Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 67


Sehemu ya 67

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, mapema Novemba 1831. Tukio lilikuwa la mkutano maalumu, na uchapishaji wa mafunuo ambayo yalikuwa tayari yamepokelewa kutoka kwa Bwana kupitia nabii yalijadiliwa na kutendewa kazi (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 1). William W. Phelps alikuwa hivi karibuni ameanzisha kiwanda cha kupiga chapa katika Independence, Missouri. Mkutano uliamua kuchapisha mafunuo katika Book of Commandments (Kitabu cha Amri) na kupiga chapa nakala 10,000 (ambazo kwa sababu ya ugumu usio tarajiwa baadae zilipunguzwa na kuwa nakala 3000). Ndugu wengi wanatoa ushuhuda wa dhati kwamba mafunuo hayo ambayo yalikusanywa kwa ajili ya kuchapishwa yalikuwa ya kweli kabisa, kama vile Roho Mtakatifu alivyowashuhudia alipomwagwa juu yao. Historia ya Joseph Smith inaandika kuwa baada ya ufunuo unaojulikana kama sehemu ya 1 kupokelewa, maoni tofauti yalikuwepo kuhusu lugha iliyotumika katika mafunuo hayo. Ufunuo huu ulifuata.

1–3, Bwana husikiliza sala za wazee Wake na kuwaangalia; 4–9, Yeye anatoa changamoto kwa mwenye hekima kutoa japo ufunuo mmoja sawa na ufunuo mmoja mdogo kati ya mafunuo Yake; 10–14, Wazee waaminifu watahuishwa na Roho na watauona uso wa Mungu.

1 Tazama na sikilizeni, Enyi awazee wa kanisa langu, ambao mmejikusanya pamoja, ambao sala zenu nimezisikia, na ambao mioyo yenu ninaijua, na ambao matakwa yenu yamepanda juu mbele zangu.

2 Tazama, na lo, amacho yangu yapo juu yenu, na mbingu na dunia zipo mikononi mwangu, na utajiri wa milele ni juu yangu kuutoa.

3 Mlijitahidi kuamini kuwa yawapasa kupokea baraka ambazo zilitolewa kwenu; lakini tazama, amini ninawaambia kuwa kulikuwa na awoga katika mioyo yenu, na amini hii ndiyo sababu ya kuwa ninyi hamkupata.

4 Na sasa Mimi, Bwana ninawapa aushuhuda wa ukweli wa amri hizi ambazo zimewekwa mbele yenu.

5 Macho yenu yamekuwa juu ya mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na alugha yake ninyi mnaijua, na udhaifu wake mnaujua; nanyi mmetafuta katika mioyo yenu maarifa ili muweze kuielekeza kupita lugha yake; hii pia mnajua.

6 Sasa, ninyi tafuteni kutoka katika Kitabu cha Amri, hata ile isiyo muhimu miongoni mwao, na mteueni yule aliye na ahekima kuliko wote miongoni mwenu;

7 Au, kama kuna yeyote miongoni mwenu ambaye atafanya mmoja kama huo, ndipo mtakuwa na haki katika kusema kuwa hamjui kwamba ni ya kweli;

8 Lakini, kama hamwezi kufanya hata mmoja kama huo, ninyi mna hatia kama ahamshuhudii kwamba ni ya kweli.

9 Kwani mnajua kuwa hamna udhalimu ndani yake, na kwamba kile kilicho cha ahaki hutoka juu, kutoka kwa Baba wa bmianga.

10 Na tena amini ninawaambia kuwa hii ni nafasi kwenu, na ahadi ninaitoa kwa wale waliotawazwa kwa huduma hii, kuwa kwa kadiri mtakavyojivua ninyi wenyewe kuondokana na awivu na bwoga, na cmkajinyenyekeza mbele zangu, kwa kuwa hamjawa wanyenyekevu vya kutosha, dpazia litapasuka nanyi emtaniona Mimi ndiye—siyo kwa akili ya kimwili wala ya asili, bali ya kiroho.

11 Kwani hakuna amtu aliyemwona Mungu wakati wowote, isipokuwa amehuishwa na Roho wa Mungu.

12 Wala haiwezekani amwanadamu wa asili akastahimili uwepo wa Mungu, wala kwa namna ya akili ya kimwili.

13 Ninyi hamwezi kustahimili uwepo wa Mungu sasa, wala kutumikiwa na malaika; kwa hiyo, endeleeni katika auvumilivu hadi mtakapokuwa bmmekamilika.

14 Na akili zenu zisiangalie nyuma; na wakati amtakapostahili, katika wakati wangu mwenyewe, mtaona na kujua kile ambacho kilitolewa juu yenu kwa mikono ya mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo. Amina.