Maandiko Matakatifu
Maneno ya Mormoni 1


Maneno ya Mormoni

Mlango wa 1

Mormoni anafupisha mabamba makubwa ya Nefi—Anaweka mabamba yale madogo na mabamba yale mengine—Mfalme Benjamini anaimarisha amani nchini. Karibia mwaka 385 B.K.

1 Na sasa mimi, aMormoni, nikikaribia kuyakabidhi yale maandishi ambayo nimeandika mikononi mwa mwana wangu Moroni, tazama nimeshuhudia karibu maangamizo yote ya watu wangu, Wanefi.

2 Na ni baada ya miaka mia akadha baada ya kuja kwa Kristo ninapompatia mwana wangu maandishi haya; na ninadhani kwamba atashuhudia maangamizo yote ya watu wangu. Lakini na Mungu amjalie aweze kuishi, ili aandike juu yao, na kwa vyovyote kuhusu Kristo, ili pengine bwafaidike katika nyakati zingine.

3 Na sasa, ninazungumza kuhusu yale ambayo nimeandika; kwani baada ya kufanya aufupisho kutoka yale bmabamba ya Nefi, hadi utawala wa huyu mfalme Benjamini, ambaye alizungumziwa na Amaleki, nilipekua miongoni mwa cmaandishi haya niliyopewa, na nikapata mabamba haya, ambayo yalikuwa na historia hii ndogo ya manabii, kutoka Yakobo hadi utawala huu wa mfalme dBenjamini, na pia maneno mengi ya Nefi.

4 Na vitu ambavyo vimo katika mabamba haya avinanifurahisha, kwa sababu ya unabii wa kuja kwa Kristo; na baba zangu wakijua kwamba vingi vimetimizwa; ndiyo, na pia najua kwamba vingi vilivyobashiriwa kutuhusu sisi hadi siku hii vimetimizwa, na vingi ambavyo vitazidi leo lazima kwa ukweli vitatokea—

5 Kwa hivyo, nachagua avitu hivi, ili nimalize maandishi yangu juu yao, maandishi ambayo nitatoa kutoka bmabamba ya Nefi; na siwezi kuandika hata sehemu moja ya cmia ya vitu vya watu wangu.

6 Lakini tazama, nitachukua mabamba haya, ambayo yana unabii na ufunuo, na kuyaweka pamoja na mabaki ya yale maandishi yangu, kwani ni bora kwangu; na ninajua kwamba yatakuwa bora kwa ndugu zangu.

7 Na ninatenda haya kwa madhumuni ya abusara; kwani ninanongʼonezewa, kulingana na kazi za Roho wa Bwana aliye ndani yangu. Na sasa, sijui mambo yote; lakini Bwana banajua vitu vyote vitakavyokuja; kwa hivyo, anafanya kazi ndani yangu ili nitende kulingana na nia yake.

8 Na asala yangu kwa Mungu ni kuhusu ndugu zangu, kwamba wamfahamu Mungu tena, ndiyo, ukombozi wa Kristo; ili tena wawe watu bwema.

9 Na sasa mimi, Mormoni, namalizia maandishi yangu, ambayo ninayatoa kutoka mabamba ya Nefi; na ninayaandika kulingana na maarifa na ufahamu ambao Mungu amenipatia.

10 Kwa hivyo, ikawa kwamba baada ya Amaleki akumpatia mfalme Benjamini mabamba haya, aliyachukua na kuyaweka pamoja na yale bmabamba mengine, ambayo yalikuwa na maandishi ambayo yalitolewa na cwafalme, kutoka kizazi hadi kizazi mpaka siku za Benjamini.

11 Na yalipitishwa kutoka mfalme Benjamini, kutoka kizazi hadi kizazi mpaka zikafika amikononi mwangu. Na mimi, Mormoni, naomba Mungu kwamba yahifadhiwe tangu sasa. Na ninajua kwamba yatahifadhiwa; kwani kuna mambo makuu ambayo yameandikwa juu yake, ambayo byatahukumu watu wangu na ndugu zao katika siku ile kuu ya mwisho, kulingana na neno la Mungu ambalo limeandikwa.

12 Na sasa, kuhusu huyu mfalme Benjamini—alikuwa na mabishano fulani miongoni mwa watu wake.

13 Na ikawa kwamba pia majeshi ya Walamani yaliondoka anchi ya Nefi, ili yapigane na watu wake. Lakini tazama, mfalme Benjamini alikusanya pamoja majeshi yake, na akawapinga; na alipigana kwa nguvu ya mkono wake mwenyewe, akitumia bupanga wa Labani.

14 Na kwa nguvu za Bwana walipigana dhidi ya maadui wao, hadi wakawaua maelfu mengi ya Walamani. Na ikawa kwamba walipigana na Walamani hadi wakawaondoa kutoka nchi yao yote ya urithi wao.

15 Na ikawa kwamba baada ya kuwa na aKristo wengi bandia, na vinywa vyao vikafungwa, na wakaadhibiwa kulingana na makosa yao;

16 Na baada ya kuwepo na manabii wa bandia, na wahubiri bandia na walimu bandia miongoni mwa watu, na hawa wote wakiwa wameadhibiwa kulingana na makosa yao; na baada ya kuwepo na ubishi mwingi na ukengeufu mwingi kwa Walamani, tazama, ikawa kwamba mfalme Benjamini, kwa msaada wa amanabii watakatifu waliokuwa miongoni mwa watu wake—

17 Kwani tazama, mfalme Benjamini alikuwa mtu amtakatifu, na alitawala watu wake kwa haki; na kulikwa na watu wengi watakatifu nchini ile, na walinena neno la Mungu kwa bnguvu na mamlaka; na walitumia cukali mwingi kwa sababu ya utukutu wa wale watu—

18 Kwa hivyo, kwa msaada wa hawa, mfalme Benjamini, kwa kutumikia kwa nguvu zote za mwili wake na uwezo wa nafsi yake yote, na pia manabii, aliimarisha tena amani katika nchi ile.