2023
Baraka za Patriaki
Mei 2023


Baraka za Patriaki

Picha
wavulana

Ecuador

Baraka Yako ya Patriaki—Mwelekeo wenye mwongozo wa kiungu kutoka kwa Baba wa Mbinguni

Na Mzee Randall K. Bennett

Wa Sabini

Baraka yangu ya patriaki ilikuwa ya muhimu sana kwangu nilipokuwa mdogo kwa sababu kadhaa. Kwanza, kupitia nguvu ya Roho Mtakataifu, baraka yangu ya patriaki ilinisaidia nielewe utambulisho wangu wa kweli wa milele—nilikuwa nani hasa na ningeweza kuwa nani. Nilijua kwamba nilijulikana na kupendwa na Baba yangu wa Mbinguni na Mwokozi wangu na kwamba Wao walijihusisha binafsi katika maisha yangu. Hii ilinisaidia nisogee karibu zaidi na Wao na niongeze imani yangu na tumaini Kwao. …

Kujua mimi nilikuwa nani hasa kulinisaidia nielewe na nitamani kufanya kile Mungu alichotarajia juu yangu.

Hii iliniongoza kujifunza maagano niliyokuwa nimefanya na baraka zilizoahidiwa katika agano la Mungu na Ibrahimu. Ilinipa mtazamo wa milele ambao ulinishawishi mimi kuyashika maagano yangu kwa ukamilifu.

Ilikuwa muhimu kwangu kupokea baraka yangu ya patriaki wakati nikiwa mdogo na wakati ambapo ushuhuda wangu ulikuwa bado unakua. …

… Kuthamini baraka yangu ya patriaki nikiwa bado mdogo kulinibariki kwa ujasiri wakati nilipokata tamaa, faraja nilipopata hofu, amani nilipohisi wasiwasi, tumaini nilipokosa tumaini na shangwe pale nilipoihitaji zaidi. Baraka yangu ya patriaki ilisaidia nikuze imani yangu na tumaini kwa Baba yangu wa Mbinguni na Mwokozi wangu. Pia iliongeza upendo wangu Kwao—na bado inafanya hivyo.

Wakati Sahihi wa Kupokea Baraka Yako ya Patriaki

Na Mzee Kazuhiko Yamashita

Wa Sabini

Wapendwa wavulana na wasichana wangu, wazazi na maaskofu, baraka za patriaki siyo tu kwa maandalizi ya kwenda kuhudumu misheni. Waumini waliobatizwa wenye kustahili wanaweza kupokea baraka zao za patriaki wakati muda unapokuwa sahihi kwao. …

Akina kaka na akina dada, ninatoa ushahidi wangu kwamba Baba wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa na Mzaliwa wa Pekee, Bwana Yesu Kristo, wako hai. Wanatupenda. Baraka za patriaki ni zawadi takatifu kutoka Kwao. Unapopokea baraka yako, utatambua na kuhisi jinsi gani Wao wanavyokupenda wewe na jinsi wanavyofokasi juu yako wewe binafsi.