Mungu Ni Chanzo cha Ukweli Wote
Tunaweza kumtegemea Mungu; Mwanawe, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu kwa ajili ya ukweli.
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu: yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Yesu ni mfano wetu mkamilifu wa jinsi ya kuishi. Mafundisho Yake hutumika kama nuru elekezi ambayo inaweza kutuelekeza kwenye amani. Mtu yeyote anayetaka kumfuata Yesu Kristo anaweza kuwa na nuru hii; Yeye anaahidi kwamba wote wanao mtafuta watampata.
Roho Mtakatifu Hutusaidia
Roho Mtakatifu, ni mjumbe wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kuna njia kadhaa ambazo kwazo Roho Mtakatifu anaweza kusaidia kutuleta karibu zaidi na Mungu. Roho Mtakatifu:
- Hufariji (ona
Yohana 14:16–17, 26 ;Moroni 8:26 ;Mafundisho na Maagano 36:2 ). - Hufunua na kushuhudia juu ya ukweli (ona
2 Nefi 32:4–5 ;Alma 5:46–47 ;Mafundisho na Maagano 8:2–3 ). - Hushuhudia juu ya Baba na Mwana (ona
Yohana 15:26 ;3 Nefi 11:32, 36 ). - Hutakasa na kusafisha (ona
Alma 13:10–12 ;3 Nefi 27:19–20 ;Moroni 6:4 ).
Je, Ninawezaje Kujua Kile Kilicho cha Kweli?
Sali kwa Baba yako wa Mbinguni
Mungu anatupenda na anataka kusikia kutoka kwetu. Yeye anaahidi kwamba tunaposali, Yeye atatupatia majibu na mwongozo.Yesu alitufundisha jinsi ya kusali katika Biblia (
Kuwa mwaminifu
Biblia inafundisha kwamba “imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” (Kumtambua Roho Mtakatifu
Mungu anawasiliana nasi kupitia Roho Mtakatifu katika njia tofauti. Katika Biblia, mara nyingi inaelezewa kama “sauti ndogo tulivu” (ona- Hisia za upendo, shangwe, amani, na wema (
Wagalatia 5:22-23 ). - Uwazi na mwongozo kwa ajili ya maisha yako (
Mafundisho na Maagano 8:2–3 ). - Mawazo akilini mwako na hisia katika moyo wako (
1 Wakorintho 2:9–11 ). - Giza likibadilishwa kuwa nuru (
Alma 19:6 ).
Fuata mfano wa Mwokozi
Yesu alionesha mfano mkuu kwetu sote. Kama tunataka kujua kile kilicho cha kweli, tunaweza kufuata mfano Wake na kufanya kile Yeye alichofanya.Hii inafananaje?
- Onesha upendo na hisani kwa wengine na kwa Mungu.
- Chunguza jinsi matendo hayo yanavyokufanya uhisi.
- Tafakari jinsi matendo hayo yanavyobadilisha maisha yako.
Je, Una Maswali Zaidi?
Waumini wa Kanisa letu ambao wanajitolea muda wao kama wamisionari wanaweza kuzungumza nawe mtandaoni au ana kwa ana ili kushiriki ujumbe wa kuvutia na kujibu maswali yako binafsi zaidi.