Maandiko Matakatifu
Mosia 24


Mlango wa 24

Amuloni anawatesa Alma na watu wake—Watauawa kama watasali—Bwana anaifanya mizigo yao iwe miepesi—Anawokomboa kutoka utumwani, na wanarajea Zarahemla. Karibia mwaka 145–120 K.K.

1 Na ikawa kwamba Amuloni alipendelewa na mfalme wa Walamani; kwa hivyo, mfalme wa Walamani aliwaruhusu yeye na ndugu zake wateuliwe kuwa walimu wa watu wake, ndiyo, hata juu ya watu waliokuwa katika nchi ya Shemloni, na katika nchi ya Shilomu, na katika nchi ya Amuloni.

2 Kwani Walamani walikuwa wamemiliki nchi hizi zote; kwa hivyo, mfalme wa Walamani alikuwa amewateua wafalme katika nchi hizi.

3 Na sasa jina la mfalme wa Walamani lilikuwa Lamani, akiitwa kwa jina la baba yake; na kwa hivyo aliitwa mfalme Lamani. Na alikuwa mfalme wa watu wengi.

4 Na aliwateua walimu wa ndugu za Amuloni katika kila nchi iliyomilikiwa na watu wake; na hivyo lugha ya Nefi ilianza kufundishwa miongoni mwa watu wote wa Walamani.

5 Na walikuwa watu ambao walipendana wao kwa wao, walakini hawakumjua Mungu; wala ndugu za Amuloni hawakuwafundisha chochote kuhusu Bwana Mungu wao, wala sheria ya Musa; wala hawakuwafundisha maneno ya Abinadi;

6 Lakini waliwafundisha kuhifadhi maandishi yao, na kwamba waandikiane wao kwa wao.

7 Na hivyo Walamani wakaanza kufanikiwa kwa utajiri, na wakaanza kufanya biashara wao kwa wao na kuwa na nguvu, na wakaanza kuwa wajanja na watu wenye hekima, kulingana na hekima ya ulimwengu, ndiyo, watu wenye ujanja mwingi, na kufurahishwa na kila aina ya uovu na uporaji, ila tu miongoni mwa ndugu zao.

8 Na sasa ikawa kwamba Amuloni alianza akuwanyanyasa Alma na ndugu zake, na kuanza kumtesa na kuwasababisha watoto wake kuwatesa watoto wao.

9 Kwani Amuloni alikuwa amemjua Alma, kwamba alikuwa ammoja wa makuhani wa mfalme, na kwamba ni yeye aliyeamini maneno ya Abinadi na kufukuzwa kutoka mbele ya mfalme, na kwa hivyo alikasirishwa na yeye; kwani alikuwa chini ya mfalme Lamani, na bado aliwanyanyasa, na kuwafanyisha kazi bngumu, na kuwawekea manyapara.

10 Na ikawa kwamba mateso yao yalikuwa makubwa hata kwamba wakaanza kumlilia Mungu.

11 Na Amuloni akawaamuru kwamba waache vilio vyao; na aliwawekea walinzi kuwalinda, kwamba yeyote atakayepatikana akimlingana Mungu auawe.

12 Na Alma na watu wake hawakupaza sauti zao kwa Bwana Mungu wao, lakini awalimfunulia mioyo yao; na alijua mawazo ya mioyo yao.

13 Na ikawa kwamba sauti ya Bwana iliwafikia katika mateso yao, ikisema: lnueni vichwa vyenu na msherehekee, kwani ninajua agano ambalo mlinifanyia; na nitaagana na watu wangu na kuwakomboa kutoka utumwani.

14 Na pia nitawapunguzia mizigo ambayo imewekwa mabegani yenu, hata kwamba hamtaisikia kamwe migongoni mwenu, hata mkiwa utumwani; na nitafanya haya ili muwe amashahidi wangu hapo baadaye, na kwamba mjue kwa hakika kwamba mimi, Bwana Mungu, huwatembelea watu wangu katika bmateso yao.

15 Na sasa ikawa kwamba mizigo ambayo ilikuwa wamewekewa Alma na ndugu zake ilipunguzwa; ndiyo, Bwana aliwapatia anguvu kwamba wabebe bmizigo yao kwa urahisi, na walinyenyekea kwa furaha na csubira kwa mapenzi ya Bwana.

16 Na ikawa kwamba imani yao na subira yao ilikuwa kuu sana hata kwamba sauti ya Bwana ikawajia tena, ikisema: Shangilieni, kwani hapo kesho nitawakomboa kutoka utumwani.

17 Na akamwambia Alma: Wewe utaenda mbele ya hawa watu, na nitaenda nawe na kuwakomboa watu hawa kutoka autumwani.

18 Na sasa ikawa kwamba Alma na watu wake walikusanya mifugo yao pamoja usiku, na pia nafaka yao; ndiyo, hata usiku wote walikusanya mifugo yao pamoja.

19 Na asubuhi Bwana alisababisha ausingizi mzito uwapate Walamani, ndiyo, na manyapara wao wote walilala usingizi mzito.

20 Na Alma na watu wake walienda nyikani; na walipokuwa wamesafiri mchana wote walipiga mahema zao katika bonde, na wakaliita lile bonde Alma, kwa sababu aliwaongoza njiani wakielekea nyikani.

21 Ndiyo, na katika bonde la Alma walimpigia ashukrani wao kwa Mungu kwa sababu amekuwa mwenye huruma kwao, na kupunguza mizigo yao, na kuwakomboa kutoka utumwani, kwani walikuwa utumwani, na hakuna yeyote ambaye angewakomboa ila tu Bwana Mungu wao.

22 Na wakamshukuru Mungu, ndiyo, waume wao wote na wake zao wote na watoto wao wote ambao waliweza kuzungumza walipaza sauti zao na kumshukuru Mungu wao.

23 Na sasa Bwana akamwambia Alma: Jiharakishe wewe na utoe watu hawa kutoka nchi hii, kwani Walamani wameamka na wanakufuata; kwa hivyo jiondoe kutoka nchi hii, na nitawazuia Walamani katika bonde hili ili wasiwafuate watu hawa.

24 Na ikawa kwamba waliondoka bondeni, na kuelekea nyikani.

25 Na baada ya kuwa nyikani kwa siku kumi na mbili walifika katika nchi ya Zarahemla; na mfalme Mosia aliwapokea kwa shangwe.