Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 30


Sehemu ya 30

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa David Whitmer, Peter Whitmer Mdogo, na John Whitmer, huko Fayette, New York, Septemba 1830, baada ya mkutano wa siku tatu huko Fayette, lakini kabla ya wazee wa Kanisa hawajaachana. Mwanzoni ufunuo huu ulichapishwa kama mafunuo matatu; yaliunganishwa pamoja kuwa sehemu moja na Nabii mwenyewe kwa ajili ya toleo la mwaka 1835 la Mafundisho na Maagano.

1–4, David Whitmer anakanywa kwa kushindwa kuhudumu kwa bidii; 5–8, Peter Whitmer Mdogo ataambatana na Oliver Cowdery katika misheni kwa Walamani; 9–11, John Whitmer ameitwa ili kuihubiri injili.

1 Tazama, ninakuambia, aDavid, kwamba bumemwogopa mwanadamu na wala chukunitegemea mimi nikupe nguvu kama ulivyotakiwa kufanya.

2 Bali akili yako imekuwa juu ya mambo ya adunia zaidi kuliko mambo yangu, Muumba wako, na huduma ambayo wewe umeitiwa; na wala hukumfuata Roho wangu, na wale waliowekwa juu yako, lakini ukashawishiwa na wale ambao sikuwaamuru.

3 Kwa hiyo, umeachwa kujiulizia mwenyewe kutoka kwangu, na akuyatafakari mambo ambayo umeyapokea.

4 Na nyumbani kwao kutakuwa katika nyumba ya baba yako, hadi nitakapokupa amri zaidi. Na utatenda ahuduma yako katika kanisa, na mbele ya ulimwengu, na katika maeneo yanayokuzunguka. Amina.

5 Tazama, ninakuambia, aPeter, kwamba utafunga bsafari yako pamoja na kaka yako Oliver; kwani cwakati umewadia unao faa kwangu Mimi kuwa yawapasa kufumbua vinywa vyenu ili kuitangaza injili yangu; kwa hiyo, usiogope, bali dtii maneno na ushauri wa kaka yako, ambao atakupa.

6 Na uteseke katika mateso yake yote, daima ukiinua moyo wako kwangu katika sala na imani, kwa ajili ya ukombozi wake na wako; kwani nimempatia yeye uwezo wa kujenga akanisa langu miongoni mwa bWalamani;

7 Na hapana yeyote niliyemteua kuwa mshauri ajuu yake katika kanisa, kuhusu mambo ya kanisa, isipokuwa kaka yake, Joseph Smith, Mdogo.

8 Kwa hiyo, yatii mambo haya na uwe mwenye bidii katika kushika amri zangu, na utabarikiwa kwa uzima wa milele. Amina.

9 Tazama, ninakuambia, mtumishi wangu John, kwamba utaanza kutoka wakati huu akuitangaza injili yangu, kama vile kwa bsauti ya parapanda.

10 Na kazi yako itakuwa huko kwa kaka yako Philip Burroughs, na katika maeneo yaliyo karibu, ndiyo, popote unapoweza kusikika, hadi nitakapokuamuru kuondoka hapa.

11 Na kazi yako yote itakuwa katika Sayuni, kwa moyo wako wote, kutoka sasa na kuendelea; ndiyo, daima utafungua kinywa chako katika kazi yangu, bila akuogopa bmwanadamu awezacho kukufanya, kwani Mimi niko cpamoja nawe. Amina.