VW Kila Wiki
Karibu kwenye VW Kila Wiki
Karibu kwenye VW Kila Wiki


Karibu kwenye VW Kila Wiki

Picha
Vijana wakubwa wakiruka

Karibu kwenye VW Kila Wiki——chapisho la kila wiki hapa katika programu yako ya Maktaba ya Injili kwa ajili ya vijana wakubwa ikitolewa na vijana wakubwa, pamoja na viongozi wa Kanisa na wataalamu wengine kwenye mada zilizo muhimu kwetu sisi leo.

Lengo Letu

Lengo letu ni kukusaidia kupata majibu ya changamoto zako na nguvu ya kuzikabili. Tutafanya hivi kwa kupitia injili ya Yesu Kristo kwa pamoja na kuchunguza jinsi vijana wakubwa ulimwenguni kote wanavyojitahidi kuiishi.

Kuhusu Sisi

Kitu cha kwanza: sehemu hii nzima ilitokana nawe. Tunakabiliwa na chaguzi, changamoto mpya na mabadiliko mengi wakati wa kipindi hiki cha maisha yetu. Na tunataka kukuongoza kupita yote hayo. Pia tunataka ujue kuwa tunakuona jinsi ulivyo badala ya hali yako ya ndoa, ndiyo maana sehemu hii haiitwi Vijana Waseja (VWS) Kila Wiki. Maudhui haya yanatengenezwa kwa ajili ya vijana wote wakubwa, waseja au walio kwenye ndoa au walio waseja tena, kwa sababu athari yenu Kanisani—na ulimwenguni—haipimiki, bila kujali hatua ya ujana wenu mliopo kwa sasa.

Pia tunafikiria kwamba mada tunazoshughulikia zitakuwa na mvuto kwa vijana wote wakubwa, hata kwa wale walio na zaidi ya miaka 30. Tunajua matamanio yenu katika mada na changamoto ambazo tutakuwa tunazizungumzia hazitabadilika kwa sababu tu mlikuwa na tarehe nyingine ya kuzaliwa. Mambo tunayokumbana nayo leo ni ya muhimu kwetu sote na la muhimu mno ni kwetu sote kuyashughulikia kwa pamoja, bila kujali umri wetu.

Tunatambua kwamba nyinyi nyote mnatoka katika sehemu tofauti za maisha, kielimu, kiuchumi, kiutamaduni na kihali. Kwa hivyo tutapitia mada tofauti tofauti, na hadithi zetu nyingi zitakuwa zikipatikana katika lugha zaidi ya 20 katika Maktaba ya Injili—tunataka kuwafikieni nyote na kuonyesha umuhimu kwenu nyote. Vijana wakubwa kutoka ulimwenguni kote wanaleta imani na vipaji vyao Kanisani. Katika sehemu nyingi, sisi si tu viongozi wa kesho, tunaongoza Kanisa leo, ikijumuisha maeneo ambapo Kanisa limeanzishwa kwa muda mrefu. Na athari yetu itaongezeka hata zaidi ya leo, kwa sababu sisi pia ni wazazi wa kizazi kijacho.

Tungeweza Kuendelea

Kuna mengi sana tungeweza kusema kuhusu thamani na umuhimu wa vijana wakubwa, lakini kama tutaendelea, itaonekana kama tunajisifu (kwa sababu kizazi chetu ni kizuri) Inatosha kusema, Mungu anatuhitaji, tunamuhitaji Mungu na Kanisa Lake na pia tunamhitaji kila mmoja wetu. Kwa pamoja, “tutaweka historia,” kama Rais Russell M. Nelson alivyosema kuhusu vijana wakubwa. “Atawawezesha kutimiza yasiyowezakana kutimizwa. …

“… Ninyi ‘ni kizazi kiteule’ (1 Petro 2:9), kilichotawazwa tangu awali na Mungu kufanya kazi ya maajabu—kusaidia kuwandaa watu wa ulimwengu huu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana!”1

Licha ya mabadiliko ya sasa na mambo yajayo yasiyojulikana, ujana unaweza kuwa wakati mzuri wa kujigundua na kukua, kupata lengo hapa duniani na kujifunza jinsi ya kuiweka injili kama kitovu cha maisha yetu. Tuna shauku ya kuwa kwenye safari hii pamoja nanyi na tunatumaini kwamba mtakuwa wageni wa kila mara!

Wapi pa Kutupata

VW Kila Wiki iko katika Maktaba ya Injili chini ya Magazeti au Watu Wazima> Vijana Wakubwa. Pia utapata kuona baadhi ya hadithi zetu katika gazeti la Liahona, ukurasa wa Facebook wa Liahona na kwenye ukurasa wa nyumbani wa ChurchofJesusChrist.org.

Tunataka Kusikia kutoka Kwako

  • Mada zipi ungependa tuziongelee?

  • Una hadithi zipi unazotaka kushiriki?

  • Mapendekezo gani unayo kwetu?

Unaweza kuwasilisha hadithi, mawazo na maoni yako mwenyewe kwenye liahona.ChurchofJesusChrist.org. Tunasuburi kwa shauku kusikia kutoka kwako!

Kumbuka

  1. Russell M. Nelson, “Simameni Kama Wamelenia Halisi,” Liahona, Oct. 2016, 50, 53.