Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 2


Sehemu ya 2

Dondoo kutoka katika historia ya Joseph Smith kuhusiana na maneno ya malaika Moroni kwa Joseph Smith Nabii, wakiwa ndani ya nyumba ya baba yake Nabii huko Manchester, New York, jioni ya 21 Septemba 1823. Moroni alikuwa wa mwisho katika safu ndefu ya wanahistoria ambao walitengeneza kumbukumbu ambayo sasa iko mbele ya ulimwengu kama Kitabu cha Mormoni. (Linganisha na Malaki 4:5–6; pia sehemu ya 27:9; 110:13–16; na 128:18.)

1, Eliya ataufunua ukuhani; 2–3, Ahadi za baba zapandikizwa katika mioyo ya watoto.

1 Tazama, nitaufunua kwenu Ukuhani, kwa mkono wa aEliya, nabii, kabla ya kuja kwa siku ile bkuu na ya kutisha ya Bwana.

2 aNaye atapandikiza katika mioyo ya watoto bahadi zilizofanywa kwa baba, na mioyo ya watoto itawageukia baba zao.

3 Kama si hivyo, dunia yote ingeliangamia kabisa wakati wa kuja kwake.