Dhima
Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni


Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

Mimi ni mwana mpendwa wa Mungu, na Yeye anayo kazi ya kufanywa na mimi.

Kwa moyo, uwezo, akili na nguvu zangu zote, nitampenda Mungu, nitashika maagano yangu, na kutumia ukuhani Wake ili kuwatumikia wengine, nikianzia nyumbani mwangu mwenyewe.

Pale ninapojitahidi kutumikia, kutumia imani, kutubu, na kujiboresha kila siku, nitastahili kupokea baraka za hekaluni na furaha ya kudumu ya injili.

Nitajitayarisha kuwa mmisionari mwenye juhudi, mume mwaminifu, na baba mwenye upendo kwa kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

Nitasaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi kwa kuwaalika wote kuja kwa Kristo na kupokea baraka za Upatanisho Wake.