Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 29


Sehemu ya 29

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, mbele ya wazee sita, huko Fayette, New York, Septemba 1830. Ufunuo huu ulitolewa siku kadhaa kabla ya mkutano, kuanzia 26 Septemba 1830.

1–8, Kristo anawakusanya wateule Wake; 9–11, Ujio wake waonyesha kuanza kwa Milenia; 12–13, Mitume Kumi na Wawili watawahukumu wana wa Israeli wote; 14–21, Ishara, mabaa, na ukiwa utautangulia Ujio wa Pili; 22–28, Ufufuo wa mwisho na hukumu ya mwisho itafuatia Milenia; 29–35, Mambo yote kwa Bwana ni ya kiroho; 36–39, Ibilisi na Majeshi yake walifukuzwa kutoka mbinguni ili wawajaribu wanadamu; 40–45, Anguko na Upatanisho huleta wokovu; 46–50, Watoto wadogo wamekombolewa kupitia Upatanisho.

1 Sikilizeni sauti ya Yesu Kristo, Mkombozi wenu, aMimi Ndimi Mkuu, ambaye mkono wake wa brehema umefanya cupatanisho kwa ajili ya dhambi zenu;

2 Ambaye aatawakusanya watu wake kama kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mabawa yake, hata wengi kadiri watakavyoifuata sauti yangu na bkujinyenyekeza mbele zangu, na kunilingana kwa sala kuu.

3 Tazama, amini, amini, ninawaambia, kwamba kwa wakati huu dhambi zenu azimesamehewa, kwa sababu hiyo pokeeni mambo haya; lakini kumbukeni msitende dhambi tena, isije hatari kubwa ikaja juu yenu.

4 Amini, ninawaambia kwamba ninyi ni wateule toka ulimwenguni kwa kuitangaza injili yangu kwa shangwe, kama shangwe, kama asauti ya parapanda.

5 Inueni mioyo yenu na furahini, kwani Mimi niko akatikati yenu, na ni bmtetezi wenu kwa Baba; na ni mapenzi yake kuwapa ule cufalme.

6 Na, kama ilivyoandikwa—Lolote amtakaloomba katika bimani, mkiwa cmmeungana katika sala mkiamini kulingana na amri yangu, mtapokea.

7 Na ninyi mmeitwa akuwakusanya bwateule wangu; kwani wateule wangu chuisikia sauti yangu na wala hawaishupazi dmioyo yao;

8 Kwa hiyo amri imetoka kwa Baba kwamba awakusanywe mahali pamoja juu ya uso wa nchi hii, ili bkuitayarisha mioyo yao na kujitayarisha katika mambo yote dhidi ya siku ile wakati ctaabu na ukiwa vitakapokuja juu ya waovu.

9 Kwani saa i karibu na siku yaja haraka wakati dunia imekomaa; na wote wenye akiburi na wao ambao hufanya maovu watakuwa kama bmakapi; na cnitawateketeza, asema Bwana wa Majeshi, kwamba uovu hautakuwepo duniani;

10 Kwani saa i karibu, na yale ayaliyonenwa na mitume wangu lazima yatatimia; kwani kama vile walivyosema ndivyo itakavyokuwa;

11 Kwani nitajifunua mwenyewe kutoka mbinguni kwa uwezo na utukufu mkuu, pamoja na amajeshi yote ya mbinguni, na kukaa katika bhaki pamoja na wanadamu duniani miaka celfu moja, na waovu hawatastahimili.

12 Na tena, amini, amini, ninawaambia, na imetolewa amri kali, kwa mapenzi yake Baba, kwamba amitume wangu, wale Kumi na Wawili ambao walikuwa nami katika huduma yangu kule Yerusalemu, watasimama mkono wangu wa kuume katika siku ile ya kuja kwangu katika nguzo ya bmoto, wakiwa wamevikwa joho ya haki, na mataji juu ya vichwa vyao, katika cutukufu kama vile Mimi nilivyo, dkuihukumu nyumba yote ya Israeli, kadiri ya wengi jinsi walivyonipenda Mimi na kushika amri zangu, na siyo wengineo.

13 Kwani aparapanda italia kwa sauti yenye kuendelea na kwa sauti, kama vile juu ya Mlima wa Sinai, na dunia yote itatetemeka, nao bwatatoka—ndiyo, hata wafu cwaliokufa katika Mimi, ili kupokea dtaji la haki, na kuvishwa, ekama Mimi, na kuwa pamoja nami, ili tuweze kuwa na umoja.

14 Lakini, tazama, ninawaambia kwamba kabla asiku hii kuu haijaja bjua litatiwa giza, na mwezi utageuzwa kuwa damu, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na kutakuwa na cishara kuu katika mbingu juu na nchi chini;

15 Na kutakuwa na kulia na akuomboleza miongoni mwa umati wa watu;

16 Na kutakuwa atufani kuu itakayoletwa ili kuangamiza mazao ya ulimwengu.

17 Na itakuwa kwa sababu ya uovu wa ulimwengu, kwamba nitalipiza akisasi juu ya bwaovu, kwa kuwa hawatatubu; kwani kikombe cha uchungu wa hasira yangu kimejaa; kwani tazama, cdamu yangu haitawatakasa kama hawatanisikiliza.

18 Kwa hiyo, Mimi Bwana Mungu nitawaleta inzi juu ya uso wa dunia, ambao watawazidi wakazi wake, nao watakula nyama zao, na kusababisha funza kuingia ndani yao;

19 Na ndimi zao zitazuiliwa kwamba ahazitanena dhidi yangu; na nyama ya miili yao itaanguka kutoka kwenye mifupa yao, na macho yao kutoka kwenye matundu yake;

20 Na itakuwa kwamba awanyama wa porini na ndege wa angani watawala.

21 Na kanisa lile kuu na la amachukizo, ambalo ni bkahaba wa ulimwengu wote, litaangamizwa kwa cmoto uteketezao, kama ilivyonenwa kwa kinywa cha Ezekieli nabii, ambaye alinena juu ya mambo haya, ambayo bado hayajatokea bali kwa hakika ni dlazima, kama vile Mimi niishivyo, kwani machukizo hayawezi kutawala.

22 Na tena, amini, amini, ninawaambia kwamba na hiyo miaka aelfu itakapokwisha, na wanadamu wakianza tena kumkataa Mungu wao, ndipo nitakapouachia ulimwengu lakini kwa bmuda mchache;

23 Na amwisho utakapokuja, na mbingu na dunia zitaangamizwa na bkupita, na hapo patakuwa na mbingu mpya na cdunia mpya.

24 Na ya kale yote ayatapita, na yote yatakuwa mapya, hata mbingu na dunia, na vyote vilivyomo, watu na wanyama, ndege wa angani, na samaki wa baharini;

25 Na hapana hata aunywele mmoja, wala chembe moja, itakayopotea, kwani hiyo ni kazi ya mikono yangu.

26 Lakini, tazama, amini ninawaambia, kabla dunia haijapita, aMikaeli, bmalaika wangu mkuu, atapiga cparapanda yake, na ndipo wafu wote dwataamka, kwani makaburi yao yatafunguka, nao ewatatoka—ndiyo, hata wote.

27 Na awenye haki watakusanywa bmkono wangu wa kuume kwa uzima wa milele; na waovu mkono wangu wa kushoto ndiyo ambao nitaona aibu kuwamiliki mbele za Baba;

28 Kwa hiyo nitawaambia—aOndokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika bmoto usio na mwisho, aliowekewa tayari cibilisi na malaika zake,

29 Na sasa, tazama, ninawaambia, kamwe wakati wowote sijawahi kueleza kutoka kinywani mwangu kwamba watarejea, kwani amahali nilipo hawawezi kufika, kwani hawana uwezo huo.

30 Lakini kumbukeni kwamba hukumu zangu zote hazijatolewa kwa wanadamu; na kama vile maneno yalivyotoka kinywani mwangu hivyo alivyo yatakayotimia, kwamba wa akwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza katika mambo yote niliyoyaumba kwa amri ya uwezo wangu, ambao ni nguvu ya Roho wangu.

31 Kwani kwa nguvu ya Roho wangu aniliviumba; ndiyo, vitu vyote vya bkiroho na kimwili—

32 Kwanza akiroho, pili kimwili, ambao ndiyo mwanzo wa kazi yangu; na tena, kwanza kimwili, na pili kiroho, ambao ndiyo mwisho wa kazi yangu—

33 Nikizungumza nanyi ili mpate kuelewa kwa namna ya kawaida; lakini kwangu mimi mwenyewe kazi zangu hazina amwisho, wala mwanzo; lakini imetolewa kwenu ili mpate kuelewa, kwa sababu mmeniomba na kukubaliwa.

34 Kwa hiyo, amini ninawaambia kwamba mambo haya yote kwangu mimi ni ya kiroho, na hata wakati wowote sijatoa sheria kwenu ambayo ni ya kimwili; wala mtu yeyote, wala wanadamu; wala si Adamu, baba yenu, ambaye nilimuumba.

35 Tazama, nilimpa yeye ili apate akujiamulia mwenyewe; na nikampa amri, lakini siyo amri ya kimwili nilimpa yeye, kwani bamri zangu ni za kiroho; siyo za kiasili wala kimwili, si tamaa ya kimwili wala si ya kianasa.

36 Na ikawa kwamba Adamu, akijaribiwa na ibilisi—kwani, tazama, aibilisi alikuwako kabla ya Adamu, kwani yeye baliniasi mimi, akisema, Nipe mimi cheshima yako, ambayo ndiyo duwezo wangu; na pia etheluthi moja ya fmajeshi ya mbinguni aliyafanya yanigeuke kwa sababu ya ghaki yao ya kujiamulia;

37 Na wakatupwa chini, na hivyo ndivyo kuja kwa aibilisi na bmalaika zake;

38 Na, tazama, kuna mahali palipotayarishwa kwa ajili yao kutoka mwanzo, mahali hapo ni ajehanamu.

39 Na hapana budi kwamba ibilisi lazima aawajaribu wanadamu, vinginevyo hawangeweza kujiamulia wao wenyewe; kwani kama kamwe hawakuonja buchungu wasingeliweza kuijua utamu—

40 Kwa hiyo ikawa kwamba ibilisi akamjaribu Adamu, na yeye akala atunda lililokatazwa, na akaivunja amri, hivyo basi akajiingiza bchini ya matakwa ya ibilisi, kwa sababu alikubali majaribu.

41 Kwa hiyo, Mimi, Bwana Mungu, anikamfukuza kutoka katika Bustani ya bEdeni, kutoka machoni pangu, kwa sababu ya uvunjaji wake wa sheria, kwa ajili hiyo akawa mfu ckiroho, ambacho ni kifo cha kwanza, ambacho ni sawa sawa na dkifo cha mwisho, ambacho ni cha kiroho, ambacho kitahukumiwa kwao walio waovu nitakaposema: Ondokeni, ninyi emliolaaniwa.

42 Lakini, tazama, ninawaambia kwamba Mimi, Bwana Mungu, nilitoa kwa Adamu na uzao wake, kwamba awasife kwa kifo cha kimwili, hadi Mimi, Bwana Mungu, nitakapowatuma bmalaika kutangaza kwao ctoba na dukombozi, kwa njia ya imani juu ya jina la eMwana Pekee.

43 Na hivyo ndivyo nilivyofanya Mimi, Bwana Mungu, kumteua mtu kama siku zake za amajaribio—kwamba kwa kifo chake cha kimwili aweza bkuinuliwa katika cmwili usiokufa hadi duzima wa milele, hata wengi kadiri watakavyoamini;

44 Na wale wasioamini juu ya alaana ya milele; kwani hawawezi kukombolewa kutokana na anguko lao la kiroho, kwa sababu hawatubu;

45 Kwani wao hupenda zaidi giza kuliko nuru, na amatendo yao ni maovu, na wao hupokea bujira wao kwa yeye wanayemtii.

46 Lakini tazama, ninawaambia, kuwa awatoto wadogo bwamekombolewa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa njia ya Mwanangu wa Pekee;

47 Kwa hiyo hawafanyi dhambi, kwani uwezo haujatolewa kwa Shetani wa akuwajaribu watoto wadogo, hadi wanapoanza bkuwajibika mbele zangu;

48 Kwani imetolewa kwao hata kama vile nitakavyo Mimi, kulingana na mapenzi yangu, ili kwamba mambo muhimu yaweze kuhitajika kutoka kwenye mikono ya ababa zao.

49 Na, tena, ninawaambia, kwamba yeyote aliye na maarifa, sijamuamuru kutubu?

50 Na yeye ambaye hana aufahamu, hubaki ndani yangu kufanya kama ilivyoandikwa. Na sasa sitasema zaidi kwenu kwa wakati huu. Amina.