufuatao:

  • Kuwa nyenzo kwa uaskofu na viongozi wengine katika kata kwenye masuala ya Muziki.

  • Anafanya kazi na uaskofu kupanga muziki kwa ajili ya mikutano ya sakramenti (ona 19.3.1 na 19’3’1).

  • Kama itakavyoombwa na uaskofu, anapendekeza waumini ili kuhudumu katika miito ya muziki katika kata. Anawaelekeza wale wanaohudumu katika miito hii, akiwapatia usaidizi, maelekezo na mafunzo kadiri inavyohitajika.

19.4.3

Miito ya ziada

Uaskofu unaweza kuwaita waumini kuhudumu katika miito ifuatayo.

19.4.3.1

Kiongozi wa Muziki katika Kata

Kiongozi wa muziki anaongoza nyimbo za dini za kuimbwa na mkutano kwa ajili ya mkutano wa sakramenti na kwa ajili ya mikutano mingine ya kata kama itakavyoombwa.

19.4.3.2

Mpiga Kiambata cha Ala

Mpiga kiambata cha ala katika kata anatoa muziki wa utangulizi na wa baada ya kufunga na kiambata kwa ajili ya nyimbo za dini wakati wa mkutano wa sakramenti na mikutano mingine ya kata kama itakavyoombwa.

19.7

Miongozo ya Ziada na Sera

19.7.2

Matumizi ya Vifaa vya Nyumba ya mikutano kwa ajili ya Mazoezi, Maelekezo Binafsi, na Mazoezi ya Kukariri

Wakati panapokuwa hakuna mbadala wenye kuleta maana, viongozi wa ukuhani wanaweza kuruhusu matumizi ya piano na vinanda vya nyumba ya mkutano vitumike kwa ajili ya mazoezi, mafunzo binafsi yaliyolipiwa, na mazoezi ya kukariri yanayowahusu washiriki wa vitengo ambavyo vinatumia nyumba ya mkutano.