Maandiko Matakatifu
Mosia 21


Mlango wa 21

Watu wa Limhi wanashambuliwa na kushindwa na Walamani—Watu wa Limhi wanakutana na Amoni na kubadilishwa—Wanamwambia Amoni kuhusu yale mabamba ishirini na nne ya Kiyaredi. Karibia mwaka 122–121 K.K.

1 Na ikawa kwamba Limhi na watu wake walirejea katika mji wa Nefi, na wakaanza kuishi tena kwa amani katika nchi.

2 Na ikawa kwamba baada ya siku nyingi Walamani walianza tena kuwachokoza wakasirike Wanefi, na wakaanza kusogea karibu na mipaka iliyozingira nchi.

3 Sasa hawakuthubutu kuwaua, kwa sababu ya kile kiapo ambacho mfalme wao alikuwa amemuapia Limhi; walakini waliwacharaza makofi kwenye amashavu, na kuwa na mamlaka juu yao; na kuwabebesha bmizigo mizito kwenye migongo yao, na kuwakimbiza kama vile wanavyomfanyia punda bubu—

4 Ndiyo, haya yote yalifanywa ili neno la Bwana litimizwe.

5 Na sasa mateso ya Wanefi yalikuwa ni makuu, na hapakuwa na njia yoyote ya kujikomboa kutoka mikononi mwao, kwani Walamani waliwazingira kwa kila upande.

6 Na ikawa kwamba watu walianza kumnungʼunikia mfalme kwa sababu ya mateso yao; na wakaanza kutamani kupigana nao. Na walimsumbua mfalme kwa malalamiko yao; kwa hivyo akawaruhusu wafanye kulingana na tamaa yao.

7 Na wakakusanyika pamoja tena, na kuvaa silaha zao, na kuwaendea Walamani ili wawafukuze kutoka nchi yao.

8 Na ikawa kwamba Walamani waliwapiga, na kuwasukuma nyuma, na kuwaua wengi wao.

9 Na sasa kulikuwa na amaombolezo makuu na kilio miongoni mwa watu wa Limhi, mjane akiomboleza mume wake, mwana na binti wakiomboleza baba yao, na kaka kwa ndugu zao.

10 Sasa kulikuwa na wajane wengi nchini, na walilia sana siku kwa siku, kwani woga mkuu wa Walamani uliwaingia.

11 Na ikawa kwamba vilio vyao viliwachochea wale watu waliobaki wa Limhi kuwakasirikia Walamani; na wakaenda vitani tena, lakini walisukumwa nyuma tena, na wakapata maafa makubwa.

12 Ndiyo, walienda tena mara ya tatu, na wakateseka kama hapo awali; na wale ambao hawakuuawa walirejea tena katika nchi ya Nefi.

13 Na wakanyenyekea mpaka mavumbini, na kujitoa kwa nira ya utumwa, na kukubali kupigwa, na kukimbizwa hapa na pale, na kulemeshwa, kulingana na matakwa ya maadui wao.

14 Na awalinyenyekea chini kabisa na hata kuwa chini ya unyenyekevu; na walimlilia Mungu sana; ndiyo, hata siku yote walimlilia Mungu wao kwamba awakomboe kutokana na mateso yao.

15 Na sasa Bwana alikuwa amzito wa kusikia kilio chao kwa sababu ya maovu yao; hata hivyo Bwana alisikia vilio vyao, na akaanza kulainisha mioyo ya Walamani kiasi kwamba wakaanza kupunguza mizigo yao; walakini Bwana hakuonelea vyema kuwakomboa kutoka utumwani.

16 Na ikawa kwamba walianza kufanikiwa nchini kidogo kidogo, na wakaanza kupanda nafaka kwa wingi, na mifugo, na wanyama, kwamba hawakuteseka kwa njaa.

17 Sasa kulikuwa na wanawake wengi, zaidi ya wanaume; kwa hivyo mfalme Limhi akaamuru kwamba kila mwanaume aatoe ili bwajane na watoto wao wapate kusaidiwa, na ili wasiangamie kwa njaa; na walitenda haya kwa sababu ya wingi wa hao waliouwawa.

18 Sasa watu wa Limhi waliishi kwa kikundi kama ilivyowezekana, na kulinda nafaka yao na mifugo yao;

19 Na mfalme mwenyewe alihofia maisha yake nje ya ukuta wa mji, isipokuwa awe na walinzi wake na yeye, akiogopa kwamba ingewezekana aanguke mikononi mwa Walamani.

20 Na akasababisha watu wake washike zamu kila mahali nchini, ili ikiwezekana wawakamate makuhani ambao walikuwa wametorokea nyikani, ambao walikuwa wamewachukua amabinti za Walamani, na ambao walikuwa wamesababisha maangamizi makuu kuwapata.

21 Kwani walitamani kuwakamata na kuwaadhibu; kwa sababu walikuwa wameingia katika nchi ya Nefi wakati wa usiku, na kuiba nafaka yao na vitu vyao vingi vyenye thamani; kwa hivyo walijificha na kuwangoja.

22 Na ikawa kwamba hakukuwa na ghasia yoyote miongoni mwa Walamani na watu wa Limhi, hadi ule wakati ambao aAmoni na ndugu zake walipowasili katika nchi.

23 Na mfalme akiwa nje ya lango la mji na walinzi wake, aliwaona Amoni na ndugu zake; na akidhani kwamba wao ni makuhani wa Nuhu, kwa hivyo aliamrisha kwamba washikwe, na kufungwa, na kuwekwa agerezani. Na kama wangekuwa makuhani wa Nuhu, angeamuru wauawe.

24 Lakini alipofahamu kwamba sio wao, walakini walikuwa ndugu zake, waliotoka nchi ya Zarahemla, alijazwa na shangwe kuu.

25 Sasa mfalme Limhi alikuwa ametuma, kikundi akidogo cha watu bkutafuta nchi ya Zarahemla, kabla ya kuwasili kwa Amoni; lakini hawakuipata, na walipotea huko nyikani.

26 Walakini, walipata nchi ambamo watu walikuwa wameishi; ndiyo, nchi ambayo ilijaa amifupa iliyokauka; ndiyo, nchi ambayo watu walikuwa wameishi na ambao walikuwa wameangamizwa; na wao, wakidhani kuwa ni nchi ya Zarahemla, walirejea katika nchi ya Nefi, wakiwa wamewasili mipakani mwa nchi siku chache kabla ya kufika kwa Amoni.

27 Na walileta maandishi, hata maandishi ya watu wale ambao walipata mifupa yao; na yalikuwa yamechorwa kwenye mabamba ya chuma.

28 Na sasa Limhi alijawa shangwe tena alipoambiwa kwa kinywa cha Amoni kwamba mfalme Mosia alikuwa na akarama kutoka kwa Mungu, ambayo ingemwezesha kutafsiri michoro kama ile; ndiyo, na hata Amoni pia alifurahi.

29 Walakini Amoni na ndugu zake walijawa na huzuni kwa sababu ndugu zao wengi walikuwa wameuawa;

30 Na pia kwamba mfalme Nuhu na makuhani wake walikuwa wamewafanya watu kumtendea Mungu dhambi nyingi na maovu; na pia waliomboleza akifo cha Abinadi; na pia bkuondoka kwa Alma na watu walioenda na yeye, ambao walikuwa wameanzisha kanisa la Mungu kwa nguvu na uwezo wa Mungu, na kwa imani katika yale maneno yaliozungumzwa na Abinadi.

31 Ndiyo, waliomboleza kuondoka kwao, kwani hawakujua walikotorokea. Sasa wangeungana nao bila kusita, kwani wao wenyewe walikuwa wameingia kwenye agano na Mungu kwamba watamtumikia na kutii amri zake.

32 Na sasa tangu kuwasili kwa Amoni, mfalme Limhi pia alikuwa ameingia kwenye agano na Mungu, na pia watu wake wengi, kumtumikia na kutii amri zake.

33 Na ikawa kwamba mfalme Limhi na watu wake wengi walitamani kubatizwa; lakini hapakuwa na yeyote katika nchi ile aliyekuwa na amamlaka kutoka kwa Mungu. Na Amoni alikataa kufanya kitu hiki, akijidhania kwamba yeye ni mtumishi asiyestahili.

34 Kwa hivyo wakati ule hawakujipanga pamoja kama kanisa, wakimsubiri Roho wa Bwana. Sasa walitamani kuwa kama Alma na ndugu zake, ambao walikuwa wametorokea nyikani.

35 Walitamani kubatizwa kama ushahidi na ushuhuda kwamba wako tayari kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote; walakini waliongeza wakati; na maelezo ya ubatizo wao ayatatolewa hapo baadaye.

36 Na sasa mawazo yote ya Amoni na watu wake, na mfalme Limhi na watu wake, yalikuwa ni jinsi ya kujikomboa kutoka mikono ya Walamani na kutoka utumwa.