Maandiko
Moroni 7


Mlango wa 7

Karibisho linapewa kuingia kwenye makao ya Bwana—Ombeni na nia ya kweli—Roho wa Kristo huwezesha watu kujua mema na maovu—Shetani anawashawishi watu wamkane Kristo na wafanye uovu—Manabii wanadhihirisha kuja kwa Kristo—Kwa imani, miujiza hufanyika na malaika wanahudumu—Watu wanapaswa kutumaini uzima wa milele na kuambatana kwenye hisani. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Na sasa mimi, Moroni, naandika machache ya maneno ya baba yangu Mormoni, ambayo alisema kuhusu aimani, tumaini, na hisani; kwani hii ndiyo njia aliyozungumza kwa watu, wakati alipowafundisha katika sinagogi ambayo walikuwa wamejenga kama mahali pa kuabudu.

2 Na sasa mimi, Mormoni, nazumgumza kwenu ndugu zangu wapendwa; na ni kwa neema ya Mungu Baba, na Bwana wetu Yesu Kristo, na mapenzi yake matakatifu, kwa sababu ya karama yake akuniita, kwamba nimekubaliwa kuzungumza kwenu wakati huu.

3 Kwa hivyo, ningewazungumzia wale ambao ni wa kanisa, ambao ni wafuasi wa imani ya Kristo, ambao wamepata tumaini la kutosha ambalo kwalo mnaweza kuingia kwenye amakao ya Bwana, kutoka wakati huu kwenda mbele mpaka mtakapopumzika na yeye mbinguni.

4 Na sasa ndugu zangu, nahukumu vitu hivi kwenu kwa sababu ya amatembezi yenu matulivu na watoto wa watu.

5 Kwani nakumbuka neno la Mungu ambalo linasema kwa matunda yao amtawatambua; kwani kama matunda yao ni mema, basi ni wema pia.

6 Kwani tazama, Mungu amesema mtu akiwa amwovu hawezi kufanya yale ambayo ni mema; kwani ikiwa atatoa karama, au bkuomba kwa Mungu, isipokuwa aifanye kwa kusudi jema haimfaidii chochote.

7 Kwani tazama, haihesabiwi kwake kwa haki.

8 Kwani tazama, ikiwa mtu amwovu anatoa zawadi, huifanya bbila kupenda; kwa hivyo inahesabiwa kwake sawa kama angeiweka ile zawadi; kwa hivyo anadhaniwa mwovu mbele ya Mungu.

9 Na kadhalika huhesibiwa pia uovu kwa mtu, ikiwa ataomba bila ania kamili ya moyo; ndiyo, na haimfaidii chochote, kwani Mungu hampokei yeyote wa aina hii.

10 Kwa hivyo, mtu akiwa mwovu hawezi kufanya kile ambacho ni chema; wala hawezi kutoa karama nzuri.

11 Kwani tazama, achimbuko chungu haliwezi kutoa maji mazuri; wala chimbuko zuri haliwezi kutoa maji chungu; kwa hivyo, mtu akiwa mtumishi wa ibilisi hawezi akamfuata Kristo; na akiwa banamfuata Kristo hapo hawezi akawa mtumishi wa ibilisi.

12 Kwa hivyo, vitu vyote vilivyo avizuri vinatoka kwa Mungu; na kile kilicho bkiovu hutoka kwa ibilisi; kwani ibilisi ni adui wa Mungu, na hupigana dhidi yake siku zote, na hukaribisha na hushawishi kufanya cdhambi, na kufanya kile kilicho kiovu siku zote.

13 Lakini tazama, kile kilicho cha Mungu hukaribisha na hushawishi kufanya mema siku zote; kwa hivyo, kila kitu kinachokaribisha na akushawishi kufanya mema, na kumpenda Mungu, na kumtumikia, bkinaongozwa na Mungu.

14 Kwa hivyo, muwe waangalifu, ndugu zangu wapendwa, kwamba msione kile ambacho ni akiovu kuwa cha Mungu, au kile ambacho ni kizuri na cha Mungu kuwa cha ibilisi.

15 Kwani tazama, ndugu zangu, mmepewa uhuru akuhukumu, kwamba mjue mema na maovu; na njia ya kuhukumu ni wazi, kwamba mjue na ufahamu kamili, kama mwangaza wa mchana kutoka kwa giza la usiku.

16 Kwani tazama, aRoho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili bajue mema na maovu; kwa hivyo, ninawaonyesha njia ya kuhukumu; kwani kila kitu kinachokaribisha kufanya mema, na kushawishi kuamini katika Kristo, kinasababishwa na uwezo na thawabu ya Kristo; kwa hivyo mngejua na ufahamu kamili kwamba ni cha Mungu.

17 Lakini kitu chochote ambacho hushawishi watu kufanya amaovu, na kutoamini katika Kristo, na kumkana, na kutomtumikia Mungu, hapo mtajua na ufahamu kamili kwamba ni cha ibilisi; kwani kwa njia hii ndiyo ibilisi hufanya kazi, kwani hamshawishi mtu yeyote kufanya mema, la, sio mmoja; wala malaika wake; wala wale ambao hujiweka chini yake.

18 Na sasa, ndugu zangu, nikiona kwamba mnajua nuru ambayo kwake mnaweza kuhukumu, nuru ambayo ni anuru ya Kristo, mhakikishe kwamba hamhukumu kwa makosa; kwani bhukumu ile mnayohukumu nayo ndiyo mtakayohukumiwa.

19 Kwa hivyo, ninawasihi ninyi, ndugu, kwamba mtafute kwa bidii katika anuru ya Kristo kwamba mngejua mema na maovu; na ikiwa utashikilia kila kitu kizuri, na usilaumu, hapo utakuwa bila shaka bmtoto wa Kristo.

20 Na sasa, ndugu zangu, inawezekanaje kwamba mshikilie kila kitu kizuri?

21 Na sasa naja kwa ile imani, ambayo nilisema nitaizungumzia; na nitawaambia njia ambayo kwake mnaweza kushikilia kwa kila kitu kizuri.

22 Kwani tazama, Mungu aakijua vitu vyote, akiwa amekuwepo kutoka milele hadi milele, tazama, alimtuma bmalaika kuhudumu kwa watoto wa watu, kuwajulisha kuhusu kuja kwa Kristo; na katika Kristo kutatokea kila kitu kizuri.

23 Na Mungu pia aliwatangazia manabii, kwa mdomo wake mwenyewe, kwamba Kristo sharti aje.

24 Na tazama, kulikuwa na njia tofauti ambazo kwake alijulisha vitu kwa watoto wa watu, ambavyo vilikuwa vyema; na vitu vyote ambavyo ni vyema hutoka kwa Kristo; la sivyo watu wangebaki kwenye hali ya akuanguka, na hakuna kitu chochote kizuri ambacho kingewajia.

25 Na kwa hivyo, kwa huduma ya amalaika, na kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, watu walianza kutenda imani katika Kristo; na hivyo kwa imani, walishikilia kila kitu kizuri; na hivi ndivyo ilivyokuwa mpaka kuja kwa Kristo.

26 Na baada ya yeye kuja watu pia waliokolewa kwa imani katika jina lake; na kwa kupitia kwa imani, wakawa wana wa Mungu. Na kwa kweli kadiri Kristo aishivyo alisema maneno haya kwa babu zetu, akisema: Kitu achochote mtakachomwuliza Baba katika jina langu, ambacho ni kizuri, kwa imani mkiamini kwamba mtapata, tazama, mtakipokea.

27 Kwa hivyo, ndugu zangu wapendwa, je, amiujiza imekoma kwa sababu Kristo amepanda mbinguni, na ameketi mkono wa kulia wa Mungu, bkudai kutoka kwa Baba haki zake za huruma ambazo anazo juu ya watoto wa watu?

28 Kwani amejibu mwisho wa sheria, na hudai wale wote ambao wana imani ndani yake; na wale ambao wana imani ndani yake awatajishikilia kwa kila kitu kizuri; kwa hivyo bhuzungumza akipendelea watoto wa watu; na huishi mbinguni milele.

29 Na kwa sababu amefanya hivi, ndugu zangu wapendwa, je, miujiza imekoma? Tazama ninawaambia, La; wala malaika hawajakoma kuwahudumia watoto wa watu.

30 Kwani tazama, wako chini yake, kuhudumu kulingana na neno la amri yake, wakijidhihirisha kwa wale walio na imani ya nguvu na akili imara katika kila kitu cha uchamungu.

31 Na kazi ya huduma yao ni kuita watu katika toba, na kutimiza na kufanya kazi ya agano la Baba, ambalo amefanya kwa watoto wa watu, kutayarisha njia miongoni mwa watoto wa watu, kwa kutangaza neno la Kristo kwa vyombo viteule vya Bwana, kwamba wangekuwa na ushahidi kumhusu.

32 Na kwa kufanya hivyo, Bwana Mungu hutayarisha njia kwamba watu wengine wangekuwa na aimani katika Kristo, kwamba Roho Mtakatifu angekuwa na mahali katika mioyo yao, kulingana na uwezo alio nao; na kwa njia hii ndiyo Baba hutimiza, maagano ambayo amefanya kwa watoto wa watu.

33 Na Kristo amesema: aIkiwa mtakuwa na imani ndani yangu mtakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote ambacho ni cha bkufaa kwangu.

34 Na amesema: aTubuni enyi miisho ya dunia, na mje kwangu, na mbatizwe katika jina langu, na muwe na imani ndani yangu, ili muokolewe.

35 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, ikiwa hivi ndivyo itakuwa kwamba vitu hivi ni kweli ambavyo nimewazungumzia, na Mungu atawaonyesha, kwa auwezo na fahari kuu katika bsiku ya mwisho, kwamba ni kweli, na ikiwa ni kweli, je, wakati wa miujiza umekoma?

36 Au malaika wamekoma kuonekana kwa watoto wa watu? Au aamesimamisha uwezo wa Roho Mtakatifu kutoka kwao? Au atasimamisha, kadiri muda utakapokuwepo au dunia itakapokuwepo, au kutakuwa na mtu mmoja juu ya uso wake kuokolewa?

37 Tazama ninawaambia, La; kwani ni kwa imani kwamba amiujiza hufanyika; na ni kwa imani kwamba malaika huonekana na kuhudumia watu; kwa hivyo, kama vitu hivi vimekoma msiba uwe kwa watoto wa watu, kwani ni kwa sababu ya bkutoamini, na yote ni bure.

38 Kwani hakuna atakayeokoka, kulingana na maneno ya Kristo, isipokuwa awe na imani katika jina lake; kwani, ikiwa hivi vitu vimekoma, basi imani imekoma pia; na kutisha ni hali ya mtu, kwani ni kama hakujakuwepo na ukombozi uliofanywa.

39 Lakini tazama, ndugu zangu wapendwa, ninaweza kuona vitu vyema zaidi kwenu, kwani ninaona kwamba mna imani katika Kristo kwa sababu ya uvumilivu wenu; kwani kama hamna imani ndani yake ahamfai kuhesabiwa miongoni mwa watu wa kanisa lake.

40 Na tena, ndugu zangu wapendwa, ninataka kuwazungumzia kuhusu atumaini. Inawezekanaje kwamba mtafikia imani, isipokuwa muwe na tumaini?

41 Na ni kitu gani amtakachotumainia? Tazama nawaambia kwamba mtakuwa na btumaini kupitia upatanisho wa Kristo na uwezo wa kufufuka kwake, kuinuliwa kwa cmaisha ya milele, na hii kwa sababu ya imani yenu kwake kulingana na ile ahadi.

42 Kwa hivyo, ikiwa mtu ana aimani blazima ahitaji kuwa na tumaini; kwani bila imani hakuwezi kuwepo na tumaini lolote.

43 Na tena, tazama ninawaambia kwamba hawezi kuwa na imani na tumaini, isipokuwa awe amnyenyekevu, na mpole katika moyo.

44 Ikiwa hivyo, aimani na tumaini lake ni bure, kwani hakuna yeyote anayekubaliwa mbele ya Mungu, isipokuwa yule aliye myenyekevu na mpole katika moyo; na mtu akiwa myenyekevu na mpole katika moyo, na bkukiri kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwamba Yesu ni Kristo, lazima awe na ahisani; kwani kama hana hisani yeye si kitu; kwa hivyo lazima awe na hisani.

45 Na ahisani huvumilia, na ni karimu, na haina bwivu, na haijivuni, haitafuti mambo yake, haifutuki kwa upesi, haifikirii mabaya, na haifurahii uovu lakini hufurahi katika ukweli, huvumilia vitu vyote, huamini vitu vyote, hutumaini vitu vyote, hustahamili vitu vyote.

46 Kwa hivyo, ndugu zangu wapendwa, kama hamna hisani, ninyi si kitu, kwani hisani haikosi kufaulu kamwe. Kwa hivyo, ambatana na hisani, ambayo ni kubwa kuliko yote, kwani vitu vyote lazima vishindwe—

47 Lakini ahisani ni bupendo msafi wa Kristo, na inavumilia milele; na yeyote atakayepatikana nayo katika siku ya mwisho, itakuwa vyema kwake.

48 Kwa hivyo, ndugu zangu wapendwa, aombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba mjazwe na upendo huu, ambao ametoa kwa wote ambao ni bwafuasi wa kweli wa Mwana wake, Yesu Kristo; ili muwe wana wa Mungu; kwamba wakati atakapoonekana ctutakuwa kama yeye, kwani tutamwona vile alivyo; ili tuwe na tumaini hili; ili dtutakaswe hata vile alivyo mtakatifu. Amina.