Misaada ya Kujifunza
TJS, Ufunuo 19


TJS, Ufunuo 19:15, 21. Linganisha na Ufunuo 19:15, 21

Mungu hutumia neno la Kristo ili kuyapiga mataifa.

15 Kutoka kinywani mwake hutoka neno la Mungu, na kwa hilo atawapiga mataifa; naye atawatawala kwa neno la kinywa chake; naye atakanyaga shinikizo la mvinyo katika ukali na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

21 Na wale mabaki waliuawa kwa neno lake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, neno ambalo lilitoka kinywani mwake; na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.