Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 108


Sehemu ya 108

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 26 Desemba 1835. Sehemu hii ilipokelewa kwa ombi la Lyman Sherman, ambaye mwanzoni alikuwa ametawazwa kama sabini, na ambaye alikuja kwa Nabii akiwa na ombi la ufunuo wa kujulishwa wajibu wake.

1–3, Lyman Sherman asamehewa dhambi zake; 4–5, Ahesabiwe pamoja na wazee viongozi wa Kanisa; 6–8, Yeye ameitwa kuihubiri injili na kuwaimarisha ndugu zake.

1 Amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwako, mtumishi wangu Lyman: Dhambi zako zimesamehewa, kwa sababu umetii sauti yangu kwa kuja hapa asubuhi hii kupokea ushauri wake yeye niliyemteua.

2 Kwa hiyo, nafsi yako na aitulie juu ya msimamo wako wa kiroho, na usiikatae tena sauti yangu.

3 Na amka na uwe mwangalifu zaidi kutoka sasa katika kutimiza nadhiri zako, ambazo umezifanya na unazozifanya, nawe utabarikiwa kwa baraka kubwa kupita kiasi.

4 Subiri kwa uvumilivu hadi akusanyiko la kiroho litakapoitishwa la watumishi wangu, ndipo nawe utakumbukwa pamoja na wazee wangu wa kwanza, na kupokea haki kwa kutawazwa na wazee wangu wengine wote ambao nimewateua.

5 Tazama, hii ni aahadi ya Baba kwako kama utaendelea kuwa mwaminifu.

6 Nayo itatimizwa juu yako katika siku ile ili uwe na haki ya akuhubiri injili yangu popote nitakapokutuma, kutoka hapo na kutoka wakati huo.

7 Kwa hiyo, awaimarishe ndugu zako katika mazungumzo yako yote, katika sala zako zote, katika kushawishi kwako kote, na katika matendo yako yote.

8 Na tazama, na lo, Mimi ni pamoja nawe ili kukubariki na akukuokoa wewe milele. Amina.