Maandiko
Moroni 10
iliyopita

Mlango wa 10

Ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni huja kwa uwezo wa Roho Mtakatifu—Vipawa vya Roho hutolewa kwa walio waaminifu—Karama za kiroho kila mara huambatana na imani—Maneno ya Moroni yanazungumza kutoka mavumbini—Njooni kwa Kristo, mkamilishwe ndani Yake, na mtakase nafsi zenu. Karibia mwaka 421 B.K.

1 Sasa mimi, Moroni, naandika machache ambayo naona ni ya kufaa; na ninaandika kwa ndugu zangu, aWalamani; na ningependa kwamba wajue kwamba zaidi ya miaka mia nne na ishirini imepita tangu ishara ilipotolewa ya kuja kwa Kristo.

2 Na ninaweka amuhuri maandishi haya, baada ya kuzungumza maneno machache kwa njia ya ushauri kwenu.

3 Tazama, ningewashauri kwamba mtakaposoma vitu hivi, ikiwa itakuwa hekima katika Mungu kwamba myasome, kwamba mngekumbuka jinsi vile Bwana amekuwa na huruma kwa watoto wa watu, kutokea kuumbwa kwa Adamu hadi chini mpaka wakati ambapo mtapokea vitu hivi, na akuitafakari katika bmioyo yenu.

4 Na mtakapopokea vitu hivi, ningewashauri kwamba amngemwuliza Mungu, Baba wa Milele, katika jina la Kristo, ikiwa vitu hivi bsi vya kweli; na ikiwa mtauliza na cmoyo wa kweli, na dkusudi halisi, mkiwa na eimani katika Kristo, fatawaonyesha gukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

5 Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu amtajua bukweli wa vitu vyote.

6 Na kitu chochote kilicho kizuri ni haki na kweli; kwa hivyo, hakuna chochote ambacho ni kizuri ambacho humkana Kristo, lakini hukubali kwamba yuko.

7 Na mngejua kwamba yuko, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu; kwa hivyo ningewashauri kwamba msikatae uwezo wa Mungu; kwani hufanya kazi kwa uwezo, akulingana na imani ya binadamu, sawa leo na kesho, na milele.

8 Na tena, ninawashauri, ndugu zangu, kwamba msikatae akarama za Mungu, kwani ni nyingi; na zinatoka kwa yule yule Mungu. Na kuna njia btofauti ambazo karama hizi hutolewa; lakini ni yule yule Mungu azitendaye kazi zote katika wote; na hupewa kwa ufunuo wa Roho wa Mungu kwa watu, kuwasaidia.

9 Kwani tazama, akwa mmoja inatolewa kwa Roho wa Mungu, kwamba bafundishe neno la hekima;

10 Na kwa mwingine, kwamba afundishe neno la elimu na Roho yule yule;

11 Na kwa mwingine, aimani kubwa sana; na kwa mwingine, karama za bkuponya na Roho yule yule;

12 Na tena, kwa mwingine, kwamba aweze kufanya amiujiza mikuu;

13 Na tena, kwa mwingine, kwamba aweze kutoa unabii kuhusu vitu vyote;

14 Na tena, kwa mwingine; kuona kwa malaika na kutumikia roho;

15 Na tena, kwa mwingine, lugha za aina zote;

16 Na tena, kwa mwingine, kutafsiri kwa lugha na andimi za aina tofauti.

17 Na karama hizi zote huja kwa Roho ya Kristo; na huja kwa kila mtu moja kwa moja, kulingana na vile anavyotaka.

18 Na ningewashauri ninyi, ndugu zangu wapendwa, kwamba mkumbuke kwamba akila karama nzuri hutoka kwa Kristo.

19 Na ningewashauri ninyi, ndugu zangu wapendwa, kwamba mkumbuke kwamba yeye ndiye ayule yule jana, leo, na milele, na kwamba karama hizi zote ambazo nimezungumzia, ambazo ni za kiroho, hazitatolewa mbali, kadiri dunia itakavyokuwepo, kulingana tu na bkutoamini kwa watoto wa watu.

20 Kwa hivyo, lazima kuwe na aimani; na ikiwa kutakuwa na imani lazima kuwe pia na tumaini; na ikiwa kutakuwa na tumaini lazima kuwe pia na hisani.

21 Na msipokuwa na ahisani hamwezi kwa vyovyote kuokolewa katika ufalme wa Mungu; wala hamwezi kuokolewa katika ufalme wa Mungu kama hamna imani; wala hamwezi ikiwa hamna tumaini.

22 Na kama hamna tumaini lazima iwe ni kwa kukata tamaa; na kukata tamaa huja kwa sababu ya uovu.

23 Na Kristo kwa kweli alisema kwa babu zetu: aMkiwa na imani mnaweza kufanya vitu vyote ambavyo vinatakikana kwangu.

24 Na sasa ninazungumzia watu wote waliomo duniani—kwamba ikiwa siku itakuja kwamba uwezo na karama za Mungu zitaondolewa kutoka miongoni mwenu, itakuwa ni kwa asababu ya bkutoamini.

25 Na ole kwa watoto wa watu ikiwa itakuwa hivyo; kwani hakutakuwa ayeyote ambaye hufanya mema miongoni mwenu, la hata mmoja. Kwani ikiwa kuna mmoja miongoni mwenu ambaye hufanya mema, atafanya kwa uwezo na karama za Mungu.

26 Na ole kwa hao ambao watatoa vitu hivi na kufa, kwani awanakufa katika bdhambi zao, na hawawezi kuokolewa katika ufalme wa Mungu; na ninaizungumzia kulingana na maneno ya Kristo; na sidanganyi.

27 Na ninawashauri mkumbuke vitu hivi; kwani wakati unafika haraka kwamba mtajua kwamba sidanganyi, kwani mtaniona katika kiti cha hukumu cha Mungu; na Bwana Mungu atasema kwenu: Je, si mimi nilitangaza amaneno yangu kwenu, ambayo yaliandikwa na mtu huyu, kama mmoja banayelia kutoka kwa wafu, ndiyo, hata kama mmoja asemaye kutoka cmavumbini?

28 Ninatangaza vitu hivi kwa kutimiza unabii. Na tazama, yatatoka nje ya mdomo wa Mungu asiye na mwisho; na neno lake alitaenda mbele kutoka kwa kizazi hadi kingine.

29 Na Mungu atawaonyesha, kwamba yale ambayo nimeandika ni ya kweli.

30 Na tena ninawashauri kwamba amngekuja kwa Kristo, na kushikilia juu ya kila karama nzuri, na bmsiguse ile karama mbovu, wala kitu kichafu.

31 Na aamka, na kutoka kwenye mavumbi, Ee Yerusalemu; ndiyo, na ujivike mavazi ya kurembesha, Ee binti wa bSayuni; na cimarisha dvigingi vyako na ongeza mipaka yako milele, kwamba ehutachanganywa tena, kwamba agano la Baba wa milele ambalo amefanya kwako, Ee nyumba ya Israeli, liwezekane kutimizwa.

32 Ndiyo, amje kwa Kristo na bmkamilishwe ndani yake, na mjinyime ubaya wote; na ikiwa mtajinyima ubaya wote, na ckumpenda Mungu na mioyo yenu, akili na nguvu zenu zote, basi neema yake inawatosha, kwamba kwa neema yake mngekamilishwa katika Kristo; na ikiwa kwa dneema ya Mungu mnakamilika katika Kristo, hamwezi kwa njia yoyote kukana uwezo wa Mungu.

33 Na tena, ikiwa ninyi kwa neema ya Mungu ni kamili katika Kristo, na hamkani uwezo wake, ndipo ammetakaswa katika Kristo kwa neema ya Mungu, kupitia kwa bupatanisho wa Kristo, ambayo ni agano la Baba kwa ckusamehewa kwa dhambi zenu, kwamba muwe dwatakatifu, bila waa.

34 Na sasa ninasema kwenu nyote, kwa herini. Hivi karibuni nitaenda akupumzika katika bpeponi ya Mungu, mpaka croho yangu na mwili dvitakapounganishwa tena, na niinuliwe juu kwa ushindi kupitia eangani, kukutana na ninyi mbele ya kiti cha enzi cha fkupendeza cha yule gYehova mkuu, hMwamuzi wa Milele wa wanaoishi na waliokufa. Amina.

Mwisho