2021
Mungu miongoni Mwetu
Mei 2021


“Mungu miongoni Mwetu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Mungu Miongoni Mwetu

Dondoo

Picha
Yesu Kristo

Tunapohisi kutokuwa muhimu, kutelekezwa, na kusahauliwa, tunajifunza kwamba tunaweza kuhakikishiwa kuwa Mungu hajatusahau—ni kweli, kwamba Yeye hutoa kwa watoto Wake wote kitu kisichofikirika: cha kuwa “warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo” [Warumi 8:17]. …

Kwa sababu ya Yesu Kristo, makosa yetu hayapaswi kututambulisha. Yanaweza kutusafisha. …

Kama tutatubu, makosa hayatufanyi tusistahili. Ni sehemu ya maendeleo yetu. …

Kila mara nimejiuliza, Je, ni kitu gani ambacho Yesu angefundisha na kufanya kama Yeye angekuwa miongoni mwetu leo? …

Mwokozi daima anafundisha ukweli wa milele. Unatumika kwa watu wa kila umri na hali yoyote.

Ujumbe wake ulikuwa ni ujumbe wa matumaini na wa kuwa sehemu ya—ushuhuda kwamba Mungu Baba yetu wa Mbinguni hajawatelekeza watoto Wake.

Kwamba Mungu yu Miongoni Mwetu! …

Tunapotafuta kumfuata Yesu Kristo na kutembea njia ya ufuasi, mstari juu ya mstari, siku itafika ambapo tutafurahia ile zawadi isiyofikirika ya kupokea utimilifu wa shangwe. …

Ninatoa kwenu upendo wangu na baraka katika msimu huu wa Pasaka ya furaha. Fungueni mioyo yenu kwa Mwokozi na Mkombozi wetu, bila kujali hali zenu, majaribu, mateso, au makosa; mnaweza kujua kwamba Yeye yu hai, kwamba Yeye anawapenda, na kwamba kwa sababu Yake, ninyi kamwe hamtakuwa wapweke.

Mungu yu Miongoni Mwetu.