Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 106


Sehemu ya 106

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Kirtland, Ohio, 25 Novemba 1834. Ufunuo huu unaelekezwa kwa Warren A. Cowdery, kaka mkubwa wa Oliver Cowdery.

1–3, Warren A. Cowdery anaitwa kuwa ofisa kiongozi wa eneo analoishi; 4–5, Ujio wa Pili hautawapita watoto wa nuru kama mwizi; 6–8, Baraka kubwa hufuata utumishi wa uaminifu katika Kanisa.

1 Ni mapenzi yangu kwamba mtumishi wangu Warren A. Cowdery ateuliwe na kutawazwa kuwa kuhani mkuu kiongozi juu ya kanisa langu, katika nchi ya aFreedom na maeneo yanayoizunguka;

2 Na ni lazima aihubiri injili yangu isiyo na mwisho, na kupaza sauti yake na kuwaonya watu, siyo tu katika sehemu yake mwenyewe, bali katika wilaya zinazopakana;

3 Na autoe muda wake wote kwa wito huu mtakatifu na wa juu, ambao sasa ninampa, aakiutafuta kwa bidii bufalme wa mbinguni na haki zake, na mambo yote ya lazima yataongezwa juu yake; kwani cmfanyakazi anastahili ujira wake.

4 Na tena, amini ninawaambia, aujio wa Bwana bunakaribia, nao utaupata ulimwengu kama cmwivi ajavyo usiku—

5 Kwa hiyo, jifungeni viuno vyenu, ili mpate kuwa watoto wa anuru, na siku ile bisiwapate kama mwivi.

6 Na tena, amini ninawaambia, palikuwa na shangwe mbinguni wakati mtumishi wangu Warren aliposujudu kwenye fimbo yangu ya ufalme, na kujitenga na ujanja wa wanadamu;

7 Kwa hiyo, heri mtumishi wangu Warren, kwani nitakuwa na huruma juu yake; na, bila kujali akiburi cha moyoni mwake, nitamwinua juu kadiri yeye atakavyo jinyenyekeza mbele zangu.

8 Nami nitampa aneema na uhakika ambao kwayo aweze kusimama; na kama ataendelea kuwa shahidi mwaminifu na nuru kwa kanisa nimeandaa taji kwa ajili yake katika bmakao ya Baba yangu. Hivyo ndivyo. Amina.