2018
Mwombee Kila Dada kwa Jina
March 2018


Kanuni za Ualimu wa Kutembelea, Machi 2018

Omba kwa ajili ya Kila Dada kwa kutaja Jina

Upendo wetu na mwongozo wa kiungu juu ya wale tunaowafundisha kwa kuwatembelea utaongezeka tuoombapo kwa unyenyekevu kwa ajili ya kila dada hasa kwa kumtaja jina.

Imani, Familia, Usaidizi

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Wa Kina Mama

Maandiko huelezea mifano mingi ya wanaume na wanawake waliowaombea wengine kwa majina. Miongoni mwa mfano wa kuvutia ni baba wa Alma Mdogo. Malaika alizungumza na Alma Mdogo, akimwambia kuwa baba yake “a[li]kuwa ameomba kwa imani kubwa kukuhusu … ; kwa hivyo, ni kwa sababu hii nimekuja kukusadikisha kuhusu uwezo na mamlaka ya Mungu, kwamba sala za watumishi wake zijibiwe kulingana na imani yao” (Mosia 27:14).

Kuombeana hufungua mioyo yetu ili kupokea baraka ambazo Bwana anatamani kutupa. Madhumuni ya maombi si kubadilisha mapenzi ya Mungu, bali ni kujipatia kwa ajili yetu sisi wenyewe na wengine baraka ambazo Mungu tayari anataka kutupa, lakini ni lazima tuziombe ili tuweze kuzipata”.1

Dada mmoja alisimulia kwamba wakati wa kipindi kigumu katika maisha yake, muito wa simu au ujumbe mfupi rahisi daima ulikuja kutoka kwa walimu wake wakumtembelea katika “siku hasa za giza.” Walionekana kujua hasa wakati alihitaji kuinuliwa. Alijua kwamba waliomba kwa ajili yake, wakati wote walipomtembelea na wakiwa peke yao.

“Fikiria kuhusu nguvu yetu ya pamoja ikiwa kila mwana dada angekuwa na maombi ya dhati kila asubuhi na usiku au, vyema zaidi, kuomba bila kukoma kama vile ambavyo Bwana ameamuru,” alisema Julie B. Beck, Rais Mkuu aliyepita wa Muungano wa Usaidizi wa Wa Kina Mama.2 Kuwaombea wale tunaowafundisha kwa kuwatembelea hutuimarisha sisi binafsi na kama wanawake wa Siku za Mwisho.

Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, alisema: “omba kwa ajili ya njia ya kupata kujua mioyo yao. … Utahitajika kujua ni kitu gani Mungu angetaka ufanye ili kuwasaidia wao na kufanya yote kwa uwezo wako wote, kuujua upendo wa Mungu kwa ajili yao.”3

Muhtasari

  1. Mwongozo wa Maandiko, “Maombi”

  2. Julie B. Beck, “Je ni nini Wanawake wa Siku za Mwisho wanafanya vyema zaidi: Simama Imara na Usiyumbishwe,” Liahona, Nov. 2007, 110.

  3. Henry B. Eyring, “Ukuhani na Maombi Binafsi,” Liahona, Mei 2015, 85.