2020
Onyesha na Sema
Oktoba 2020


Onyesha na Sema

Mkutano mkuu upo mwezi huu! Hapa ni kile baadhi ya watoto hufurahia kuhusu mkutano.

Picha
Show and Tell

Shelem, Josué, Mía, na Ruth C., umri wa miezi 5, 8, 6, na miaka 3, Durango, Mexico, walifurahi kuangalia mkutano mkuu nyumbani. Ulikuwa ni mkutano maalum!

Annelle, Ruth, Sarah, na Samira K., miaka 8, 2, 6, na 6, Littoral, Benin, walipenda kuangalia mkutano pamoja kama familia.

Nilipoangalia mkutano mkuu, nilijifunza kuhusu jinsi Joseph Smith alivyotafsiri Kitabu cha Mormoni ili tuweze kuwa na neno la Mungu. Kitabu cha Mormoni kinanifundisha kuhusu Yesu Kristo.

Shalom A., miaka 6, Mkoa wa Dakar, Senegali

Ninapenda muziki wa Kwaya ya Tabernacle. Daima najisikia amani.

Jared B., miaka 7, Normandy, Ufaransa

Gabriel F., miaka 10, Minas Gerais, Brazili

Isabella B., miaka 5, Guatemala, Guatemala

Ilse N., miaka 5, Nuevo León, Mexico