Maandiko Matakatifu
Mosia 13


Mlango wa 13

Abinadi analindwa kwa nguvu takatifu—Anafundisha Amri Kumi—Wokovu hauji kwa sheria ya Musa pekee—Mungu Mwenyewe atafanya upatanisho na awakomboe watu Wake. Karibia mwaka 148 K.K.

1 Na sasa mfalme alipoyasikia maneno haya, aliwaambia makuhani wake: Mwondolee huyu mtu mbali, na mwuueni; kwani tutafanya nini na yeye, kwani ana kichaa.

2 Na wakasimama na kumsogelea na kujaribu kumkamata; lakini aliwazuia, na akawaambia:

3 Msiniguse, kwani Mungu atawapiga mkinishika, kwani sijatoa ujumbe ambao Bwana alinituma kuutoa; wala sijawaambia yale ambayo amliniuliza niwaambie; kwa hivyo, Mungu hatakubali kwamba niangamizwe sasa.

4 Lakini lazima nitimize amri ambazo Mungu ameniamuru; na kwa sababu nimewaambia ukweli mnanikasirikia. Na tena, kwa sababu nimezungumza neno la Mungu mmenihukumu kuwa mimi nina kichaa.

5 Na sasa ikawa kwamba baada ya Abinadi kuzungumza maneno haya watu wa mfalme Nuhu hawakumkamata tena, kwani Roho wa Bwana alikuwa na yeye; na uso wake aulimetameta kwa mngʼaro mkuu, hata vile uso wa Musa ulivyongʼara katika mlima wa Sinai, alipokuwa akizungumza na Bwana.

6 Na alizungumza kwa auwezo na mamlaka kutoka kwa Mungu; na akaendelea na maneno yake, akisema:

7 Mnaona kwamba hamna uwezo wa kuniua, kwa hivyo namaliza ujumbe wangu. Ndiyo, na ninaona kwamba ainawakera mioyoni yenu kwa sababu nimewaambia ukweli kuhusu maovu yenu.

8 Ndiyo, na maneno yangu yanawajaza na mshangao na bumbuwazi, na hasira.

9 Lakini namaliza ujumbe wangu; na kisha haijalishi ni wapi nitakapoenda, ikiwa kama nitaokolewa.

10 Lakini nawaambia haya, yale mtakayonifanyia, baada ya haya, yatakuwa ni kama amfano au kivuli cha vitu vitakavyokuja.

11 Na sasa nitawasomea aamri za Mungu zilizosalia, kwani nahisi kwamba hazijaandikwa mioyoni yenu; nahisi kwamba mmesoma na kufundisha uovu kwa muda mrefu maishani mwenu.

12 Na sasa, mnakumbuka kwamba niliwaambia: Hamtajitengenezea sanamu ya kuchonga, au mfano wa vitu vyovyote vilivyo juu mbinguni, au vilivyo chini ardhini, au vilivyo majini chini ya ardhi.

13 Na tena: Hamtaviinamia, wala kuvitumikia; kwani mimi Bwana Mungu wako ni Mungu wa hamasa, niteremshiaye watoto maovu ya babu zao, kwa kizazi cha tatu na cha nne kwa wale wanaonichukia;

14 Na kuonyesha rehema kwa maelfu ya wale wanaonipenda na kutii amri zangu.

15 Usichukue jina la Bwana Mungu wako bure; kwani Bwana hatamfikiria kama asiye na hatia yule anayechukua jina lake bure.

16 Kumbuka siku ya asabato, kuiweka takatifu.

17 Utafanya kazi kwa siku sita, na kufanya kazi yako yote.

18 Lakini siku ya saba, sabato ya Bwana Mungu wako, usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti wako, wala mtumishi wako wa kiume, wala mjakazi wako, wala mifugo yako, wala mgeni wako anayeishi nawe;

19 Kwani kwa siku asita Bwana aliumba mbingu na dunia, na bahari, na vyote vilivyo ndani yake; kwa hivyo Bwana aliibariki siku ya sabato, na kuitakasa.

20 aHeshimu baba yako na mama yako, ili maisha yako yawe marefu katika ya nchi ambayo Bwana Mungu wako amekupatia.

21 aUsiue.

22 aUsizini. bUsiibe.

23 Usitoe aushahidi wa uwongo dhidi ya jirani yako.

24 aUsitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mfanyi kazi wake, wala mjakazi wake, wala dume wake, wala punda wake, wala chochote cha jirani yako.

25 Na ikawa kwamba baada ya Abinadi kumaliza kusema maneno haya kwamba akawaambia: Mmewafundisha watu hawa kutii vitu hivi vyote ili watii amri hizi?

26 Nawaambia, La; kwani kama mngekuwa mmefanya hivyo, Bwana hangenisababisha nije na nitoe unabii wa uovu kuhusu watu hawa.

27 Na sasa mmesema kwamba wokovu huja kwa asheria ya Musa. Nawaambia kwamba ni muhimu mtii sheria ya Musa sasa; lakini nawaambia, kwamba wakati utafika ambapo bhaitakuwa muhimu kutii sheria ya Musa.

28 Na juu ya hayo, nawaambia, kwamba awokovu hauji kwa bsheria pekee; na kama sio kwa sababu ya cupatanisho, ambao Mungu atautoa kwa sababu ya dhambi na uovu wa watu wake, kwamba lazima waangamie, ingawa sheria ya Musa ipo.

29 Na sasa nawaambia kwamba ilikuwa lazima kwamba wana wa Israeli wapewe sheria, ndiyo, sheria iliyo angumu, kwani walikuwa watu wenye shingo ngumu, walio na bharaka ya kutenda maovu, na wavivu kwa kumkumbuka Bwana Mungu wao;

30 Kwa hivyo kulikuwa na asheria ambayo walipewa, ndiyo, sheria ya sherehe na bmasharti, sheria ambayo walitakiwa ckuitii siku kwa siku, ili kuwakumbusha Mungu na jukumu lao kwake.

31 Lakini tazama, nawaambia, kwamba vitu hivi vyote vilikuwa ni amfano wa vile vitakavyokuja.

32 Na sasa, je, walifahamu sheria? Nawaambia, La, wote hawakufahamu ile sheria; na hii ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; kwani hawakufahamu kwamba hakuna yeyote angeokolewa aila tu kwa ukombozi wa Mungu.

33 Kwani tazama, si Musa aliwatolea unabii kuhusu kuja kwa Masiya, na kwamba Mungu atawakomboa watu wake? Ndiyo, na hata manabii awote ambao wametoa unabii tangu mwanzo wa ulimwengu—Je, hawajanena mengi au machache kuhusu vitu hivi?

34 Je, hawajasema kwamba aMungu mwenyewe atashuka chini miongoni mwa watoto wa watu, na ajivike hali ya mwanadamu, na atembee usoni mwa dunia kwa uwezo mkuu?

35 Ndiyo, na je, hawakusema pia kwamba atawezesha aufufuo wa wafu, na kwamba yeye, mwenyewe, atanyanyaswa na kusumbuliwa?