Maagizo na Matangazo
Familia: Tangazo kwa Ulimwengu


Familia

Tangazo kwa Ulimwengu

Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili wa Kanisa La Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Sisi, Urais wa Kwanza na Baraza la Mitume Kumi na Wawili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunatangaza kwa heshima kwamba ndoa kati ya mwanaume na mwanamke imetakaswa na Mungu, na kwamba familia ni ya muhimu katika mpango wa Muumba kwa maisha ya milele ya watoto Wake.

Wanadamu wote—wanaume na wanawake—wameumbwa katika mfano wa Mungu. Kila moja ni mwana au binti mpendwa wa kiroho wa wazazi wa mbinguni, na, kama hivyo, kila moja ana asili takatifu na takdiri Jinsia ni hulka muhimu ya utambuzi wa milele wa maisha kabla ya maisha ya dunia, na maisha ya dunia ya mtu na utambulisho na dhamira.

Katika ufalme kabla ya maisha ya dunia, wana na mabinti wa kiroho walijua na kumwabudu Mungu kama Baba yao wa Milele na kukubali mpango Wake ambao ungewezesha watoto Wake kupokea mwili na kupata uzoefu wa dunia ili kukua kwa ukamilifu na hatimaye kutambua maisha yao matakatifu kama warithi wa maisha ya milele. Mpango mtakatifu wa furaha unawezesha uhusiano wa familia kuendelezwa zaidi ya kaburi. Maagizo na maagano matakatifu yanayopatikana katika mahekalu matakatifu yanawezesha watu binafsi kurudi katika uwepo wa Mungu na kwa familia kuunganishwa milele.

Amri ya kwanza ambayo Mungu aliwapa Adamu na Hawa ilihusiana na uwezo wao wa uzazi kama mume na mke. Tunatangaza kwamba amri ya Mungu kwa watoto Wake ya kuzaana na kujaza dunia imebaki ikizingatiwa. Tunatangaza tena kwamba Mungu ameamuru kwamba nguvu takatifu za kuzaa ni lazima zitumike tu, kati ya mwanamume na mwanamke, ambao wameoana kihalali kama mme na mke.

Tunatangaza njia ambayo maisha ya dunia yanaumbwa imechaguliwa kitakatifu. Tunathibitisha utakatifu wa uhai na umuhimu wake katika mpango wa milele wa Mungu.

Mume na mke wana jukumu muhimu la kupenda na kutunza kila mmoja na mwingine na watoto wao. “Watoto ni urithi wa Bwana” (Zaburi 127:3). Wazazi wanajukumu takatifu la kulea watoto wao katika upendo na utakatifu, kukimu mahitaji yao ya kimwili na kiroho, na kuwafundisha kupenda na kutumikiana mmoja na mwingine, kutii amri za Mungu, na kuwa wananchi wenye kutii sheria popote wanapoishi. Waume na wake— akina mama na kina baba—watapasishwa mbele ya Mungu kwa utimizaji wa majukumu haya.

Familia imetakaswa na Mungu. Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa mpango Wake wa milele. Watoto wana haki ya kuzaliwa ndani ya mikataba ya ndoa, na kulewa na baba na mama wanaoheshimu viapo vya ndoa kwa uaminifu kamili. Furaha katika maisha ya familia itapatikana kwa urahisi ikiwa imejegwa katika mafundisho ya Bwana Yesu Kristo. Ndoa na familia zenye ufanisi zimejengwa na kukuzwa katika misingi ya imani, maombi, toba, msamaha, heshima, upendo, huruma, kazi, na matendo mazuri ya maburudisho. Kwa mpango mtakatifu, akina baba wanapaswa kusimamia familia zao katika upendo na utakatifu na wana jukumu la kukimu mahitaji ya maisha na ulinzi kwa familia zao. Akina mama wana jukumu la kimsingi kwa utunzaji wa watoto wao. Katika majukumu haya matakatifu, akina baba na mama wana wajibu wa kusaidiana mmoja kwa mwingine kama washiriki sawa. Ulemavu, kifo, au hali zingine zinaweza kulazimisha utohozi wa kibinafsi Ukoo unapaswa kutoa usaidizi unapohitajika.

Tunaonya kwamba watu wanaovunja maagano ya usafi , wanaodhulumu wenzi au uzao, au wanaokosa kutimiza majukumu ya familia siku moja wataweza kusimama kupasishwa mbele ya Mungu. Zaidi, tunaonya kwamba kusambaratika kwa familia kutaletea watu binafsi, jamii na mataifa majanga yaliyotabiriwa na manabii wa zamani na wa kisasa.

Tunawasihi wananchi wote waliowajibika na maafisa wa serikali kila mahali kuendeleza kanuni ambazo zimedhamiriwa kustawisha na kuimarisha familia kama sehemu muhimu ya jamii.