2012
Mimi Nitamwona Yeye Tena
Aprili 2012


Vijana

Mimi Nitamwona Yeye Tena

Baba alitufanya kila mmoja wetu sisi watoto kuhisi maalum. Alitupenda na angetusamehe kwa urahisi. Alifanya aliyoweza kuhakikisha kuwa kila mmoja wetu alikuwa na furaha na aliweka wazi kuwa alitaka yaliyo bora kwetu. Nilimpenda sana.

Nilipokuwa katika darasa la sita, babangu alikufa katika ajali ya gari, Familia yangu nami tulidhikishwa. Kuna pengo kubwa katika familia yetu. Baba alikuwa ndiye niliyemtegemea, niliyemwendea nilipokuwa na shida. Badala ya kutafuta usaidizi, niliacha hasira na uchungu kukaa. Mwishowe nikaamua ilikuwa makosa ya Mungu. Niliacha kusoma maandiko na kuomba. Nilienda Kanisani tu kwa sababu mama alinitaka niende. Nilijaribu kukaa mbali na Baba yangu wa Mbinguni.

Kisha nikaenda katika kambi ya Wasichana kwa mara ya kwanza. Nilifurahia kukutana na marafiki wapya lakini bado sikusoma maandiko yangu. Katika usiku wa mwisho, tulikuwa na mkutano wa ushuhuda. Nilihisi kitu ambacho sikuwa nimehisi kwa muda mrefu. Niliwastahi wasichana walioamka na kutoa shuhuda zao, lakini nilibaki nimeketi kwa sababu nilifikiri sikuwa na ushuhuda. Ghafla, nilihisi kuwa ilinibidi kusimama. Nilifungua mdomo wangu, nikishindwa na la kusema. Nilisema nilifurahia Kambi ya Wasichana. Kisha nikajipata nikisema kuwa nilijua Yesu Kristo alikufa kwa ajili yangu, na kwamba Baba yangu wa Mbinguni alinipenda na kuwa Kanisa ni la kweli.

Nilijawa na amani ya ajabu kwa ajili ya uzoefu huu, ninaweza kusema kuwa ninajua nitamwona baba yangu tena kwa sababu ya Upatanisho na Ufufuo wa Mwokozi.