Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 5


Sehemu ya 5

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Harmony, Pennsylvania, Machi 1829, kwa maombi ya Martin Harris.

1–10, Kizazi hiki kitapokea neno la Bwana kupitia Joseph Smith; 11–18, Mashahidi watatu watakishuhudia Kitabu cha Mormoni; 19–20, Neno la Bwana litadhihirishwa kama katika nyakati zilizopita; 21–35, Martin Harris aweza kutubu na kuwa mmoja wa mashahidi hao.

1 Tazama, ninakuambia wewe, kwamba kama vile mtumishi wangu aMartin Harris alivyotaka ushahidi kutoka kwangu, kwamba wewe, mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, unayo bmabamba, ambayo umeyashuhudia na umeshuhudia kwamba umeyapata kwangu;

2 Na sasa, tazama, hili ndilo utakalomwambia yeye—yule aliyesema nawe, alikuambia: Mimi, Bwana, ndiye Mungu, na nimekupa mambo haya wewe, mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na nimekuamuru wewe kwamba usimame kama ashahidi wa mambo haya;

3 Na nimekusababisha wewe kwamba uingie katika agano na Mimi, kwamba yakupasa usiyaonyeshe, ila kwa awatu wale tu ambao nimekuamuru, na wala huna buwezo juu yake ila ninapokupa.

4 Na unacho kipawa cha kutafsiri mabamba haya; na hiki ni kipawa cha kwanza nilichokupa; na nimekuamuru kwamba usidai kipawa kingine chochote mpaka makusudi yangu yatakapotimilika katika hili; kwani sitakupatia kipawa kingine mpaka itakapomalizika.

5 Amini, ninakuambia wewe, kwamba huzuni itawajia wakazi wa dunia kama ahawatasikiliza maneno yangu;

6 Kwani baada ya hapa autatawazwa na kuanza kuyaeneza bmaneno yangu kwa wanadamu.

7 Tazama, kama ahawatayaamini maneno yangu, hawatakuamini wewe, mtumishi wangu Joseph, hata kama ingewezekana kwamba uwaonyeshe mambo haya yote ambayo nimeyakabidhi kwako.

8 O, hiki kizazi akisichoamini na cha wenye bshingo ngumu—hasira yangu inawaka juu yao.

9 Tazama, amini ninakuambia wewe, animeyahifadhi mambo haya ambayo nimeyaaminisha mikononi mwako, mtumishi wangu Joseph, kwa kusudi la hekima yangu, na itajulikana katika vizazi vijavyo;

10 Lakini kizazi hiki kitapata neno langu kupitia kwako;

11 Na kwa nyongeza juu ya ushuhuda wako, aushuhuda wa watumishi wangu watatu, ambao nitawaita na kuwatawaza, ambao kwa hao nitayaonyesha mambo haya, nao watakwenda na maneno yangu ambayo yatatolewa kupitia kwako.

12 Ndiyo, wao watajua kwa uhakika kwamba mambo haya ni ya kweli, kwani kutoka mbinguni nitawatangazia.

13 Nitawapa wao uwezo kwamba waweze kuyatazama na kuyaona mambo haya kama yalivyo;

14 Na asitatoa uwezo huu kwa mtu mwingine awaye yeyote, kupokea ushuhuda wa aina hii miongoni mwa watu wa kizazi hiki, katika huu mwanzo wa kuinuka na kuchomoza kwa bkanisa langu kutoka nyikani—wazi kama cmbalamwezi, na angavu kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye bendera.

15 Na kwa ushuhuda wa amashahidi watatu nitalieneza neno langu.

16 Na tazama, wale wote awatakaoamini juu ya maneno yangu, hao bnitawajia kwa cufunuo wa dRoho wangu; nao ewatazaliwa kwangu, hata kwa maji na kwa Roho—

17 Na lazima usubiri kitambo kidogo, kwani bado ahaujatawazwa

18 Na ushuhuda wao pia utaenea kama ahukumu kwa kizazi hiki kama wataishupaza mioyo yao dhidi yao;

19 Kwani apigo la ukiwa litapita miongoni mwa wakazi wa ulimwengu, nalo litazidi kumiminwa kutoka wakati hadi wakati, kama bhawatatubu, mpaka dunia itakuwa ctupu, na wakazi wake wameteketezwa na wameangamizwa kabisa kwa mngʼaro wa dkuja kwangu.

20 Tazama, ninakuambia mambo haya, kama vile anilivyowaambia watu juu ya kuangamia kwa Yerusalemu; na bneno langu litadhihirika wakati huu kama lilivyodhihirika hapo awali.

21 Na sasa ninakuamuru wewe, mtumishi wangu Joseph, kutubu na kutembea wima zaidi mbele zangu, na wala usishawishiwe tena na wanadamu;

22 Na ya kwamba uwe imara katika akushika amri ambazo nimekuamuru wewe; na kama utayafanya haya, tazama nitakupa uzima wa milele, hata kama butauawa.

23 Na sasa, tena, ninakuambia wewe, mtumishi wangu Joseph, kuhusu amtu huyo autakaye ushahidi—

24 Tazama, ninamwambia yeye, anajikweza yeye mwenyewe na wala hajinyenyekezi vya kutosha mbele zangu; ila kama atainama mbele yangu, na kujinyenyekeza mwenyewe katika sala ya nguvu na imani, katika dhamira thabiti ya moyo wake, ndipo nitampa yeye akuyaona mambo anayotamani kuyaona.

25 Na ndipo atasema kwa watu wa kizazi hiki: Tazama, nimeyaona mambo ambayo Bwana ameyaonyesha kwa Joseph Smith, Mdogo. Na aninajua kwa hakika kuwa ni ya kweli, kwani nimeyaona, na yameonyeshwa kwangu kwa nguvu za Mungu na wala siyo kwa nguvu za mwanadamu.

26 Na Mimi Bwana, ninamwamuru yeye, mtumishi wangu Martin Harris, kwamba hatasema tena kwao kuhusu mambo haya, bali atasema: Nimeyaona, na kwamba yameonyeshwa kwangu kwa nguvu za Mungu; na haya ndiyo maneno atakayosema.

27 Lakini kama atayakana haya atavunja agano ambalo ameagana na Mimi, na tazama, amelaaniwa.

28 Na sasa, kama hakujinyenyekeza mwenyewe, na kukiri kwangu mambo ambayo ameyafanya siyo sahihi, na kuagana na Mimi kwamba atazishika amri zangu, na kuwa na imani nami, tazama, ninamwambia yeye, hatapata kuyaona, kwani sitampa yeye kuona mambo haya ambayo nimeyazungumza.

29 Na kama hivyo ndivyo ilivyo, ninakuamuru wewe, mtumishi wangu Joseph, kwamba utamwambia yeye, kwamba asifanye zaidi, wala asinisumbue tena juu ya jambo hili.

30 Na kama hivyo ndivyo ilivyo, tazama, ninakuambia wewe Joseph, wakati wewe utakapokuwa umetafsiri kurasa nyingine chache na usimame kwa kipindi, hadi nitakapokuamuru tena; ndipo waweza kutafsiri tena.

31 Na endapo hautafanya haya, tazama, wewe hutakuwa na kipawa tena, na nitachukua kutoka kwako mambo ambayo nimekuaminisha wewe.

32 Na sasa, kwa sababu ninawaotea watu wenye hila wanaovizia kukuangamiza, ndiyo, ninaotea kwamba, kama mtumishi wangu Martin Harris hajinyenyekezi mwenyewe na akapokea ushuhuda kutoka mkononi mwangu, kwamba ataanguka katika uvunjaji wa sheria;

33 Na kuna wengi wanaovizia kwa hila akukuangamiza wewe kutoka katika uso wa dunia; na kwa sababu hiyo, kwamba siku zako zitaongezwa, nimekupa wewe amri hizi.

34 Ndiyo, kwa sababu hii, nimesema: Simama, na ubaki hivyo mpaka nitakapokuamuru, na anitakupa njia ambazo wewe waweza kumalizia mambo haya niliyokuamuru.

35 Na kama wewe utakuwa amwaminifu katika kuzishika amri zangu, na wewe butainuliwa juu siku ile ya mwisho. Amina.