2015
Kutumia sala
Septemba 2015


VijanaK

utumia sala

Rais Eyring anafundisha kuwa familia yako inaweza kubarikiwa kwa uhusiano wako wenye nguvu na Baba wa Mbinguni. Unaweza kuboresha uhusiano wako Naye kwa kuboresha sala yako! Hapa kuna mawazo machache ya jinsi ya kufanya hivyo:

Kabla ya kuanza sala, chukua muda kidogo kufikiria kuhusu kile unachotaka kusema. Fikiria maswali unayoweza kuwa nayo au vitu ambavyo vimekuwa vikikusumbua —unaweza hata kuviandika ili usisahau. Tumia muda huu kuweka wazi akili yako kutokana na kelele za siku ili uweze kuzingatia mwongozo mtulivu wa Roho Mtakatifu. Ikiwa akili yako ina hali ya kutangatanga unaposali, jaribu kuvuta taswira ya Baba wa Mbinguni akisikiliza. Zungumza wazi. Pia acha dakika chache mwishoni ili kusikiliza mwongozo wa Roho Mtakatifu. Unaweza kuandika hisia zako kwenye shajara yako.

Kumbuka kwamba sala ni aina ya kazi, usiwe na wasi wasi ikiwa inahitaji mazoezi au ikionekana kuwa ngumu! Juhudi zako katika sala zinaweza kusaidia kujenga uhusiano na Mungu utakaobariki vizazi.