Maandiko Matakatifu
Ibrahimu 2


Mlango wa 2

Ibrahimu aondoka Uru kwenda Kanaani—Yehova amtokea huko Harani—Baraka zote za injili zimeahidiwa kwa uzao wake na kupitia uzao wake kwenda kwa wote—Anakwenda Kanaani na kuendelea hadi Misri.

1 Sasa Bwana Mungu akazidisha njaa kuwa kali sana katika nchi ya Uru, kiasi kwamba aHarani, kaka yangu, akafa; lakini bTera, baba yangu, bado aliishi katika nchi ya Uru, ya Wakaldayo.

2 Na ikawa kwamba mimi, Ibrahimu, nikamchukua aSarai kuwa mke wangu, na bNahori, kaka yangu, akamchukua Milka kuwa mke wake, aliyekuwa binti wa Harani.

3 Sasa Bwana alikuwa aameniambia: Ibrahimu, toka katika nchi yako, na kutoka kwa jamaa zako, na kutoka nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayokuonyesha.

4 Kwa hiyo nikaondoka nchi ya aUru, ya Wakaldayo, na kwenda katika nchi ya Kanaani; nami nikamchukua Loti, mwana wa kaka yangu, na mke wake, na Sarai mke wangu; na pia bbaba yangu akanifuata, kwenye nchi ambayo tuliita Harani.

5 Na njaa ikapungua; na baba yangu akakaa katika Harani na akaishi hapo, kwa vile palikuwa na mifugo mingi katika Harani; na baba yangu akageukia tena kwenye kuabudu asanamu zake, kwa hiyo akaendelea katika Harani.

6 Lakini mimi, Ibrahimu, na aLoti, mwana wa kaka yangu, tukamwomba Bwana, na Bwana bakanitokea, na akaniambia: Simama, na umchukue Loti pamoja nawe; kwa maana nimekusudia kuwatoa ninyi nje ya Harani, na kukufanya mhudumu wa kulichukua cjina langu katika dnchi ya kigeni nchi ambayo nitaitoa kwa uzao wako baada yako kuwa miliki isiyo na mwisho, wakiisikiliza sauti yangu.

7 Kwa maana Mimi ndimi Bwana Mungu wako; ninakaa mbinguni; dunia ni pa akuwekea miguu yangu; ninanyoosha mkono wangu juu ya bahari, nayo huitii sauti yangu; huufanya upepo na moto kuwa bgari langu; ninaiambia milima—Ondoka hapa—na tazama, inaondolewa kwa upepo wa tufani, katika kitambo kidogo, mara moja.

8 Jina langu ni aYehova, nami bninajua mwisho kutoka mwanzo; kwa hiyo mkono wangu utakuwa juu yako.

9 Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nami anitakubariki kupita kipimo, na kulifanya jina lako kuwa kubwa miongoni mwa mataifa yote, nawe utakuwa baraka kwa uzao wako baada yako, ili katika mikono yao wataichukua huduma hii na bUkuhani kwa mataifa yote;

10 Nami nitawabariki wao kupitia jina lako; kwani kadiri wengi watakavyoipokea aInjili hii wataitwa kwa jina lako, nao watahesabiwa kuwa buzao wako, na watainua na kukubariki, kama cbaba yao;

11 Nami nitawabariki wao wenye akukubariki wewe, na nitawalaani wao wenye kukulaani wewe; na katika wewe (yaani, katika Ukuhani wako) na katika buzao wako (yaani, Ukuhani wako), kwani ninakupa ahadi kwamba chaki hii itaendelea ndani yako, na katika uzao wako baada yako (ndiyo kusema, uzao wako halisi, au uzao wa mwili wako) familia zote za dunia zitabarikiwa, hata kwa baraka za Injili, ambazo ni baraka za wokovu, hata za uzima wa milele.

12 Sasa, baada ya Bwana alipojiondoa kutoka kusema nami, na kuondoa uso wake kwangu, nikasema moyoni mwangu: Mtumishi wako aamekutafuta kwa dhati; sasa nimekupata;

13 Wewe uliwatuma malaika zako ili akunikomboa kutoka kwa miungu wa Elkena, nami nitafanya vyema kuisikiliza sauti yako, kwa hiyo mwache mtumishi wako asimame na kuondoka kwa amani.

14 Hivyo mimi, Ibrahimu, nikaondoka kama Bwana alivyoniambia, na Loti pamoja nami; na mimi, Ibrahimu, nilikuwa na umri wa miaka asitini na miwili wakati nilipoondoka kutoka Harani.

15 Nami nikamchukua aSarai, ambaye nilimchukua kuwa mke wangu wakati nilipokuwa bUru, katika Ukaldayo, na Loti, mwana wa kaka yangu, na mali yetu yote tuliyoikusanya, na watu wale ctuliowapata Harani, na tukatoka katika njia ya kwenda nchi ya dKanaani, na kukaa katika mahema tulipokuwa tukisafiri;

16 Kwa hiyo, milele yalikuwa maficho yetu na amwamba wetu na wokovu wetu, tulipokuwa tukisafiri kutoka Harani kwa njia ya Jershoni, ili kuja nchi ya Kanaani.

17 Sasa mimi, Ibrahimu, nikajenga amadhabahu katika nchi ya Jershoni, nami nikamfanyia Bwana sadaka, na nikaomba kwamba bnjaa ipate kugeuzwa kutoka nyumba ya baba yangu, ili wasiangamie.

18 Na kisha tukapita kutoka Jershoni kupitia nchi ya mahali pa Sechemu; iliyokuwa katika nyanda za More, na tulikuwa tayari tumekuja katika mipaka ya nchi ya aWakanaani, nami nikatoa bdhabihu hapo katika nyanda za More, na nikamwitia Bwana kwa moyo mkuu, kwa sababu tulikuwa tayari tumekuja katika nchi ya taifa hili la miungu wa uongo.

19 Na Bwana akanitokea katika kujibu sala zangu, na akaniambia: Uzao wako nitawapa anchi hii.

20 Na mimi, Ibrahimu, nikaamka kutoka mahali pa madhabahu ambayo nilimjengea Bwana, na nikaondoka kutoka mahali hapo kuelekea mlima wa mashariki ya aBetheli, na nikapiga hema langu hapo, Betheli upande wa magharibi, na bAi upande wa mashariki; na huko nikamjengea Bwana madhabahu nyingine, na cnikaliitia tena jina la Bwana.

21 Na mimi, Ibrahimu, nikasafiri, nikiendelea kuelekea kusini; na kulikuwa na kuendelea kwa njaa katika nchi; nami, Ibrahimu, nikaishia kwenda katika Misri, ili kukaa huko, kwa kuwa njaa imekuwa kali.

22 Na ikawa wakati nilipokaribia kuingia Misri, Bwana akaniambia: Tazama, aSarai, mke wako, ni mwanamke mzuri wa sura;

23 Kwa hiyo itakuwa, wakati Wamisri watakapomwona, watasema—Huyu ni mke wake; nao watakuua, lakini watamwacha mke wako hai; kwa hiyo angalia kwamba unafanya hekima hii:

24 Mwache yeye aseme kwa Wamisri, kuwa yeye ni dada yako, na nafsi yako itaishi.

25 Na ikawa kwamba mimi, Ibrahimu, nikamwambia Sarai, mke wangu, yale yote ambayo Bwana aliniambia—Kwa hiyo uwaambie, ninakuomba, kuwa wewe u dada yangu, ili ipate kuwa heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu itaishi kwa sababu yako.