Maandiko Matakatifu
Omni 1


Kitabu cha Omni

Mlango wa 1

Omni, Amaroni, Kemishi, Abinadomu, na Amaleki, kila mmoja, anaweka yale maandishi—Mosia anavumbua watu wa Zarahemla, ambao walitoka Yerusalemu katika siku za Zedekia—Mosia anafanywa kuwa mfalme wao. Wazao wa Muleki katika Zarahemla walikuwa wamevumbua Koriantumuri, Myaredi wa mwisho—Mfalme Benjamini anamrithi Mosia—Inafaa wanadamu wamtolee Kristo nafsi zao kama sadaka. Karibia mwaka 323–130 K.K.

1 Tazama, ikawa kwamba mimi, Omni, nikiwa nimeamriwa na baba yangu, Yaromu, kwamba niandike kwenye mabamba haya, ili nasaba yetu ihifadhiwe—

2 Kwa hivyo, ningetaka mjue kwamba, katika maisha yangu, nilipigana sana kwa upanga ili kuwahifadhi watu wangu, Wanefi, wasianguke mikononi mwa maadui wao, Walamani. Lakini tazama, mimi mwenyewe ni mtu mwovu, na sijatii amri za Bwana na sheria zake kama vile ilivyonipasa.

3 Na ikawa kwamba miaka mia mbili, sabini na sita ilikuwa imepita, na tulikuwa na vipindi vingi vya amani; na tulikuwa na vipindi vingi vya vita na umwagaji wa damu. Ndiyo, na kwa ufupi, miaka mia mbili, themanini na miwili ilikuwa imepita, na nilikuwa nimeweka mabamba haya kulingana na aamri za baba zangu; na nikampatia mwana wangu Amaroni mabamba haya. Na ninakoma hapa.

4 Na sasa mimi, Amaroni, naandika vitu ambavyo ninaandika, ambavyo ni vichache, katika kitabu cha baba yangu.

5 Tazama, na ikawa kwamba miaka mia tatu na ishirini ilikuwa imepita, na sehemu kubwa ya Wanefi waovu aikaangamizwa.

6 Kwani Bwana hangeruhusu, baada ya kuwaongoza kutoka nchi ya Yerusalemu na kuwahifadhi wasianguke mikononi mwa maadui zao, ndiyo, hangekubali kwamba yale maneno ambayo aliwaambia baba zetu, yasithibitishwe, akisema kwamba: Msipotii amri zangu hamtafanikiwa nchini.

7 Kwa hivyo, Bwana aliwaadhibu kwa hukumu kuu; walakini, aliwaokoa wenye haki kwamba wasiangamie, lakini aliwakomboa kutoka mikononi mwa maadui zao.

8 Na ikawa kwamba nilimpatia Kemishi kaka yangu yale mabamba.

9 Sasa mimi, Kemishi, naandika vitu vichache, katika kitabu sawa na kaka yangu; kwani tazama, niliona ya mwisho aliyoandika, kwamba aliandika kwa mkono wake mwenyewe; na aliyaandika siku ile aliyonipatia. Na tunaweka maandishi katika njia hii, kwani ni kulingana na amri za baba zetu. Na ninakoma hapo.

10 Tazama, mimi, Abinadomu, ni mwana wa Kemishi. Tazama, ikawa kwamba mimi niliona vita vingi na ubishi kati ya watu wangu, Wanefi, na Walamani; na mimi, kwa upanga wangu mwenyewe, nimeondoa maisha ya Walamani wengi kwa ulinzi wa ndugu zangu.

11 Na tazama, maandishi ya watu hawa yameandikwa katika mabamba ambayo yamekuwa na wafalme, kulingana na vizazi; na sijui ufunuo wowote ambao haujaandikwa, wala unabii; kwa hivyo, yaliyoandikwa yametosha. Na ninakoma hapo.

12 Tazama, mimi ni Amaleki, mwana wa Abinadomu. Tazama, nitawazungumzia kuhusu Mosia, ambaye alitawazwa mfalme katika nchi ya Zarahemla; kwani tazama, yeye akiwa ameonywa na Bwana kwamba atoroke kutoka nchi ya aNefi, na wale wengi watakaotii sauti ya Bwana pia nao bwaondoke nchini na yeye, na waelekee nyikani—

13 Na ikawa kwamba alitenda kulingana na vile Bwana alivyomwamuru. Na walitoka nchi ile na kuelekea nyikani, wote ambao walisikiliza sauti ya Bwana; na waliongozwa kwa mahubiri mengi na unabii. Na wakaonywa kila mara kwa neno la Mungu; na waliongozwa kwa nguvu za mkono wake, huko nyikani hadi wakafika katika nchi inayoitwa nchi ya Zarahemla.

14 Na wakawavumbua watu, walioitwa watu wa aZarahemla. Sasa, kulikuwa na furaha kuu miongoni mwa watu wa Zarahemla; na pia Zarahemla alifurahi sana, kwa sababu Bwana alikuwa ametuma watu wa Mosia pamoja na bmabamba ya shaba nyeupe ambayo yalikuwa na maandishi ya Wayahudi.

15 Tazama, na ikawa kwamba Mosia alivumbua kuwa awatu wa Zarahemla waliondoka Yerusalemu wakati bZedekia, mfalme wa Yuda, alipohamishwa Babilonia utumwani.

16 Na wakasafiri nyikani, na wakavushwa kwa mkono wa Bwana katika yale maji makuu, hadi katika nchi ile ambayo Mosia aliwavumbua, na wakaishi katika nchi ile tangu tangu wakati ule na kuendelea.

17 Na ule wakati Mosia alipowavumbua, walikuwa wamekuwa wengi sana. Walakini, walikuwa wamekuwa na vita vingi na mabishano makubwa, na walikuwa wameanguka kwa upanga mara kwa mara; na lugha yao ilikuwa imechafuka; na hawakuwa wamebeba amaandishi yoyote; na walikana uwepo wa Muumba wao; na Mosia, wala watu wa Mosia, hawakuweza kuwaelewa.

18 Lakini ikawa kwamba Mosia akasababisha kwamba wafundishwe kwa lugha yake. Na ikawa kwamba baada ya kufundishwa lugha ya Mosia, Zarahemla akatoa nasaba ya baba zake, kulingana na ukumbuko wake; na yameandikwa, lakini sio katika mabamba haya.

19 Na ikawa kwamba watu wa Zarahemla, na watu wa Mosia, awaliungana pamoja; na bMosia akateuliwa kuwa mfalme wao.

20 Na ikawa kwamba katika siku za Mosia, aliletewa jiwe kubwa lililokuwa na maandishi juu yake; na aakatafsiri hayo maandishi kwa karama na nguvu za Mungu.

21 Na yalieleza historia ya mmoja aliyeitwa aKoriantumuri, na mauaji ya watu wake. Na Koriantumuri alivumbuliwa na watu wa Zarahemla; na akaishi nao kwa muda wa miezi tisa.

22 Na pia ilizungumza maneno machache kuhusu babu zake. Na wazazi wake wa kwanza walitoka katika ule amnara, wakati Bwana balipochanganya lugha za watu; na mapigo ya Bwana yaliwashukia kulingana na hukumu zake, ambazo ni za haki; na cmifupa yao ilitawanyika katika nchi za kaskazini.

23 Na tazama, mimi, Amaleki, nilizaliwa katika siku za Mosia; na nimeishi kuona kifo chake; na mwana wake, aBenjamini anatawala mahali pake.

24 Na tazama, nimeona, katika siku za mfalme Benjamini, vita vikali na umwagaji wa damu miongoni mwa Wanefi na Walamani. Lakini tazama, Wanefi walipata ushindi juu yao; ndiyo, hadi mfalme Benjamini akawafukuza kutoka nchi ya Zarahemla.

25 Na ikawa kwamba nilianza kuzeeka; na nikiwa sina uzao, na nikijua kwamba mfalme aBenjamini alikuwa mwenye haki kwa Bwana, kwa hivyo, bnitamkabidhi mabamba haya, nikiwasihi wanadamu wote wamjie Mungu, yule Mtakatifu wa Israeli, na kuamini katika unabii, na katika ufunuo, na kuhudumu kwa malaika, na katika kipawa cha kunena kwa ndimi, na katika kipawa cha kutafsiri ndimi, na katika vitu vyote vilivyo cvyema; kwani hakuna lolote jema lisilotokana na Bwana: na kwamba yale yaliyo maovu yanatokana na ibilisi.

26 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, natamani amje kwa Kristo, ambaye ni Mtakatifu wa Israeli, na mpokee wokovu wake, na nguvu za ukombozi wake. Ndiyo, njooni kwake, na bmumtolee nafsi zenu kama csadaka kwake, na muendelee katika dkufunga na kusali, na kuvumilia hadi mwisho; na kama vile Bwana anavyoishi mtaokolewa.

27 Na sasa nitazungumza machache kuhusu wengine walioelekea nyikani ili kurejea katika nchi ya Nefi; kwani kulikuwa na wengi waliotamani kumiliki nchi yao ya urithi.

28 Kwa hivyo, walielekea nyikani. Na kiongozi wao akiwa mtu mwenye nguvu na shujaa, na mtu mwenye shingo ngumu, kwa hivyo alisababisha ubishi miongoni mwao; na wote awakauawa, huko nyikani, isipokuwa hamsini, na wakarejea katika nchi ya Zarahemla.

29 Na ikawa kwamba waliwachukua wengine pia, na wakaelekea katika safari nyingine huko nyikani.

30 Na mimi, Amaleki, nilikuwa na kaka yangu, ambaye pia alienda pamoja nao; na tokea hapo sijajua lolote juu yao. Na sasa ninakaribia kulala katika kaburi langu; na amabamba haya yamejaa. Na ninamaliza mazungumzo yangu.