2021
Shiriki hadithi yako kwenye kurasa za eneo za Liahona
Julai 2021


Shiriki Hadithi Yako

Shiriki hadithi yako kwenye kurasa za eneo za Liahona

Je, una uzoefu binafsi wa kukuza imani ambao ungependa kuushiriki?

Tunataka kusikia kutoka kwako!

Ikiwa wewe ni muumini mwaminifu wa Kanisa katika Afrika ya Kati ambaye umekuwa imara au umejifunza jambo jipya kupitia uzoefu binafsi, tungependa kusikia kutoka kwako.

Mahususi, unakaribishwa kushiriki uzoefu binafsi kwenye dhamira za Mpango wa Eneo wa 2021, ambazo zinajumuisha:

  • Kukuza imani katika Yesu Kristo

  • Kujifunza Kitabu cha Mormoni

  • Kuitakasa Siku ya Sabato

  • Kushiriki injili

  • Kuwaimarisha waumini wapya

  • Kuwarejesha wasioshiriki kikamilifu

  • Kufanya historia ya familia na kupeleka majina ya familia hekaluni

  • Kujitayarisha kuhudumu misheni

  • Kulipa zaka kwa uaminifu

  • Kuishi sheria ya mfungo

Nini cha kufanya:

  • Andika uzoefu wako kwa uwazi na kwa urahisi, ukiweka fokasi yako kwenye kanuni za injili.

  • Hadithi yako haipaswi kuwa na maneno zaidi ya 800.

  • Tafadhali hakikisha makala yako imejikita kwenye uzoefu binafsi na kile ulichojifunza kutokana na uzoefu huo.“Hotuba” huenda zisichapishwe.

  • Tuma barua pepe ya wasilisho lako kwenda africacentral-communication@ChurchofJesusChrist.org

  • Tafadhali jumuisha jina lako kamili, kata, kigingi na namba ya simu juu ya hati.

Tafafadhali kumbuka:

  • Hadithi yako itahaririwa.Tafadhali jiandae kufanya kazi na wahariri wetu.

  • Inaweza kuchukua miezi kadhaa kupokea jibu kutoka kwa timu yetu.

  • Si mawasilisho yote yatachapishwa.