Vitabu vya Maelekezo na Miito
Akidi ya Wazee


“8. Akidi ya Wazee,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“8. Akidi ya Wazee “ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
wanaume wakizungumza

8.

Akidi ya Wazee

8.1

Dhumuni na Muundo

8.1.1

Dhumuni

Wanaume wanaostahili wenye umri wa miaka18 na zaidi wanaweza kupokea Ukuhani wa Melkizedeki na kutawazwa kwenye ofisi ya mzee. Mwanamume aliyetawazwa kwenye ofisi hiyo anaingia katika agano takatifu kumsaidia Mungu katika kukamilisha Kazi Yake (ona Mafundisho na Maagano 84:33-44).

8.1.2

Ushiriki katika Akidi ya Wazee

Kila kata ina akidi ya wazee. Inajumuisha akina kaka wafuatao:

  • Wazee wote katika kata.

  • Wazee watarajiwa wote katika kata ( ona 8.4..

  • Makuhani wakuu wote katika kata, isipokuwa wale ambao kwa sasa wana hudumu kwenye urais wa kigingi, katika uaskofu, kwenye baraza kuu, au kama patriaki.

Kijana anaweza kuanza kuhudhuria mikutano ya akidi ya wazee anapofikisha miaka 18, hata kama bado hajatawazwa kuwa mzee. Katika umri wa miaka 19 au unapohama kutoka nyumbani, kama vile kuhudhuria masomo ya chuo kikuu au kuhudumu misheni, kijana anapaswa kutawazwa mzee kama anastahili.

Wanaume waliooa chini ya miaka 18 ni wazee watarajiwa na pia ni washiriki wa akidi ya wazee.

8.2

Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

8.2.1

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

8.2.1.2

Kujifunza Injili katika Mikutano ya Akidi

Mikutano inafanyika katika Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi. Inadumu kwa dakika 50. Urais wa Akidi ya Wazee unapanga mikutano hii. Mshiriki wa urais anaendesha.

Mikutano ya Akidi inalenga kwenye mada katika moja au zaidi ya hotuba kutoka mkutano mkuu wa hivi karibuni.

8.2.1.3

Shughuli

Urais wa akidi ya wazee unaweza kupanga shughuli. Shuguli nyingi zinafanyika katika siku tofauti na Jumapili au Jumatatu.

8.2.2

Kuwajali Wale Wenye Mahitaji.

8.2.2.1

Uhudumiaji

Washiriki wa akidi ya wazee wanapokea kazi za uhudumiaji kutoka kwa urais wa akidi. Kwa maelezo zaidi, ona sura ya 21.

8.2.2.2

Mahitaji ya muda mfupi

Akina kaka wahudumiaji wanatafuta kuelewa na kutoa majibu ya shida za wale wanaowatumikia. Waumini wanaweza kuhitaji msaada wa muda mfupi nyakati za ugonjwa, uzazi, vifo, upotevu wa kazi, na hali zingine.

Wanapohitajika, akina kaka wahudumiaji wanaomba msaada kwa urais wa akidi ya wazee.

8.2.2.3

Mahitaji ya Muda Mrefu na Kujitegemea

Kama ilivyoratibiwa na askofu, urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi wanawasaidia Waumini kwa mahitaji ya muda mrefu na kujitegemea.

Rais wa akidi ya wazee, rais wa Muungano wa Usaidizi, au kiongozi mwingine anamsaidia mtu huyo au familia kuanzisha Mpango wa Kujitegemea. Akina kaka au akina dada wahudumiaji wanaweza pia kusaidia kwenye mpango huo.

8.2.2.4

Wakati Muumini wa Kata Anapofariki

Wakati muumini wa Kata anapofariki, Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanatoa faraja na msaada. Chini ya mwongozo wa askofu, wanaweza kusaidia kwenye mazishi.

Kwa maelezo zaidi, ona 38.5.8.

8.2.3

Kuwaalika Wote Waipokee Injili

Rais wa akidi ya wazee anampangia mshiriki mmoja wa urais kusaidia kuongoza kazi ya umisionari kwa waumini katika kata. Anafanya kazi na mshiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi aliyepangiwa ili kuratibu juhudi hizi.

Ona 23.5:1 na 23.5:3.

8.2.4

Kuziunganisha Familia Milele

Rais wa akidi ya wazee anampangia mshiriki wa urais kusaidia kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata. Anafanya kazi na mshiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi aliyepangiwa ili kuratibu juhudi hizi.

Ona 25.2:2.

8.3

Viongozi wa Akidi ya Wazee

8.3.1

Uraisi wa Kigingi na Askofu

Rais wa akidi ya Wazee anawajibika moja kwa moja kwa urais wa kigingi. Anakutana mara kwa mara na mshiriki wa urais ili kupokea maelekezo na kuripoti juu ya wajibu wake.

Rais wa akidi ya wazee pia anapokea mwongozo kutoka kwa askofu, ambaye ni afisa anayeongoza katika kata. Wanakutana mara kwa mara.

8.3.2

Mjumbe wa Baraza Kuu

Urais wa kigingi unampangia mjumbe wa baraza kuu kuwawakilisha katika kila akidi ya wazee. Majukumu yake yameelezwa kwa muhtasari katika 6.5..

8.3.3

Urais wa Akidi ya Wazee

8.3.3.1

Kuita Urais wa Akidi ya Wazee

Baada ya kushauriana na askofu, rais wa kigingi anamwita mzee au kuhani mkuu kuhudumu kama rais wa akidi ya wazee.

Kama kitengo ni kikubwa vya kutosha rais wa akidi ya wazee anampendekeza kwa rais wa kigingi mzee au kuhani mkuu mmoja au wawili kuhudumu kama washauri wake.

8.3.3.2

Majukumu:

Rais wa akidi ya wazee ana majukumu yafuatayo. Washauri wake wanamsaidia.

  • Kuhudumu kwenye baraza la kata.

  • Kuongoza juhudi za akidi kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona sura ya 1).

  • Kuratibu na kusimamia huduma ya akina kaka wahudumiaji.

  • Chini ya mwongozo wa askofu, anashauriana na waumini watu wazima wa kata.

  • Kuratibu juhudi za akidi ya wazee za kuwaimarisha akina kaka vijana wakubwa, wote waseja na waliooa.

  • Kukutana binafsi na kila mshiriki wa akidi angalau mara moja kwa mwaka.

  • Kuwafundisha washiriki wa akidi kazi zao za ukuhani (ona Mafundisho na Maagano 107:89). Hii inajumuisha kuwafundisha jinsi gani ya kutumia ukuhani wao katika kufanya ibada na kutoa baraka.

  • Kusimamia rekodi za akidi, ripoti, na fedha (ona LCR.ChurchofJesusChrist.org).

8.3.3.3

Mkutano wa Urais

Urais wa akidi ya wazee na katibu hukutana mara kwa mara. Rais huendesha mikutano hii. Mjumbe wa baraza kuu ailiyepangwa kwenye akidi anahudhuria mara moja moja.

Ajenda inaweza kujumuisha mambo yafuatayo:

  • Kupanga jinsi ya kuwaimarisha washiriki wa akidi (ikijumuisha wazee watarajiwa) na familia zao.

  • Kuratibu kazi ya umisionari na kazi ya hekaluni na historia ya familia.

  • Kushughulikia majukumu kutoka katika mikutano ya baraza la kata.

  • Kurejelea upya taarifa kutoka katika mahojiano na wahudumiaji.

  • Kuwafikiria akina kaka wa kuhudumu katika miito na majukumu mengineyo.

  • Kupanga mikutano na shughuli za akidi.

8.3.4

Katibu

Kwa idhini ya askofu, mshiriki wa urais wa akidi ya wazee anaweza kumwita mshiriki wa akidi awe katibu wa akidi.

8.4

Kuwasaidia Wazee Watarajiwa Wajiandae Kupokea Ukuhani wa Melkizedeki

Mzee mtarajiwa ni muumini wa Kanisa mwanamume ambaye hajapokea Ukuhani wa Melkizedeki na (1) ni mwenye umri wa miaka 19 au zaidi au (2) chini ya miaka 19 na ameoa.

Kuwasaidia wazee watarajiwa wajiandae kupokea Ukuhani wa Melkizedeki ni moja ya vipaumbele vya juu sana vya urais wa akidi.