Maandiko Matakatifu
Yakobo (KM) 6


Mlango wa 6

Bwana ataifufua Israeli katika siku za mwisho—Ulimwengu utachomwa kwa moto—Lazima wanadamu wamfuate Kristo ili kuepuka ziwa la moto na kiberiti. Karibia mwaka 544–421 K.K.

1 Na sasa, tazameni, ndugu zangu, kama vile nilivyowaambia kwamba nitatoa unabii, tazama, huu ndiyo unabii wangu—kwamba vile vitu ambavyo huyu nabii aZeno alizungumza, kuhusu nyumba ya Israeli, ambapo aliwalinganisha na mzeituni, lazima vitimie.

2 Na siku ambayo atanyoosha mkono wake tena mara ya pili ili akuwaokoa watu wake, ni siku ile, ndiyo, hata mara ya mwisho, ambayo bwatumishi wa Bwana wataenda mbele kwa cnguvu zake, dkulisha na kupogoa eshamba lake la mizabibu; na baada ya hayo fmwisho utafika.

3 Na heri wale ambao wametumikia shamba lake la mizabibu kwa bidii; na jinsi gani watakavyolaaniwa wale ambao watatupwa mahala pao! Na ulimwengu autachomwa kwa moto.

4 Na jinsi gani alivyoturehemu sisi Mungu wetu, kwani anakumbuka nyumba ya aIsraeli, mizizi pamoja na matawi; na anawanyoshea bmikono yake siku yote na ni watu wenye cshingo ngumu na ubishi; lakini wale wote ambao hawatashupaza mioyo yao wataokolewa katika ufalme wa Mungu.

5 Kwa hivyo, ndugu zangu wapendwa, ninawasihi kwa maneno ya kiasi kwamba mtubu, na mje kwa moyo wa lengo moja, na amjishikilie kwa Mungu kama vile anavyowashikilia. Na msishupaze mioyo yenu, wakati amewanyoshea bmkono wake wa huruma mchana.

6 Ndiyo, leo, kama mtasikia sauti yake, msishupaze mioyo yenu; kwani, kwa nini amfe?

7 Kwani tazama, baada yenu kulishwa kwa neno jema la Mungu kwa siku yote, je, mtazaa matunda maovu, ili amkatwe na kutupwa motoni?

8 Tazameni, je, mtayakataa maneno haya? Je, mtayakataa maneno ya manabii; na je, mtayakataa maneno yote ambayo yamezungumzwa kuhusu Kristo, baada ya wengi sana kuzungumza kumhusu yeye; na kukana neno jema la Kristo, na nguvu ya Mungu, na akipawa cha Roho Mtakatifu, na kuzimisha Roho Mtakatifu, na kufanyia mzaha ule mpango mkuu wa ukombozi, ambao mmepangiwa ninyi?

9 Je, hamjui kwamba mkitenda vitu hivi, kwamba nguvu za ukombozi na ufufuo, ambazo ziko katika Kristo, zitawaleta kusimama katika akiti cha hukumu cha Mungu kwa aibu na bhatia kuu?

10 Na kulingana na nguvu za ahaki, kwani haki haiwezi kuzuiwa, lazima mtupwe kwenye lile bziwa la moto na kiberiti, ambalo ndimi zake za moto hazizimiki, na ambalo moshi wake unapaa juu milele na milele, ambalo ziwa la moto na kiberiti ni cmateso dyasiyo na mwisho.

11 Ee basi, ndugu zangu wapendwa, tubuni ninyi, na muingie katika amlango uliosonga, na mwendelee katika njia ambayo ni nyembamba, hadi mtakapopokea uzima wa milele.

12 Ee muwe wenye ahekima; niseme nini zaidi?

13 Mwishoni, nawaaga kwa heri, hadi nitakapokutana nanyi kwa furaha katika kiti cha enzi cha Mungu, kiti ambacho kinawatia walio waovu woga na hofu ya akutisha. Amina.