Maandiko
Musa 1
iliyopita inayofuata

Teuzi kutoka
Kitabu cha Musa

Kiziduo kutoka tafsiri ya Biblia kama kilivyofunuliwa kwa Joseph Smith Nabii, Juni 1830–Februari 1831.

Mlango wa 1

(Juni 1830)

Mungu Anajionyesha mwenyewe kwa Musa—Musa anageuzwa sura—Anakabiliana ana kwa ana na Shetani—Musa anaona dunia nyingi zenye kukaliwa na watu—Dunia zisizo na idadi ziliumbwa na Mwana—Kazi na utukufu wa Mungu ni kuleta maisha katika mwili usio kufa na uzima wa milele wa mwanadamu.

1 Maneno ya Mungu, ambayo aaliyaongea kwa bMusa wakati Musa alipokuwa amenyakuliwa juu katika Mlima mrefu sana,

2 Naye aakamwona Mungu buso kwa uso, na akaongea naye, na cutukufu wa Mungu ukawa juu ya Musa; kwa hiyo Musa aliweza dkustahimili uwepo wake.

3 Na Mungu akamwambia Musa, akisema: Tazama, Mimi ndimi Bwana Mungu aMwenyezi, na bBila Mwisho ndilo jina langu; kwa maana Mimi sina mwanzo wa siku wala mwisho wa miaka; je, na hii siyo bila mwisho?

4 Na, tazama, wewe u mwanangu; kwa sababu hiyo aangalia, nami nitakuonyesha wewe kazi za bmikono yangu; lakini siyo zote, kwa maana ckazi zangu hazina dmwisho, na pia emaneno yangu, kwa maana hayakomi.

5 Kwa sababu hiyo, hakuna mwanadamu awezaye kuziona kazi zangu zote, isipokuwa ameuona utukufu wangu wote; na hakuna mtu awezaye kuuona utukufu wangu wote, na baadaye akabaki katika mwili duniani;

6 Na ninayo kazi kwa ajili yako, Musa, mwanangu; nawe u amfano wa Mwanangu wa bPekee; na Mwanangu wa Pekee ni Mwokozi, na atakuwa cMwokozi, kwa maana yeye amejaa dneema na ekweli; lakini fhakuna Mungu zaidi yangu, na vitu vyote viko mbele zangu, kwani gninavijua vyote.

7 Na sasa, tazama, jambo hili moja ninalionyesha kwako, Musa, mwanangu, kwa maana wewe uko ulimwenguni, na sasa ninalionyesha kwako.

8 Na ikawa kwamba Musa akaangalia, na akauona aulimwengu ambao juu yake aliumbwa; na Musa bakauona ulimwengu na miisho yake, na wanadamu wote waliopo, na ambao waliumbwa; alishangaa na ckustajaabu mno juu ya hayo.

9 Na uwepo wa Mungu ukatoweka mbele ya Musa, na kwamba utukufu wake haukuwa juu ya Musa; na Musa akaachwa pekee yake. Na vile alivyoachwa pekee yake, akaanguka chini.

10 Na ikawa kwamba masaa mengi yalipita kabla ya Musa kurudiwa tena na anguvu zake za kiasili kama mwanadamu; naye alijisemea: Sasa, kwa jinsi hii ninajua kwamba mwanadamu bsi kitu, kitu ambacho sikukidhania.

11 Lakini sasa macho yangu yenyewe yamemwona aMungu; lakini siyo kwa macho yangu ya basili, bali kwa macho yangu ya kiroho, kwa maana macho yangu ya asili hayangeweza kumwona; kwani cningelinyauka na dkufa mbele zake; lakini utukufu wake ulikuwa juu yangu; nami nikauona euso wake, kwa kuwa fnilibadilishwa mbele zake.

12 Na ikawa kwamba wakati Musa aliposema maneno haya, tazama, aShetani akaja bkumjaribu, akisema: Musa, mwana wa mtu, niabudu mimi.

13 Na ikawa kwamba Musa akamtazama Shetani na akasema: Wewe ni nani? Kwa maana tazama, mimi ni amwana wa Mungu, katika mfano wa Mwanawe wa Pekee; na u wapi utukufu wako, hata nipate kukuabudu?

14 Kwani tazama, sikuweza kumwangalia Mungu, isipokuwa utukufu wake ulipokuwa juu yangu, nami anikabadilishwa mbele zake. Lakini ninaweza kukuangalia wewe katika hali ya kiasili ya mwanadamu. Je, hakika si ndivyo ilivyo?

15 Na libarikiwe jina la Mungu wangu, kwa maana Roho wake hajajiondoa kwangu moja kwa moja, au vinginevyo utukufu wako u wapi, kwa maana ni giza kwangu? Nami ninaweza kuwatofautisha kati yako wewe na Mungu; kwa maana Mungu aliniambia: aMwabudu Mungu, kwa maana ni yeye pekee butakayemtumikia.

16 Nenda zako, Shetani; usinidanganye; kwa maana Mungu aliniambia: Wewe ni amfano wa Mwanangu wa Pekee.

17 Naye pia alinipa amri wakati aliponiita kutoka akichaka kilichokuwa kinaungua, akisema: bMlingane Mungu katika jina la Mwanangu wa Pekee, na kuniabudu Mimi.

18 Na tena Musa akasema: Sitaacha kumlingia Mungu, ninayo mambo mengine ya kumwuliza: kwa maana utukufu wake ulikuwa juu yangu, kwa sababu hiyo ninaweza kuwatofautisha kati yake yeye na wewe. Ondoka hapa, Shetani.

19 Na sasa, Musa alipokwisha kusema maneno haya, Shetani akalia kwa sauti kubwa, na kujitapa juu ya nchi, na kuamuru, akisema: Mimi ndiye aMwana wa Pekee, niabudu mimi.

20 Na ikawa kwamba Musa akaanza kuogopa kupita kiasi; na mara alipoanza kuogopa, akaona machungu ya ajehanamu. Hata hivyo, bakamlingana Mungu, naye akapokea nguvu, naye akaamuru, akisema: Ondoka kwangu, Shetani, kwa maana ni Mungu huyu mmoja tu nitakayemwabudu, ambaye ndiye Mungu wa utukufu.

21 Na sasa aShetani akaanza kutetemeka, na nchi kutingishika; na Musa akapata nguvu, na kulilingania jina la Mungu, akisema: Katika jina la Mwana wa Pekee, ondoka, Shetani.

22 Na ikawa kwamba Shetani akalia kwa sauti kubwa, kwa kuomboleza, na huzuni, na akusaga meno; na akaondoka mahali hapo, hata kutoka uwepo wa Musa, kwamba hakumwona.

23 Na sasa juu ya jambo hili Musa analishuhudia; lakini kwa sababu ya uovu halijakuwepo miongoni mwa wanadamu.

24 Na ikawa kwamba Shetani alipokuwa ameondoka katika uwepo wa Musa, kwamba Musa aliinua macho yake mbinguni, akiwa amejaa aRoho Mtakatifu, ambaye huwashuhudia Baba na Mwana;

25 Na akalilingania jina la Mungu, akauona utukufu wake tena, kwa maana ulikuwa juu yake; na akasikia sauti, ikisema: Heri wewe, Musa, kwa maana Mimi, Mwenyezi, nimekuchagua wewe, nawe utafanywa kuwa mwenye nguvu kushinda amaji mengi; kwa maana yatatii bamri yako kama vile, wewe ndiye cMungu.

26 Na lo, Mimi nipo pamoja nawe, hata mwisho wa siku zako; kwa maana wewe autawakomboa watu wangu kutoka butumwani, hata cIsraeli dmteule wangu.

27 Na ikawa kwamba, wakati sauti ikiwa bado inaongea, Musa alitupa macho yake na aakaiona dunia, ndiyo, hata dunia yote; na hakuna sehemu yake yoyote ambayo hakuiona, akiitambua kwa uwezo wa Roho wa Mungu.

28 Naye pia aliwaona wakazi wake, na hapakuwa na nafasi ambayo hakuiona; na alizitambua kwa uwezo wa Roho wa Mungu; na idadi yao ilikuwa kubwa, hata isiyohesabika kama vile mchanga juu ya pwani ya bahari.

29 Naye aliona nchi nyingi; na kila nchi iliitwa adunia, nako kulikuwapo na wakazi juu ya uso wake.

30 Na ikawa kwamba Musa akamlingana Mungu, akisema: Niambie, nakuomba, kwa nini mambo haya yako hivi, na kwa njia gani wewe uliyatengeneza?

31 Na tazama, utukufu wa Bwana ulikuwa juu ya Musa, na hivyo Musa alisimama katika uwepo wa Mungu, na kuzungumza naye auso kwa uso. Na Bwana Mungu akamwambia Musa: Kwa bmadhumuni yangu Mimi mwenyewe nimeyatengeneza mambo haya. Hii ndiyo hekima nayo yabaki kwangu.

32 Na kwa aneno la uwezo wangu, nimeviumba, ambaye ndiye Mwanangu wa Pekee, aliyejaa bneema na ckweli.

33 Na adunia zisizo na idadi bnimeziumba; na pia nimeziumba kwa madhumuni yangu mwenyewe; na kwa njia ya Mwana nimeziumba, ambaye ndiye cMwanangu wa Pekee.

34 Na mwanadamu wa akwanza kwa wanadamu wote nikamwita bAdamu, ambalo ni cwengi.

35 Lakini ni maelezo ya dunia hii tu, na wakazi wake, ndiyo nikupayo. Kwa maana tazama, ziko dunia nyingi ambazo zimepita kwa neno la uwezo wangu. Na ziko nyingi ambazo sasa zinasimama, na kwa mwanadamu hazihesabiki; lakini vitu vyote vinahesabika kwangu, kwa kuwa ni vyangu nami anavijua.

36 Na ikawa kwamba Musa akamwambia Bwana, akisema: Umrehemu mtumishi wako, Ee Mungu, na uniambie juu ya dunia hii, na wakazi wake, na pia mbingu, na ndipo mtumishi wako ataridhika.

37 Na Bwana Mungu akasema kwa Musa, akisema: aMbingu hizi, ziko nyingi, nazo haziwezi kuhesabika kwa mwanadamu; lakini zinahesabika kwangu, kwa kuwa ni zangu.

38 Na kama vile dunia moja itakavyopita, na mbingu zake na hivyo nyingine zitakuja; na hakuna amwisho wa kazi zangu, wala wa maneno yangu.

39 Kwa maana tazama, hii ndiyo akazi yangu na butukufu wangu—kuleta ckutokufa na uzima wa dmilele wa mwanadamu.

40 Na sasa, Musa, mwanangu, nitakuambia juu ya dunia hii ambayo juu yake wewe umesimama; nawe autaandika mambo ambayo nitayasema.

41 Na katika siku ambayo wanadamu watakapoyachukulia maneno yangu kuwa kazi bure na akuyaondoa mengi kutoka kwenye kitabu ambacho utakiandika, tazama, nitamwinua mwingine bkama wewe; cnayo yatasikika tena miongoni mwa wanadamu—miongoni mwa wengi kadiri watakavyoamini.

42 (Maneno haya ayalinenwa kwa Musa mlimani, mlima ambao jina lake halitajulikana miongoni mwa wanadamu. Na sasa yananenwa kwako. Usiyaonyeshe kwa yeyote isipokuwa wao waaminio. Hivyo ndivyo. Amina.)