Maandiko Matakatifu
Helamani 12


Mlango wa 12

Wanadamu si waaminifu na ni wapumbavu na ni wepesi kutenda maovu—Bwana huwarudi watu Wake—Ubure wa wanadamu unalinganishwa na uwezo wa Mungu—Katika siku ya hukumu, watu watapata maisha yasiyo na mwisho au laana isiyo na mwisho. Karibia mwaka 6 K.K.

1 Na hivyo tunaweza kuona vile uwongo, na pia kutoaminika kwa mioyo ya watoto wa binadamu; ndiyo, tunaweza kuona kwamba Bwana katika uzuri wake usio na mwisho hubariki na akufanikisha wale ambao huweka bimani yao kwake.

2 Ndiyo, na tunaweza kuona kwa ule wakati anaofanikisha watu wake, ndiyo, kwa kuongeza mavuno yao, na wanyama wao na mifugo yao, na kwa dhahabu, na kwa fedha, na katika kila aina ya vitu vya thamani vya kila aina na umbo; kuachilia maisha yao, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya maadui wao; kugusa mioyo ya maadui wao ili wasitangaze vita dhidi yao; ndiyo, na kwa kifupi, akifanya vitu vyote kwa ustawi na furaha ya watu wake; ndiyo, na hapo ni wakati ambao awanashupaza mioyo yao, na humsahau Bwana Mungu wao, na bkumkanyaga chini ya miguu yao yule Mtakatifu—ndiyo, na wanafanya hivi kwa sababu ya utulivu wao, na mafanikio yao makubwa sana.

3 Na hivyo tunaona kwamba Bwana aasipowaadhibu watu wake kwa mateso mengi, ndiyo, isipokuwa awaadhibishe kwa kifo na kwa vitisho, na kwa njaa na kwa namna yote ya magonjwa, bhawatamkumbuka.

4 Ee jinsi gani wapumbavu, na jinsi gani bure, na waovu, na wenye uibilisi, na jinsi gani hufanya mabaya kwa aurahisi, na jinsi gani watoto wa watu, hufanya mema polepole, ndiyo, huwa wepesi kuyasikia maneno ya mwovu, na kuweka bmioyo yao kwenye vitu vilivyo bure vya ulimwengu!

5 Ndiyo, jinsi gani kwa haraka wanainuliwa kwa akiburi; ndiyo, jinsi gani ni wepesi kwa kujisifu, na kufanya kila aina ya yale ambayo ni ya uovu; na jinsi gani wana upole kumkumbuka Bwana Mungu wao, na kusikiza amri zake, ndiyo, na jinsi gani ni wapole bkutembea kwenye njia za hekima!

6 Tazama, hawataki kwamba Bwana Mungu wao, ambaye aamewaumba, aongoze na bkutawala juu yao; ijapokuwa uzuri wake na rehema yake kuwaelekea, wanachukua kama bure mawaidha yake, na hawataki awe kiongozi wao.

7 Ee ni kubwa jinsi gani hali ya akutokuwa na kitu ya watoto wa watu; ndiyo, hata wako hafifu kuliko mavumbi ya dunia.

8 Kwani tazama, mavumbi ya dunia huvuma hapa na pale, na hata kugawanyika mbali, wakati inavyoamrishwa kufanya hivyo na Mungu wetu mkuu na asiye na mwisho.

9 Ndiyo, tazama kwa sauti yake vilima na milima hutetemeka na akutapatapa.

10 Na kwa auwezo wa sauti yake inavunjika, na kuwa laini, ndiyo, hata kama bonde.

11 Ndiyo, kwa uwezo wa sauti yake dunia ayote hutetemeka;

12 Ndiyo, kwa uwezo wa sauti yake, misingi ya miamba, hutikisika hata mpaka katikati.

13 Ndiyo, na ikiwa ataambia dunia—Songa—itasonga.

14 Ndiyo, na ikiwa ataambia aduniabUtarudi nyuma, ili ciongeze siku kwa masaa mengi—itafanyika;

15 Na hivyo, kulingana na neno lake dunia hurudi nyuma, na huonekana kwa binadamu kwamba jua linasimama mahali pamoja; ndiyo, na tazama, hivyo ndivyo ilivyo; kwani kwa kweli ni dunia ndiyo husogea na sio jua.

16 Na tazama, pia, ikiwa ataambia kilindi cha amaji ya bahari—bKauka—inafanyika.

17 Tazama, ikiwa atauambia huu mlima—aInuka juu, na uangukie mji huo, ili uzikwe—tazama inafanyika.

18 Na tazama, ikiwa mtu aanaficha hazina ndani ya ardhi, na Bwana aseme—Ebu bilaaniwe, kwa sababu ya ubaya wa yule aliyeificha—tazama, italaaniwa.

19 Na ikiwa Bwana atasema—Wewe ulaaniwe, kwamba hakuna mtu yeyote atakayekupata sasa hadi milele—tazama, hakuna mtu atakayeipata kutokea hiyo siku hadi milele.

20 Na tazama, ikiwa Bwana atamwambia mtu—Kwa sababu ya uovu wako, utalaaniwa milele—itafanyika.

21 Na ikiwa Bwana atasema—Kwa sababu ya uovu wako utatolewa kutoka kwenye uwepo wangu—atasababisha kwamba itakuwa hivyo.

22 Na ole kwake yeye ambaye atamwambia hivi, kwani itakuwa kwake ambaye atafanya maovu, na hataweza kuokolewa; kwa hivyo, kwa sababu hii, kwamba binadamu wangeokolewa, toba imetangazwa.

23 Kwa hivyo, heri wale ambao watatubu na kusikiza sauti ya Bwana Mungu wao; kwani hawa ndiyo wale ambao awataokolewa.

24 Na Mungu akubali, kwa utimilifu wake mkuu, kwamba watu waonyeshe nia ya kutubu na kufanya matendo mazuri, kwamba wangerudishwa kwenye aneema kwa neema, kulingana na vitendo vyao.

25 Na ningetaka kwamba watu wote waokolewe. Lakini tunasoma kwamba katika ile siku kuu ya mwisho kuna wengine ambao watatupwa nje, ndiyo, ambao watatolewa kwenye uwepo wa Bwana;

26 Ndiyo, ambao watawekwa kwa hali yenye taabu isiyo na mwisho, kwa kutimiza maneno ambayo yanasema: Wale ambao wametenda mema watakuwa na amaisha yasiyo na mwisho; na wale ambao wametenda maovu watapata blaana isiyo na mwisho. Na hivyo ndivyo ilivyo. Amina.