2011
Fedha za Kutosha
Juni 2011


Vijana

Fedha za Kutosha

Nilikutana na wamisionari wakati nilipokuwa umri wa miaka 17. Wakati huo kaka yangu mkubwa na nami tulikuwa tunaishi pamoja. Mama yetu alikuwa ameaga dunia mwaka uliokuwa umepita, na maisha yalikuwa magumu. Wamisionari waliponifunza, Niliona kwamba Kanisa hili ndio lile niliokuwa nikitafuta kila mara. Lakini ushawishi wa marafiki zangu ulinizuia mimi kutokwenda kanisani Jumapili.

Siku moja nilienda shughuli za Kanisani katikati ya wiki. Kuona vijana wote wakicheka na kucheza kuliniletea mimi shangwe kuu. Wamisionari, pamoja na vijana, walichukua nafasi hio kunifunza somo la kwanza la injli, na kuhisi vyema niliamua kubatizwa.

Lakini hata baada ya kujiunga na Kanisa, nilikumbana na changamoto. Nilikuwa mshiriki wa pekee wa Kanisa katika sehemu hio ya mji na niliishi mbali sana na jumba la mkutano. Marafiki zangu hawakutaka tena kuhusishwa nami. Nilipohisi kuwa mpweke, niliomba na kuhisi upendo wa Bwana.

Kila mwezi, nilipokea kiasi kidogo cha mgawo wa fedha kutoka kwa hazina iloachwa na mama yangu. Ilikuwa ni vigumu kujikimu kimaisha na fedha ndogo namna hiyo. Lakini nilijitahidi kuwa mtiifu. Nilitoa fungu la kumi na pia nilikuwa nijilipie usafiri kwenda mkutano wa seminari na Jumapili. Sikuelewa vipi, lakini mwisho wa mwezi, nilipata kumekuwa na fedha za kutosha za kufanya hayo yote.

Najua kwamba nimebarikiwa kwa sababu ya kutoa fungu la kumi. Kutii amri hii kulinisaidia mimi kupata ushuhuda imara, kuhudumu misheni, na kutambua baraka ili niwaimarishe washiriki wapya ambao wanaokumbana na changamoto.