2012
Ualimu tembelezi, Kazi ya Wokovu
Desemba 2012


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Disemba 2012

Ualimu Tembelezi, Kazi ya wokovu

Soma kifaa hiki kwa maombi na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Picha
Alama ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani • Familia • Usaidizi

Ualimu tembelezi huwapa wanawake nafasi ya kutunza, kuimarisha na kufundishana—kwa kweli ni kazi ya wokovu. Kupitia kwa ualimu tembelezi, akina dada wanahudumu kwa niaba ya Mwokozi na kusaidia kuwatayarisha wanawake kwa baraka za uzima wa milele.

“Sisi ni wa ‘kuwaonya, kuelezea, kushawishi, na kufundisha, na kuwakaribisha [wengine] kuja kwa Kristo’ (D&C 20:59), vile Bwana alivyosema katika funuo zake,” alisema Rais Spencer W. Kimball (1895–1985). Zaidi, alisema, “Ushuhuda wako ni chombo cha ajabu.”1

Wakati sisi kama walimu watembelezi tunapoongeza ufahamu wetu wa kweli za injili, shuhuda zetu zinaimarisha na kuwasaidia akina dada wanaojitayarisha kubatizwa na kuthibitishwa. Tunawasaidia washiriki wapya kuwa imara katika injili. Matembelezi yetu na upendo utasaidia “kuwarudisha wale ambao wamepotoka [na] kutia joto mioyo ya wale wamekuwa baridi katika injili.”2 Na tunawahimiza akina dada kuja kwa Kristo kupitia mahudhurio ya hekalu.

“Mutaokoa nafsi,” alisema Rais Kimball kwa walimu watembelezi, “na nani anajua isipokuwa wale watu wema wanaoshiriki kikamilifu Kanisani hivi leo, wanashiriki kikamilifu kwa sababu mlikuwa nyumbani mwao na kuwapa mtazamo mpya, ono jipya. Mlivuta nyuma pazia. Mlipanua upeo wao. …

“Mnaona, hamuokoi tu akina dada hawa, lakini pengine pia waume wao na nyumba zao.”3

Kutoka kwa Maandiko

Mafundisho na Maagano 20:59; 84:106; 138:56

Kutoka kwa Historia Yetu

Wakati Nabii Joseph Smith alipounda Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alisema kuwa wanawake hawakuwa tu wa kuwalinda walio maskini bali pia kuokoa nafsi. Alifundisha kuwa wanawake Kanisani wana jukumu muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni wa wokovu.4 Tukiongozwa na kanuni zilizofundishwa na Nabii Joseph Smith, sisi kama akina dada katika Muungano wa Usaidizi wa kina Mama tunaweza kufanya kazi pamoja kuwatayarisha wanawake na familia zao kwa baraka kuu zaidi za Mungu

“Na tuwe na huruma sisi kwa sisi,” alisema Rais Brigham Young (1801–77), “na hebu [wale walio] na nguvu kuwatunza kwa wororo walio wadhaifu hadi kwa nguvu, na hebu wale wanaoweza kuona kuongoza walio vipofu hadi watakapoweza kuona njia wenyewe.”5

Muhtasari

  1. Spencer W. Kimball, Katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 116.

  2. Eliza R. Snow, katika Daughters in My Kingdom, 83.

  3. Spencer W. Kimball, katika Daughters in My Kingdom, 117.

  4. Ona Joseph Smith, katika Daughters in My Kingdom, 171–72.

  5. Brigham Young, Katika Daughters in My Kingdom, 107.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama unanitayarisha vipi kwa baraka za uzima wa milele?

  2. Nitafanya nini ili kuongeza imani ya wale ninaowalinda?